WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU POLISI JAMII KUKAMATA BODABODA, ASKARI POLISI KUKAMATA VYOMBO VYA MOTO BILA KUVAA SARE ZA JESHI

Na:Tatyana Celestine

 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku Polisi jamii kukamata bodaboda zinazofanya makosa ya usalama barabarani nchini.
 
Pia Waziri huyo amepiga marufuku polisi wa usalama barabarani kukamata vyombo vya moto wakiwa hawajavaa sare za Jeshi.
image 2019 03 08
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro, leo. Lugola yupo Mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
 
Akizungumza na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mafisa, Kata ya Mwembesongo, mjini Morgoro, jana, Lugola alisema Polisi Jamii hawana ujuzi wa kijeshi wa ukamataji wa bodaboda hivyo kuendelea kuifanya kazi hiyo ni kuwanyanyasa wananchi.
 
“Nimepata malalamiko mengi ninapofanya ziara zangu hapa nchini, wengi wanawalalamikia Polisi Jamii kuwaonea, kuwaomba rushwa na kuwakamata pasipofuata utaratibu unaotakiwa kijeshi, hapa Morogoro pia, katika mkutano huu wa hadhara mnayasema yale yale, sasa natangaza kuanzia leo, marufuku Polisi Jamii kukamata bodaboda,” alisema Lugola. 
 
Waziri Lugola pia alipiga marufuku baadhi ya Polisi wa Usalama barabarani ambao wenye tabia ya kutovaa sare za Jeshi na kuingia barabarani au mitaani na kuyakamata magari na bodaboda.
Lugola alisema lazima polisi wafate sheria za usalama barabarani hasa wanapokamata magari yanayofanya makosa, uvaaji wa sare za Jeshi ni muhimu na unapaswa kufutwa.
 
image 2019 03 08
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimfafanulia jambo Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Regina Chonjo (katikati), mara baada ya kumaliza Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, SACP-Wilbroad Mutafungwa.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Waziri Lugola aliongeza kuwa, bodaboda au vyombo vingine vya moto, zinazovunja sheria za usalama barabarani zinapaswa kukamatwa bila kuwaonea huruma, ila ni kosa Polisi kuwanyanyasa vijana hao ambao wanapata ridhiki kupitia biashara hiyo.
 
“Mnapaswa kukamata hizi bodaboda zinapofanya makosa, tabia ya kukurupuka huku mkitafuta fedha zisizo halali, huko ni kuwaonea waendesha bodaboda,” alisema Lugola.
 
Lugola alifafanua kuwa, bodaboda zinazotakiwa kuwepo kituo cha polisi ni zile zilizopo katika makundi matatu ambayo ni Bodaboda zilizohusika kwenye uhalifu, zilizotelekezwa au zilizookotwa na zilizohusika katika ajali.
 
“Bodaboida hizo ndizo zinapaswa kuwepo vituoni, lakini kuziweka bodaboda ambazo hazipo katika makundi hayo, napiga marufuku na hii nataka Polisi nchi nzima munielewe,” alisema Lugola.
Pia Lugola aliwataka waendesha bodaboda mjini Morogoro na Tanzania kwa ujumla wafate sheria za usalama barabarani zikiwemo kuvaa kofia ngumu, kutokubeba abiria zaidi ya mmoja na pia wakiendesha wanapaswa kuwasha taa. 
 
Lugola ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani humo akitembelea Wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilosa na Gairo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake. 
 
Lugola mwaka jana alitoa maagizo kwa makamanda wa mikoa nchini ambayo ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.
 
Waziri Lugola amemaliza ziara Wilaya ya Morogoro na leo ataanza ziara yake katika Wilaya ya Movemero, na Machi 10, 2019 atamalizia Wilaya ya Gairo ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni.
 
 
 

Prof. Robinson Mdegela: Kufikia mwaka 2050 kutakuwa na ongezeko la vifo kutokana na matumizi mabaya ya vyakula

Na:Vedasto George

Kutokana na kuwepo kwa  ongezeko kubwa la magonjwa ya wanyama,mimea  na binadamu  nchini  wadau kutoka Vyuo Vikuu vinavyofundisha  maswala ya  Afya  ya wanyama na binadamu  ikiwemo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)  wamepewa mafunzo ya jinsi   watakavyo  fundisha  somo la Afya Shirikishi (Afya  moja) kwa wanafunzi kuanzia ngazi ya cheti na astashaada.

afya moja 2

Mwezeshaji Mkuu kutoka  Chuo Kikuu cha Afya  Muhimbili (MUHAS) Prof. Japhet Killewo(Kushoto) pamoja na Msimamizi Mkuu wa shuguli za mtandao wa Afya Shirikishi (AFYA MOJA)Prof Robinson Mdengela  (Kulia) wakifuatilia namna mafunzo hayo yanavyoendelea.(Picha na Vedasto George).

 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Msimamizi Mkuu wa shuguli za mtandao wa Afya Shirikishi (AFYA MOJA)Prof Robinson Mdengela Amebainisha kutokana na Bara la Afrika inatarajiwa kufikia mwaka 2050 kutakuwa na ongezeko la vifo kutokana na matumizi mabaya ya vyakula pamoja na kutumia viuwatilifu kwenye mbogamboga hivyo itapelekea magonjwa kama Kansa na Shinikizo la damu.

Aidha amesema kuwa mafanzo hayo yanayotolewa yatakuwa na faida kwa kila eneo hasa vijijini kwani walengwa wa mafunzo hayo ni wale waishio vijijini ambapo maafisa ugani wenye elimu ya afya ngazi ya cheti na astashaada ndio wanaohudumu vijijini  hivyo  itakuwa rahisi kuweza kufikisha elimu hiyo kirahisi kwa walengwa.

afya mojaWashiriki katika mafunzo ya Afya Shirikishi (Afya moja) wakifuatilia mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.(Picha na Vedasto George).

 

Nae Mwezeshaji Mkuu kutoka  Chuo kikuu cha Afya  Muhimbili (MUHAS) Prof. Japhet Killewo  amesema kuwa  kutoka mwaka 2010 wamekuwa wakitoa mafunzo kwa  wadau wanaofundisha maswala ya  Afya  ya wanyama,mimea  na binadamu kwa lengo la  kuona jinsi gani  wanaweza kukabiliana  na changamoto itokanayo na magonjwa ya mlipuko yanayo ambukiza ikiwemo Ebola.

