Wajumbe Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) watakiwa kuwasilisha hoja kwenye Baraza Kuu la Wafanyakazi ili kupatiwa majibu

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimefanya Mkutano wa 115 wa Baraza kuu la wafanyakazi Juni 20 na kujadili
taarifa mbalimbali zinazohusu Chuo pamoja na ustawi wake.

Awali akifungua mkutano huo wa Baraza Kuu la Wafanyakazi  SUA  Mwenyekiti wa Baraza hilo Prof. Raphael Chibunda
aliwataka wajumbe kuimba wimbo wa mshikamano ambao unaoshiria umoja na mshikamano kwa wafanyakazi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo SUA Prof. Chibunda amewataka wajumbe kushiriki kikamilifu
katika kuitisha vikao kwenye mabaraza madogo na kuhakikisha wanawasilisha hoja walizoziibua kwenye mabaraza hayo madogo na hatimaye
kuyaleta kwenye baraza kuu la wafanyakazi la chuo ili yaweze kujadiliwa na kupatiwa majibu.
Aidha amesisitiza kuwa mabaraza ambayo yamekuwa hayana utamaduni wa kukaa yatafutwa endapo yataendelea kutokuzingatia suala la
kukaa kwenye mabaraza hayo madogo ambayo kimsingi yapo kisheria,
Baraza la wafanyakazi hufanyika mara nne kwa mwaka ambapo kupitia mkutano huo wafanyakazi huweza kujadili mambo mbalimbali na
hufanyika wiki moja kabla ya mkutano mkuu wa baraza kuu la Chuo

Mpango kabambe wa mifugo wa Mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022 ni tumaini jipya kwa wafugaji nchini

Na Calvin Gwabara

Wadau wa Sekta ya Mifugo nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mpango kabambe wa mifugo wa Mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022 ili kuwezesha kupunguza uhaba wa nyama

na kuboresha maisha ya wafugaji nchini.
Mtaalam kutoka Dawati la Sekta binafsi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Michael akijibu maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakati wa semina jijini Dodoma.

Wito huo umetolewa na Mtaalam kutoka Dawati la sekta binafsi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Stephen Michael  wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa siku mbili

ulioandaliwa na Jukwaa huru la wadau wa kilimo (ANSAF) kwa lengo la kuwajengea uwezo wanahabari kuripoti na kuishawishi Jamii na Serikali kuwekeza kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi kuboresha
sera inazosimamia.

Mtaalamu huyo amesema Tanzania imekuwa nchi ya pili kuanzisha mlango huo barani Afrika baada ya Ethiopia na hii ni baada ya kuona  Sekta ya Mifugo haijapewa kipaumbele kwenye mipango

ya nchi hususani katika sera husika.

Waandishi wa Habari za mifugo nchini wakifuatilia mada zinazowasilishwa kwenye semina ya lengo la kuwajengea uwezo wanahabari katika kuripoti na kuishawishi Jamii

pamoja na Serikali kuwekeza kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

 
Amesema katika mpango huo waliangalia idadi ya mifugo na Mazao yake na wakaenda mbali zaidi kuangalia  kama idadi ya kila aina ya mfugo unatoa matokeo stahiki kulingana na Mazao tarajiwa.

Mtaalamu huyo kutoka Wizara ya mifugo na uvuvi ameongeza kuwa Mwaka  2016, Sekta ya mifugo na Uvuvi ilichangia asilimia 7.7 ya pato la taifa na ilikuwa kwa asilimia 2.6 huku kaya milioni 4.6

zilionekana kujishughulisha na mifugo.

Aidha ameongeza kuwa  Nyama nyekundu na nyeupe zinachangia kwa asilimia 40% kwenye pato la taifa, Maziwa asilimia 30% huku aina nyingine za Mazao ya mifugo zikichangia asilimia 30.


Amesema kuwa matokeo ya utafiti huo walioufanya wamegundua kuwa mahitaji ya nyama ni makubwa kuliko uzalishaji, vilevile kwenye maziwa lakini changamoto kubwa ni Magonjwa,
malisho, maji pamoja na Mbari (Breed).
 
Washiriki na Viongozi wa ANSAF wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (mwenye miwani mstari wa mbele) Bw.Amos Zephania 
Bwana Michael amesema kufikia mwaka 2032 upungufu wa nyama nyekundu utakuwa tani 1,731,000 Sawa na asilimia 33 ya mahitaji huku eneo lililotengwa kwenye ufugaji ni asilimia 9.4 ya eneo la Taifa.