Shabani Mshamu kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Selestina Amos kutoka Wakala wa  mafunzo ya Afya ya Mifugo na uzalishaji (LITA) ni baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakaeleza jinsi watakavyo tekeleza mafunzo kwa vitendo katika maeneo yao ya kazi.

Serikali yatakiwa kushirikiana na wajasiriamali kutatua changamoto zinazowakabili

Na, Catherine Mangula Ogessa

Katika maisha changamoto ni sehemu ya maisha ambayo mtu hupitia katika kuelekea  mafanikio. Wakristu wanaamini kuwa katika maisha hakuna Pasaka pasipo  Ijumaa kuu. Maneno haya yakimaanisha kuwa, daima mtu lazima apitie magumu ili kuweza kufikia kwenye mafanikio. Kauli hii inajidhihirisha ukisoma kwenye maandiko ya  Biblia takatifu katika kitabu cha  Marko 15:34, 37. Marko 16:6, Mathayo 28:5,6.

3.PROFPROF. ESRON KARIMURIBO akifungua mkutano wa wajasiriamali picha na Vedasto George

Inawezekana hata wewe ni mmoja wa watu ambao wamekutana na changamoto katika maisha, lakini hili sio kusudio la ninachotaka kusema katika Makala haya bali ninachotaka kusema ni changamoto wanazokutana nazo wajasiriamali katika kufikia mafanikio kwa yale wanayotamani kuyafanya. Kwanza kabisa msomaji wa Makala haya nikukumbushe kuwa  kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake nyingi na ni wazi kuwa kinachoweza kuzitofautisha  ni  chanzo cha hizo changamoto na namna  ambavyo mtu anaweza kuzitatua pindi zinapojitokeza . 

 2.Bi.Peace mushi mjasirialiamali picha na Vedasto georgeBi.Peace Mushi mjasirialiamali.( picha na Vedasto George.)

Wajasiriamali walio wengi huzitaja miongoni mwa changamoto ambazo zinawakabili kwenye shughuli zao kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji, uhakika wa masoko na nyingine nyingi. Hivi karibuni Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia kituo chake kinacho shughulika na masuala ya jinsia ambacho kinaratibu mpango wa kuendeleza na kuwawezesha vijana na wanawake wajasiriamali wa Tanzania, Kenya na Uganda, hivi karibuni kulikuwa na warsha iliyolenga kubadilishana uzoefu na uelewa kwa wajasiriamali ambao wamenufaika na ufadhili wa kwenda kujifunza nchini Marekani ambapo Michingan State University ndiyo wanaotekeleza mpango huo.

Katika warsha hiyo washiriki waliweza kueleza changamoto ambazo wanakutana nazo katika ujasiriamali wao ambazo ni pamoja na ukosefu wa pesa za kuweza kuendesha shughuli zao, ukosefu wa uwezeshwaji kutoka serikalini lakini pamoja na ushirikiano kutoka kwa jamii.

4.Bi. Enikia Wilfred Bisanda akiwasilisha mchango katika warsha Picha na Vedasto George.1Bi. Enikia Wilfred Bisanda akiwasilisha mchango katika warsha Picha na Vedasto George

Wakibadilishana uzoefu washiriki hao walibainisha kuwa miongoni mwa mambo ambayo ni changamoto kwao waliyoyabainisha kutoka nchini Tanzania ambayo ni tofauti na Marekani, miongoni mwa wanufaika wa ufadhili wa kwenda kujifunza nchini Marekani ni Bi. PEACE MUSHI ambaye ni mjasiriamali katika kilimo na ufugaji alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo wameyaona nchini Marekani ni pamoja na Serikali kuwa karibu zaidi na wajasiriamali , ambapo kwa hapa Tanzania ni tofauti.

“ Marekani serikali imekuwa ikishirikiana na wajasiriamali katika kupanga mambo yao kuhusu shughuli za kijasiriamali, kuwapatia wataalam, kusaidia katika kutangaza, namna ya kupata wateja wa bidhaa zao, pamoja na kuweka mipango yao”, alisema Bi. Peace Mushi.

Katika kukabiliana na changamoto washiriki hao waliiomba Serikali kukaa karibu na wajasiriamali ili waweze kujua changamoto zinazo wakabili na baadae kuweza kuangalia njia ya kuzitatua changamoto hizo kwani changamoto nyingi ambazo wajasiriamali wamekuwa nazo inawezekana hazifahamiki kwa serikali.

5.Daktari John Jeckoniah1Daktari John Jeckoniah.

Kauli hiyo imetolewa na wanufaika wa mpango wa kuwaendeleza na kuwawezesha vijana na wanawake wajasiriamali wa Tanzania, Kenya na Uganda ambao walipata ufadhili wa ziara ya mafunzo kwa wajasiriamali kwenda wiki nne za mafunzo nchini Marekani.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  PROF. ESRON KARIMURIBO aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuhakikisha wanajifunza njia za namna ya kujiajiri wenyewe lakini pia kutafuta namna ya kuzibadilisha changamoto kuwa fursa.

“Warsha hii ilete manufaa kwenu kwa kila upande kuhakikisha inawaunganisha wajasiriamali na wabunifu ili kila upande uweze kujifunza kwa mwenzake na hatimaye mjifunze namna ya kuweza kupata ajira”, alisema Prof. Esron Karimuribo.

1.Washiriki wa warsha ya wajasiriamali picha na Vedasto GeorgeWashiriki wa warsha ya wajasiriamali picha na Vedasto George

Pamoja na changamoto hizo lakini pia watu wengi wamekuwa hawawezi kuthubutu kufanya jambo wakihofia kushindwa lakini Bi.  Enikia Wilfred Bisanda ambaye ni miongoni mwa wanufaika wa ufadhili huo wa ziara ya mafunzo aliwataka vijana pamoja na wanawake kuacha woga wa kujihusisha kwenye masuala ya biashara pamoja na ujasiriamali kwa kuhofia  changamoto ambazo zinaweza kujitokeza  na badala yake wathubutu kufanya kile walichonacho.

“Vijana na wanawake ni muhimu wahakikishe wanathubutu kwani wakifanya hivyo watajua namna ya kukabiliana na changamoto, lakini pia itawasaidia kujua wafanye nini ili kuweza kuzalisha kulingana na mahitaji ya soko” , alisema Bi. Enikia Wilfred Bisanda.

 

Katika hatua nyingine Bi. Sanda amewataka kuhakikisha wanakuwa wanashiriki semina pindi wanaposikia kuna fursa hizo kwani semina hizo zitawajenga katika masuala ya ujasiriamali

Awali akielezea washiriki wa mpango huo mratibu wa mpango huo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA ambapo wao wamekuwa wakiratibu na watekelezaji wake wakiwa ni Michingani State University Daktari John Jackonare ambaye pia ni mratibu katika kituo cha masomo ya jinsia amesema kuwa kwanza kabisa mpango huo unashirikisha vyuo vikuu vitatu ambavyo ni SUA cha Tanzania, Nairobi cha Kenya pamoja na Kyambogo cha nchini Uganda.

NDAMA ALIYEZALIWA NA PUA MBILI AMEFIKISHWA SUA KWA MATIBABU

Na Amina Hezron,Morogoro

Ndama wa ajabu mwenye pua mbili ameezaliwa jana katika Gereza la Mbigiri wilayani Mvomero na kufikishwa leo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Akizungumza na SUAMEDIA, Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya Prof. Donald Mpanduji amesema kuwa walipokea taarifa ya kuzaliwa kwa ndama huyo kutoka katika gereza la Mbigiri na kuagiza ndama huyo kuletwa katika Kliniki ya Mifugo ambayo pia ni ya Rufaa chuoni hapo.

picha tatu

Mkuu wa Rasi wa Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za afya Prof. Donald Mpanduji wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) akitoa maelezo juu ya ng'ombe wa ajabu aliyefikishwa katika Kliniki ya Rufaa ya wanyama SUA.

 

Prof. mpanduji amesema lengo la kuagiza ndama huyo kuletwa ni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ambapo pia amesema tatizo hilo ni la kawaida kwa mnyama kutokea.

Prof. Mpanduji amefafanua kuwa hii ni mara ya kwanza kwa tatizo kama hilo kuripotiwa katika kliniki hiyo hivyo ndama huyo kwa sasa atafanyiwa uchunguzi ili iweze kutambulika ukubwa wa tatizo lake hasa katika njia ya mfumo wa hewa na chakula.

picha ya Ndama

Ndama wa ajabu mwenye pua mbili aliyezaliwa katika Gereza la Mbigiri wilayani Mvomero amefikishwa katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwaajili ya uchunguzi zaidi.

 

Aidha Prof Mpanduji amewataka wafugaji wanapokutwa na matatizo kama hayo kwa wanyama kutokimbilia kuhusisha na Imani za kishirikina na kuripoti katika sehemu za taaluma ikiwemo katika Kliniki hiyo iliyopo katika Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi za Afya kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu na kuwataka pia wafugaji kufata ufugaji bora wa wanyama.

MRADI WA RIPAT SUA WAWAWEZESHA WAKULIMA MOROGORO

Na: Bujaga I. Kadago

Wanachuo wanaosomea shahada ya usimamizi katika  wa miradi chuoni SUA wameridhika na matokeo ya mfumo shirikishi wa kuleta mapinduzi ya kilimo RIPAT baada ya kujionea shughuli za kilimo na ufugaji katika wilaya ya Mvomero.

kakaaa

Mwenyekiti wa Kikundi cha Twawave Bwana Jerome Jacob kutoka Kijiji cha Mnyanza Kata ya Tangeni akifafanua jambo kwa wanafunzi wanaosomea Shahada ya Uzamili ya Usimamizi katika  wa miradi SUA.

Ziara hiyo ya Wananchuo wa SUA  kutembelea vijiji vya Changarawe,Tangeni,Kauzeni na Mnyanza katika Wilaya ya Mvomero na Manispaa ya Morogoro ilikuwa sehemu ya mafunzo kwa vitendo baada ya kusoma nadharia ya mfumo huo wa RIPAT

kijanaaMhadhiri wa SUA Dkt. Goodluck Masawe  aliyeambatana na kundi la kwanza la wananfunzi hao walio nyuma yake akizungumza na wanakikundi hawapo pichani.

Mmoja wa wanachuo hao Bwana Mrutu Ally amesema mfumo huo wa RIPAT ni rahisi na sahihi katika kuhamasisha teknolojia kutoka kwa watafiti na kuzipeleka kwa wakulima wadogo vijijini ambapo matokeo yake ni Dhahiri kwani mikungu ya migomba ni mikubwa.

mgomba 

Shamba la migomba la kikundi cha NURU katika Kijiji cha Changarawe Mvomero.

Aidha wanachuo hao wameridhishwa na mfumo wa uanzishwaji vikundi, uchaguzi wa aina ya zao wanalopenda kulilima na pia mfumo wa mafunzo ya vitendo katika kufundishwa teknolojia mpya za kilimo na ufugaji wanazopelekewa.

 

VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ILLINOIS MAREKANI WATEMBELEA SUA

Na: Bujaga I. Kadago

Viongozi waandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Illinois na wengine kutoka Benki ya chakula ya Midwest ya nchini Marekani wamefanya ziara ya kikazi katika Chuo kikuu cha  Sokoine cha kilimo SUA ili kubaini fursa na maeneo ya ushirikiano baina ya taasisi hizo.

kipimoMtekinika Mwandamizi Bw. Jackson Bagilisha akitoa maelezo kwa wageni kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Illinois  nchini Marekani kuhusiana na Utafiti wa ubora wa afya ya mbegu wakati wa Ziara yao Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.(Picha na Tatyana Celestine)

Ujumbe huo kutoka Chuo cha Illinois ukiongozwa na Dr. Larry Dietz ambaye ni Rais wa Chuo hicho na Bw.Ralf Endress  kutoka Benki ya Chakula ya Midwest, umepokelewa na mwenyeji wao Makamu wa Mkuu wa chuo cha SUA Prof. Rafael Chibunda pamoja na  Viongozi wengine waandamizi wa chuo.

Akizungumza kwa niaba ya  Makamu wa Mkuu wa chuo, Mhadhiri Mwandamizi Idara ya Teknolojia ya Chakula na Sayansi ya Lishe na Mlaji Dr. Kisa Kulwa amesema ujumbe huo ni muhimu kwani utafungua fursa katika maeneo mbalimbali ikiwemo Nyanja za utafiti,ufundishaji na ubadilishanaji wa wakufunzi na wanafunzi baina ya vyuo hivyo kwa lengo la kupata uzoefu na changamoto mpya.

 

mkonoWageni kutoka Chuo Kikuu cha Illinois cha nchini Marekani wakielezea faida waliyoipata kutembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA. (Picha na Tatyana Celestine)

Aidha Dr. Kisa amesema kuwa  Chuo kinatambua mahitaji ya jamii hususani katika kilimo hivyo chuo kinaendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kutoa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.

shambaaMtekinika Mwandamizi Bw. Jackson Bagilisha akielezea jinsi teknolojia ya uzalishaji wa migomba kwa wingi inavyofanyika na hatua zake katika Kitalu nyumba kimojawapo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).(Picha na Tatyana Celestine)

Ziara hiyo imekamilika Alhamis  Jan 31,2019 kwa majadiliano ya maswala mbalimbali pamoja na kutembelea baadhi ya idara ikiwemo Idara ya Sayansi ya Uhandisi na Teknolojia na  Kituo cha Utafiti wa Ubora na Afya ya mbegu.

WAKULIMA WATAKIWA KUITUMIA MAABARA YA UDONGO YA SUA ILI KULIMA KWA UFANISI

Na: Farida Mkongwe

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeahidi kuendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA  katika kuhakikisha chuo hicho kinatimiza majukumu yake ipasavyo hasa yale yanayohusu kilimo.

nyambiMkuu wa Idara ya Sayansi ya Udongo Dr. Nyambilila Amor akitoa maelezo kwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe, Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Peter Gillah wakati wa ziara ya Naibu Katibu huyo yenye lengo la kujionea namna maabara ya udongo SUA  inavyofanya kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa James Mdoe wakati alipofanya ziara katika Maabara ya Udongo iliyopo Idara ya Sayansi ya Udongo SUA kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika maabara hiyo.

Prof. Mdoe amesema serikali inashirikiana na vyuo vikuu nchini ikiwemo SUA katika kuhakikisha vyuo hivyo vinatimiza majukumu yake na tayari makubaliano yameshafanyika ya kuangalia namna ya kuvisaidia vyuo hivyo.

mlee

“Nimefika na kujionea maabara nzuri ya udongo namna inavyofanya kazi sisi tumejipanga kuwasaidia jambo la msingi nawashauri wakulima wazitumie maabara hizi ili waweze kulima kilimo chenye tija kwa sababu ili kuzalisha kwa ufanisi ni lazima kujua aina ya udongo unaohitajika”, alisema Prof. Mdoe.

Naibu Katibu Mkuu pia ametembelea nyumba za uatamizi katika mradi unaoendeshwa na SUA kwa kushirikiana na shirika la PASS na kuwapongeza SUA pamoja na vijana waliojitokeza kushiriki katika mradi huo ambao utawawezesha kupata maarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazohusu kilimo.

Kwa upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amemueleza Naibu Katibu Mkuu changamoto kubwa iliyopo katika maabara ya Udongo kuwa ni upungufu wa wataalamu wa maabara na kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo chuo kimeajiri wataalamu wawili kwa malipo ya ndani jambo ambalo limepongezwa na Prof. Mdoe.

 

SUA imewakutanisha wadau wa mnyororo wa thamani wa wakulima wa Alizeti na wafugaji wa kuku

Na: Calvin Gwabara

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na wadau wengine kimewakutanisha wadau wa mnyororo wa thamani wa wakulima wa Alizeti na wafugaji wa kuku kwa lengo la kujadili changamoto zinazozikabili sekta hizo na kuweka mikakati ya kuzitatua ili kuongeza tija kupitia mnyororo wa thamani.

mbeleeWadau wa Mnyororo wa Thamani  wa zao la Alizeti na Ufugaji kuku wakiwa kwenye mkutano wa wadau wote kujadili namna ya kujenga mashirikiano .   (Picha na Calvin Gwabara)

Akizungumza nje ya mkutano huo Mratibu wa Programu ya Building Stronger Universities  BSU kwenye kitengo kinachosimamia mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo Dkt. Daniel Ndyetabula Kutoka Shule Kuu ya Uchumi Kilimo na Stadi za Biashara amesema kuwa hivi sasa wanafanya utafiti wa kuangalia mnyororo wa thamni na namna ambavyo wadau wanaweza kushirikiana.

Amebainisha kuwa wameitisha mkutano huo kwa kuwajumuisha wadau wanaofanya kazi kwenye mnyororo wa thamanii wa kuku na zao la alizeti ili  kuona namna wanavyoweza kushirikiana katika kujadili namna bora za kutatua changamoto za mnyororo wa thamani.

unenee (Picha na Calvin Gwabara)

Amefafanua kuwa matarajio yao makubwa  yalikuwa ni kufikia maazimio ya namna bora ya kushirikiana kati ya watafiti na wadau na kupitia mkutano huo  wamefanikiwa kutengeneza mpango bora wa mashirikiano ambao utatoa dira ya namna ya sekta hizo zitakavyoweza kutoa tija inayokusudiwa.

“Vigezo vilivyotumika  kuchangia mnyororo wa thamani wa alizeti na kuku ni kutafuta sekta ambazo zinaweza kutoa ajira kwa watu wengi ndio maana tukaona tuanze na kuku na alizeti kwa  kuwa sehemu hizo zina uwezo wa kutoa ajira nyingi kuliko zingine”, alisema Dkt.Ndyetabula.

Kwa upande wake Julie Mkambaita ambaye ni Afisa Mtendaji wa Chama cha Wasindikaji wa Alizeti mkoa wa Manyara na Prince Mosha amesema kuwa Kilimo cha alizeti kinakabiliwa na changamoto nyingi hususani mbegu bora kulingana na maeneo hivyo watafiti kuamua kusimamia zao hilo kutasaidia kupatikana kwa  ufumbuzi wa changamoto hiyo.

muzungu (Picha na Calvin Gwabara)

Naye Mwenyekiti wa Ushirika wa Wafugaji wa Kuku mkoa wa Morogoro amekishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine na wadau wengine kwa kuitisha mkutano huo ambao umeweka mikakati ya namna ya kuboresha na kuinua sekta hiyo inayokuwa kwa kasi.

Amesema kupitia ushirikiano huo wafugaji wa kuku wataweza kupata taarifa muhimu za masoko na kupata mbinu bora za ufugaji kutoka kwa watafiti hao tofauti na hivi sasa ambapo kila mtu anaingia kwenye ufugaji bila kujua undani wa biashara hiyo.

 

Jamii imeshauriwa kuwa waangalifu katika kuepuka  ajali zinazoweza kujitokeza majumbani kutokana na wanyama wapya wawafugao

Na: Josephine Mallango

Jamii imeshauriwa kuwa waangalifu katika kuepuka  ajali zinazoweza kujitokeza majumbani hasa wanapoleta wanyama wapya kwa kuwa wanyama hao wanakuwa hawajazoeana na wanadamu na wanyama wengine waliopo katika eneo hilo.

Ushauri huo umetolewa na Daktari Mkazi  katika Hospital ya Rufaa ya Wanyama SUA Dk. Isaac Kashoma  wakati wakiwa katika maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa mguu  mnyama aina ya mbwa aitwaye Bobi aliyejeruhiwa vibaya na mbwa wengine wenyeji.mbwaa

 Mbwa aliyejeruhiwa na Mbwa wenzie akifanyiwa upasuaji mara baada ya kufikishwa katika Hospital ya Rufaa ya Wanyama SUA 

Mbwa huyo jike anasadikiwa kuwa na umri wa kati ya miezi 4 au 5  ambaye ana majeraha makubwa shingoni unayoweza kusema amekatwa kwa mapanga au amenusurika kuchinjwa huku akiwa amevunjika mguu wa mbele wa kushoto ambaye alishambuliwa na mbwa wenzake.

Akisimulia mkasa huo daktari mkazi Isaac Kashoma amesema walimpokea mbwa huyo siku ya jumatano iliyopita jioni akiwa na hali mbaya na ndipo walimlaza wodini na kuanza kumpa huduma ikiwepo ya dripu za maji na kupigwa X-Ray ambapo alifanyiwa upasuaji na sasa anaendelea vizuri.

shingoo

 

Katika hatua nyingine Dk. Kashoma amesema kwa sasa jamii imekuwa na mwamko wa kuhudumia wanyama wanaofungwa  majumbani tofauti na miaka ya nyuma kutokana na ongezeko la wanyama wanaotibiwa katika hospital ya rufaa ya SUA kuongezeka ikiwa ni kutoka mkoani morogoro na nje ya Morogoro ikiwemo jijini Dar es Salaam.

kidonda Mbwa aliyejeruhiwa na Mbwa wenzie akionekana mara baada ya  kufanyiwa upasuaji katika Hospital ya Rufaa ya Wanyama SUA 

 

Ameongeza kuwa  wafugaji wanaotibu wanyama ni wa hali zote na idadi kubwa ni watu wa kawaida na hasa watoto wanaoleta mbwa  wao katika utaratibu wa kawaida wa kuwaosha na chanjo siku ya jumamosi huku idadi inayofuata ni wale wenye kipato cha kati  wanaoleta mbwa wenye magonjwa ya kutibiwa na kuondoka na wengine ni wale wanaoleta mbwa kwa ajili ya kulazwa na upasuaji.

 

SUA ni moja kati ya vyuo vinavyotoa elimu bora ya masomo ya Sayansi Afrika na Duniani

Na: Joel Memba

Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Sokoine cha Kililmo SUA  Prof. Peter Gillah amewahakikishia wanafunzi waliochagua kujiunga na masomo ya shahada ya juu kuwa Chuo kitahakikisha kinawasaidia kufikia malengo katika mafanikio yao ya kielimu

Prof. Gillah amesema hayo katika siku ya ukaribisho na utambulisho wa kuyajua mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa “New Lecture Theater”  uliopo Kampasi Kuu ya chuo hicho huku  ikihudhuriwa na wakuu Ndaki,Shule ya Uchumi Kilimo,Wakurugenzi mbalimbali wa Taasisi na Viongozi wengine wa Chuo.karimuribo

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Peter Gillah akijadili na Mkurugenzi wa Uzamili,Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri SUA Prof. Ezron Karimuribo  

 

Prof. Gillah amesema kuwa  SUA ni moja kati ya vyuo vinavyotoa elimu bora ya masomo ya Sayansi Afrika na Duniani hivyo wanafunzi waliopata fursa ya kuchaguliwa ni muhimu wafuate kanuni, sheria na taratibu za kimaadili za Chuo ili kufikia malengo yao kitaluma na kimaisha.

 

washiriki

Viongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA pamoja na wanafunzi walioshiriki katika siku ya ukaribisho na utambulisho wa kuyajua mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa “New Lecture Theater”  uliopo Kampasi Kuu.

Prof.Gillah amewataka wanafunzi hao kushiriki kikamilifu katika michezo,dini na maswala mengine ya kijamii bila kuathiri lengo la msingi la kitaaluma na kusisitiza kuwa huduma za kimatibabu,maabara na maktaba kuwa zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uzamili,Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri Prof. Ezron Karimuribo amewakumbusha wanafunzi waliopokelewa kujiunga na masomo ya shahada ya juu kutambua wajibu wao binafsi, kwa familia,Taasisi na Taifa na kuepuka mambo yanayoweza kupelekea kufukuzwa chuoni.

group

Katika picha ya pamoja Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma SUA Prof. Peter Gillah wa tano kutoka kulia mstari wa mbele, Viongozi na Wanafunzi katika siku ya ukaribisho na utambulisho wa kuyajua mazingira iliyofanyika katika ukumbi wa “New Lecture Theater”  uliopo Kampasi Kuu

Wanafunzi SUA wajengewa uzoefu katika Sekta ya Utalii

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza hadi wa tatu wanaosoma Shahada ya Utalii katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wamepanda mlima Uluguru hadi katika eneo la Morning Site linalomilikiwa na Chuo hicho kwa lengo la kufanya mazoezi kwa vitendo na kujifunza mbinu za kuongoza watalii kwenye maeneo ya milima.

IMG 8302

Akiongea na SUAMEDIA Mkuu wa Idara ya Utalii na Mapumziko uishi Dkt. Agnes Sirima amesema kuwa idara hiyo imekuwa ikiwafundisha wanafunzi hao nadharia lakini pia huwawezesha kwenda katika maeneo ya kitalii ya aina mbalimbali kwa lengo la kupata uzoefu wa kutosha kabla hawajamaliza masomo yao na kuingia kwenye soko la ajira.

“Tunaposema utalii wa kupanda kwenye milima,shughuli za utalii, uongozaji watalii na ushirikishwaji wa jamii katika utalii na vitu vingine vingi katika sekta ya utalii lazima wanafunzi wajifunze kwa matendo, hivyo tumekuja nao kuwaonyesha kituo hiki cha Morning site ili wajue kipo kwenye idara yetu na waweze kukitumia kwa ajili ya mafunzo yao ya utalii” alisema Dkt. Sirima.

Amesema hii ni mara ya pili wamekuwa wanawapelekea wanafunzi katika eneo hilo lakini mwaka huu muitikio umekuwa mkubwa tofauti na mara zingine kwani wanafunzi na waalimu wao wamejitokeza kwa wingi na anaamini zoezi hilo litakuwa endelevu ili kusaidia kuwa na wahitimu bora.

Dkt. Sirima amesema hii inawajengea wanafunzi hao ambao wanatarajiwa kuja kuongoza watalii baadae kujiamini na kujua ni vitu gani vya muhimu wanapaswa kuvizingatia kabla ya kupanda mlima na watalii ikiwa ni pamoja na kufikia malengo ya mtalii kwa kumuandaa kikamilifu kwa mavazi,viatu na vitu vingine.

Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi wa kozi hiyo Irene Ibrahim amesema kuwa imemjengea uwezo wa kujua changamoto za upandaji milima na kujua mambo muhimu anayopaswa kufanya kabla ya kuanza kupanda mlima peke yake au pale atakapokuwa anaongoza mtalii katika kupanda mlima.

Amesema awali hakuzingatia aina za mavazi na viatu anavyotakiwa kuvaa wakati wa kupanda mlima hali ambayo imemfanya yeye na wanafunzi wengine kupanda mlima huyo kwa tabu kutokana na viatu na mavazi waliyovaa kutokuwa sahihi.

Kwa upande wake mratibu wa safari hiyo ya mafunzo Dkt. John Ngonja amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati SUA na vyuo vingine nchini ambavyo vinatoa kozi ya utalii kwani chuo hicho kipo karibu na asili na hivyo kutoa fursa nzuri kwa wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo na hivyo kuwa bora kuliko vyuo vingine.

Amesema msisitizo wa kozi wanazozitoa ni tofauti kwani wanajitahidi kuwafundisha utalii wa asili kwahiyo hiyo ni sehemu ya kutambua asili kwa kutoa kozi za Utalii wa Wanyamapori, Masoko na utalii, Uchumi,Ukarimu na Uongozaji Watalii.

Wakulima wa Kanda ya Mashariki wametakiwa kuchukua tahadhari

Na: Tatyana Celestine 

Wakulima wa Kanda ya Mashariki wametakiwa kuchukua tahadhari ili kuepukana na panya waharibifu wa mazao katika kipindi hiki cha mvua ambapo panya hao huleta uharabifu unaoweza kufikia asilimia 100.

Hayo yamesemwa Januari 17 na Prof Loth Mulungu kutoka Kituo cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisi kwake.

Prof. Mulungu amesema wakulima wengi hivi sasa wamenza kupanda mazao ya chakula lakini kama watachukua hatua za tahadhari wanaweza kujikuta wanapata hasara kubwa na kushindwa kunufaika na kilimo.

pori panyaPicha na Mtandao

Amesema ni muhimu wakulima waache kilimo cha mazoea ambacho huona kupata hasara ni jambo la kawaida kwani upo uwezekano wa kuzuia uharabifu kwa kusafisha mashamba yao mapema ikiwezekana mwezi mmoja kabla ya kupanda mbegu.

Aidha amebainisha kuwa wale ambao wamekwisha panda mazao yao mashambani pasi kufanya usafi na tayari panya wameanza kuvamizi wanatakiwa kuwaomba maafisa ugani wawape njia bora za kukabiliana na panya hao.

WANAFUNZI WANAOSOMA SUA WAKIWEMO WA KIGENI WABORESHEWA MAZINGIRA YA HOSTELI

Na Gerald Lwomile

Katika kuhakikisha usalama wa wanafunzi wa kigeni ambao husoma Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, Chuo hicho kimefanya ukarabati wa moja ya Hosteli zilizopo chini ya Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE  chuoni hapo jambo ambalo litasaidia kuhakikisha wanakuwa na maisha ya usalama muda wote watakaokuwa SUA.

IMG 8168

Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Chibunda (wa pili kusoto) , na viongozi wengine wa Chuo wakipokea maelezo ya jengo lilikarabatiwa toka kwa Msimamizi wa Kitengo cha Huduma za Mikutano,Hosteli na Mgahawa katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza Dkt. Devotha Kilave wa kwanza kushoto.(Picha na Gerald Lwomile)

Akikagua ukarabati huo Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda amesema SUA itatoa kipaumbele kwa wanafunzi hao ambao wakati mwingine hujikuta wanakaa sehemu ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wao na mali zao.

Akizungumzia ukarabati huo Msimamizi wa Kitengo cha Huduma za Mikutano,Hosteli na Mgahawa katika Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza Dkt. Devotha Kilave amesema ukarabati wa Hosteli hiyo umegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 80 ukijumuisha samani mbalimbali ambazo zimewekwa katika hosteli hiyo.

JENGO

Muonekano wa Hostel iliyokarabatiwa katika Taasisi ya |Elimu ya Kujiendeleza (ICE. (Picha na Gerald Lwomile)

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE Prof. Dismas Mwaseba amemshukuru Makamu wa Mkuu wa Chuo kwa kukubali Taasisi hiyo ifanye ukarabati huo ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia wanafunzi na hasa watokao nje ya nchi kujifunza wakiwa katika mazingira mazuri.

Katika ukaguzi huo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Chibunda aliongozana na Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick Kahimba, Mkurugenzi wa Uzamili, Utafiti na Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri Prof. Esron Karimuribo na Mkuu wa Kitengo cha Uthibiti Ubora SUA Prof. Justin Urassa.

 

LUGOLA AMPA SIKU 30 MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI KUFANYA UKAGUZI TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI NCHINI KAMA ZINA VIFAA VYA ZIMAMOTO

Na Felix Mwagara, MOHA-Biharamulo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto.

PIX 3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Biharamulo, Mkoani Kagera, leo. Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Lugola alisema ukaguzi huo pia ulenge zaidi katika shule za msingi, sekondari na vyuo, vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepukana na ajali zitokanavyo na vyanzo vya moto.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, ambao ulifanyika katika uwanja wa mpira Mjini Biharamulo, Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema atafuatilia utekelezaji wa agizo lake kama litakua limefanyiwa kazi jinsi anavyotaka yeye.

PIX 2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Kagera, Raymond Mwampashe, lipokua anamfafanulia jambo wakati Waziri huyo alipofika katika Gereza la Biharamulo mkoani humo kujua utendaji wa kazi wa Gereza hilo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Pia Waziri Lugola amewaomba Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kununua vifaa za zimamoto katika taasisi za Serikali wanazoziongoza.

“Haiwezekani wanafunzi, wagonjwa katika zahanati mbalimbali au vituo vya afya wapate tatizo la ajali la moto halafu wakurugenzi na mameneja au wakuu wa taasisi hizo wakishindwa kuweka vifaa vya zimamoto licha ya kupokea fedha za kutolea huduma,” alisema Lugola.

PIX 1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, (RPC) Revocatus Malimi (kushoto), wakati Waziri huyo alipopata malalamiko kuhusu ng’ombe za Mkazi wa Mji wa Biharamulo (kulia) kukamatwa na Polisi Wilayani Biharamulo. Hata hivyo, RPC alimfafanulia Waziri huyo kuhusiana na malalamiko hayo dhidi ya mifugo iliyokamatwa na Polisi na kuhifadhiliwa katika Gereza la Biharamulo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

 

Aidha, Waziri Lugola amezitaka taasisi za dini kuendesha ibada kwa kuhakikisha majengo yanasajiliwa na pia Miiskiti na Makanisa yasitumike kuhifadhi wahalifu wanaotumia migongo ya kuwa wachungaji na mashekhe kama mwavuli wa maadili mema bila uzalendo.

“Makanisa na miskiti itakayobainika ina malengo hayo, sitaona haya kuifutia usajili, na pia nawataka viongozi wa dini endapo migogoro inaibuka hakikisheni  mnaitatua wenyewe kwa amani,” alisema Lugola.

Pia Lugola alisisitiza akiitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kupitia upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili waweze kuwabaini  na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Ufunguzi wa Mradi wa Mafunzo kwa Vijana ya kujenga Vitalu Nyumba na Uzalishajiwa Mazao ya Mbogamboga Kibiashara kupitia Vitalu Nyumba

bango

fredrick kahimbaNaibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick Kahimba akiongea kwa niaba ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakati wa ufunguzi wa Mradi wa mafunzo kwa vijana ya kujenga vitalu nyumba na uzalishajiwa mazao ya mbogamboga kibiashara kupitia vitalu nyumba chuoni hapo. (Picha na Tatyana Celestine)

kusaini kitabu

Naibu Waziri Watu wenye Ulemavu Bi.Sella Ikupa (katikati), Naibu Waziri Kazi, Ajira Anthony Mavunde (kulia)  wakitia saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kushoto ni Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick Kahimba. (Picha na Tatyana Celestine)mapokezi

Naibu Waziri Kazi, Ajira Anthony Mavunde akipeana mkono na Mkurugenzi wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario mara baada ya kuwasili Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). (Picha na Tatyana Celestine)

mezakuu

 

mita

Naibu Waziri Kazi, Ajira Anthony Mavunde akikagua mita kabla ya kupandikiza nguzo ya kujengea hema la kikaushia mazao (Green house) wakati wa ufunguzi wa Ufunguzi wa Mradi wa Mafunzo kwa Vijana ya kujenga Vitalu Nyumba na Uzalishajiwa Mazao ya Mbogamboga Kibiashara kupitia Vitalu Nyumba. (Picha na Tatyana Celestine)

viazi lishe

Mkurugenzi wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario  akiwaonesha baadhi ya bidhaa ambazo zinazalishwa na SUGECO Naibu Waziri wa Watu wenye ulemavu Bi.Sella Ikupa (katikati) na Naibu Waziri Kazi, Ajira Anthony Mavunde (kushoto). (Picha na Tatyana Celestine)

walemavu waziri

Naibu Waziri wa Watu wenye ulemavu Bi.Sella Ikupa akizungumza wakati wa ufunguzi waUfunguzi wa Mradi wa Mafunzo kwa Vijana ya kujenga Vitalu Nyumba na Uzalishajiwa Mazao ya Mbogamboga Kibiashara kupitia Vitalu Nyumba. (Picha na Tatyana Celestine)

washiriki

Baadhi ya washiriki waliopata mafunzo na walioudhuria katika ufunguzi wa Ufunguzi wa Mradi wa Mafunzo kwa Vijana ya kujenga Vitalu Nyumba na Uzalishajiwa Mazao ya Mbogamboga Kibiashara kupitia Vitalu Nyumba. (Picha na Tatyana Celestine)zege

Naibu Waziri Kazi, Ajira Anthony Mavunde akiweka zege katika nguzo ya kujengea hema la kukaushia mazao(Green House)  katika kufungua Ufunguzi wa Mradi wa Mafunzo kwa Vijana ya kujenga Vitalu Nyumba na Uzalishajiwa Mazao ya Mbogamboga Kibiashara kupitia Vitalu Nyumba. (Picha na Tatyana Celestine)

WAZIRI LUGOLA AWATAKA WANANCHI KUMLETEA KERO KATIKA MIKUTANO YAKE YA HADHARA

Na Felix Mwagara, MOHA-Bukoba.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Bukoba Mkoani Kagera, kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nane kwa kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo akisikiliza kero za wananchi pamoja na kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake.

Waziri Lugola ameanza ziara yake leo tarehe 2, 2019 mjini Bukoba kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, leo, Lugola amesema baada ya kuzungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake pamoja na kupokea changamoto zao, atafanya mkutano mkubwa wa hadhara wa wananchi utakaofanyika uwanja wa uhuru mjini humo ili aweze kusikiliza na kuzitatua kero mbalimbali zinazowakabili.

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru eneo la Mayunga hapa mjini Bukoba, ambapo utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa mji huu wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola.

Pia Lugola alisema lengo la ziara hiyo ni kufuatilia maagizo yake mbalimbali ambayo aliyatoa mwaka jana 2018 katika mikutano yake kama yalifanyiwa kazi na viongozi wa Taasisi anazoziongoza au yalipuuzwa, yakiwemo ya dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia kupiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.

Lugolapic

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma aligundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea.

Waziri Lugola ameongeza kuwa, kupitia mikutano yake ya wananchi mkoani Kigoma ndipo ameamua kufanya ziara ya pili kwa kuutembelea Mkoa wa Kagera ambao changamoto zake zinafanana kwa sehemu kubwa kwa kuwa mikoa hiyo ni ya mipakani na changamoto kubwa ni uwepo wa wahamiaji haramu pamoja na matukio kadhaa ya ujambazi ambayo kwa kiasi kikubwa Serikali inaendelea kuyadhibiti.

“Wananchi wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Dokta Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola.

Waziri Lugola baada ya kumaliza ziara yake mjini Bukoba, ataenda Wilaya za Misenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Januari 8, 2019 atamalizia ziara yake Wilaya ya Muleba ambapo katika Wilaya hizo pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

Uzinduzi wa Bendera ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA

 

MATUKIO KATIK A PICHA 

nde

Bendera ya  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ya kwanza kushoto  ikiwa imepandishwa kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa rasmi.(Picha na Gerald Lwomile)bbendMakamu wa Mkuu wa Chuo Prof.Raphael Chibunda akiongoza zoezi la upandishwaji  Bendera ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa mara ya kwanza.(Picha na Gerald Lwomile)beBaadhi Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakishuhudia zoezi la kupandisha Bendera ya Chuo hicho kwa mara ya kwanza chuoni hapo.(Picha na Gerald Lwomile)woteKatika picha ya pamoja Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA aliyevaa Tai nyekundu mstari wa mbele, Uongozi na baadhi ya Wafanyakazi mara baada ya zoezi la kupandisha Bendera kukamilika.(Picha na Gerald Lwomile)

 

PICHA: Ndege Mpya Airbus A220-300 Ikiwa Tayari Kuletwa Tanzania Kutoka Canada

mnde

Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazindegeNdege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi ikiwa imebatizwa jina la Ngorongoro

nd 

Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazindegg

Mmoja wa wajumbe wa Tanzania akipata maelezo ya Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazingged

Ujumbe wa Tanzania ukiwa na Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi

Njia za kukabiliana na maoni mabaya juu ya kazi yako

Maoni ni sehemu muhimu ya ukuaji wa kazi zako kitaaluma. Huonyesha ikiwa utendaji wako ni mzuri au mbaya na ni maeneo gani unapaswa kuboresha. Kupokea maoni hasi kazini inaweza kuwa ni kitu kigumu kusikia, lakini ni fursa ya kujifunza na kutumia somo utakalolipata kuwa mfanyakazi mzuri zaidi.

Kuweza kugeuza maoni hasi kuwa kitu chanya ni hatua muhimu kwa mafanikio ya kazi yako. Hizi ni njia 6 za kukabiliana na maoni mabaya juu ya kazi yako:

maoni hasi

  1. Jipe Muda Na Nafasi ya Kutosha Kutafakari

Wakati wa ukiwa unapewa maoni juu ya kazi yako, unaweza kuwa na hisia sana. Inawezekana ukashindwa kuendelea kumsikiliza bosi wako au ukachagua kujibishana nae. Hii inaweza kukufanya ukose maelezo ya muhimu au kusababisha kutokuelewana. Ni muhimu kujipa wakati na nafasi ya kutosha ili kuchuja na kupokea vyema maoni hayo. Hii itakusaidia kupata muda mzuri kufikiria juu ya hali hiyo kwa uwazi zaidi na kupanga majibu yanayojiridhisha. Unaweza kuomba muda wa kukusanya mawazo yako kabla ya kujibu maoni hayo..

  1. Tambua Vitu Chanya tu Kutoka kwenye Maoni

Maoni ni kitu muhimu kwa ukuaji wako binafsi na wa kitaaluma. Hata wakiyawasilisha kwa njia nzuri au mbaya, meneja au mfanyakazi mwenzako watakupa maoni mabaya ili uweze kufanya kazi bora zaidi. Ili kusimama imara juu ya taaluma yako, chagua kutenga na kuchukua maoni chanya na ufanyie kazi bora zaidi.

  1. Fikiria ni Kwa Nia njema

Njia nyingine ya kubakia kuwa mchapakazi hata baada ya maoni hasi ni kwa kufikiria juu ya nia njema ya bosi au mfanyakazi mwenzako kwanza. Maoni ni ishara kwamba wanataka kukusaidia kufanya kazi bora ambayo itasababisha kufanikiwa katika kazi yako. Ikiwa utaona kuwa watoa maoni wana nia nzuri na wanaweza kukusaidia kuleta matokeo bora, itakuwa rahisi kwako kufanya mabadiliko mazuri.

4. Sikiliza kwa Makini

Kubishana na mfanyakazi au meneja wako kwa sababu ya maoni yao, hata kama ni hasi haitasaidia. Wanaweza kuwa na mawazo ambayo yangekusaidia kufanya kazi bora, lakini wakashindwa kufanya hivyo. Badala ya kujitetea sana au kupambana na kubishia maoni yao, jaribu kuwasisitiza kwa upole wakupe maelezo zaidi. Uliza maswali kama ‘Unaweza Kunipa ufafanuzi zaidi? Una sampuli ya kazi kama hiyo? Unaweza kunionyesha mfano ili nifanye vizuri zaidi?’ Kwa njia hii, utakuwa na uwezo wa kuifanya kazi hiyo vizuri zaidi.

 

5. Zingatia na Jifunze

Inapotokea unapata matokeo mabaya ya kazi yako pamoja na maoni hasi, unapaswa kuepuka kuanza kuelezea jinsi wengine wamehusika. Itakupotezea muda na kukupunguzia kasi ya kujifunza kutoka makosa na uwezekano wa kurekebisha kosa. Zingatia mpango wako unaofata na tumia fursa hii kufikiria njia ambazo utatumia kurekebisha kazi, tabia na mtazamo wako.

  1. Usiyachukulie Kibinafsi

Kugundua makosa kwenye kazi yako mwenyewe inaweza kuwa kazi ngumu. Unapomaliza, huenda usijue wapi pa kurekebisha na wapi pa kuacha. Hivyo, wakati meneja au  mfanyakazi mwenzako anaelezea makosa hayo, badala ya kuchukia, unapaswa kumshukuru badala yake. Daima kumbuka kwamba hawa wanakosoa kazi yako na si wewe. Kukubali kwa moyo na akili moja maoni hayo, na uulize kama wana wazo bora juu ya namna unaweza kuboresha kazi yako.

Kukosolewa na maoni hasi ni fursa nzuri ya kumwonyesha mwajiri wako kwamba unaweza kubadilika na kufanya mabadiliko muhimu. Unapokosolewa, chukulia kama ni nafasi ya kuboresha utendaji wako na utayari wako wa kurekebisha makosa yoyote.

Subcategories

Page 7 of 44