Ametoa wito kwa waandishi wa habari kujikita katika kutangaza Sekta ya Uvuvi na Mifugo pamoja  fursa zilizopo ili jamii iongeze kasi ya kushiriki na kutumia mazao yake yanayozalishwa kikamilifu

 kutoka kwenye sekta hiyo .

Sekta ya Mifugo inaweza kuchangia zaidi ya asilimia 7.9 ya pato la taifa

Na Calvin Gwabara

Dodoma

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Amos Kulwa Zephania amesema Sekta ya mifugo inaweza kuchangia zaidi ya asilimia 7.9 ya pato la taifa   ya sasa endapo Serikali na wadau wengine watawekeza zaidi katika kuondoa changamoto zinazoikabili sekta hiyo

Amos Kulwa Zephania ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi  wa habari za mifugo nchini kutoka vyombo mbalimbali vya habari iliyoandaliwa na Shirika la ANSAF ili kujadili changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo hapa nchini.

Bwana Zephania amesema pamoja na Tanzania kuwa nchi ya pili kwa wingi wa mifugo barani Afrika baada ya kugawanywa kwa nchi ya Sudan lakini bado mifugo inachangia asilimia ndogo kwenye pato la taifa huku ikikua kwa asilimia 4.9 tu.

Mgeni Rasmi ANSAF

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Mifugo na Uvuvi bwana Amos Kulwa Zephania (Katikati) Akitoa neno kwa wanahabari(hawapo pichani) wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa waandishi nguli wa habari za mifugo nchini kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

“Kwa makadirio yetu mwaka 2020 tutakuwa na Ng’ombe milioni 32.2, Mbuzi milioni 20, Kuku wa asili na wa kisasa watakuwa milioni 79.1 na nguruwe milioni 2 hivyo lazima tujiulize rasilimali  hizi zote zinatusaidia nini na kama uzalishaji wetu wa maziwa kwa mwaka ni lita bilioni 2.7 wakati matumizi yetu ni asilimia 47 kwa mwaka” Alisema Zephania.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa watu hawatumii bidhaa za ndani zinazotoka kwenye mifugo hivyo waandishi wa habari wasaidie kutoa elimu juu ya faida zinazotokana na bidhaa zetu za ndani huku akibainisha kuwa Wizara inafanya mageuzi makubwa kwenye sekta hiyo ili kuhakikisha inatoa mchango unaostahili katika pato la taifa lakini kwa wafugaji na washiriki wa nyororo  wa thamani wa mifugo.

Amesema kupitia oparesheni Zagambo ya kukamata bidhaa feki za mifugo kutoka nje na zilizoisha muda wake ambazo zinaathari kubwa kwa afya ya binadamu kumewezesha kupata zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa mwezi kupitia aparesheni hiyo nchini.

Amesema hivi sasa serikali imekamilisha na kuanza kurekebisha mpango kabambe wa mifugo Tanzania ambao umelenga kuhakikisha afya ya mifugo kwa kuwezesha upatikanaji wa dawa na chanjo za mifugo kwa urahisi ili kufikia soko la kimataifa hasa baada ya kuona mazao mengine ya mifugo hayaruhusiwi kuingia kwenye masoko ya nchi mbalimbali duniani.

Mkurugenzi ANSAF

Mkurugenzi Mkuu wa ANSAF bwana Audax Rukonge akitoa neno kwa wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo.

Pia amesema mpango huo umezingatia swala la kuboresha malisho kwa wafugaji ili kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji pamoja na kuhakikisha swala la uhamilishaji wa mifugo linapewa nafasi ili kupata aina za mifugo inayohitajika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la ANSAF Bwana Audax Rukonge akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo amesema fursa zinaendelea kutokea kila siku lakini watu hawaziangalii na kuzichangamkia.

“Hivi karibuni tunatarajia Afrika kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia na idadi kubwa ya watu watakaokuja watahitaji Nyama, Mayai na Maziwa hivyo lazima tujipange ili wakati huo ukifika na sisi tukauze bidhaa zetu baada ya kukosa fursa kama hiyo mashindano hayo yalipofanyika Afrika ya Kisini” Alisema Rukonge.
Waandishi ANSAF 2

Wanahabari wakifuatilia neno la ufunguzi kutoka kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mifugo na uvuvi.

Mkurugenzi huyo wa ANSAF amesema sekta hiyo inahitaji uwekezaji wa serikali, sekta binafsi na wadau wengine ili iweze kutoa tija inayotakiwa huku akibainisha maeneo ya fursa kuwa ni katika unenepeshaji wa mifugo,Madawa ya mifugo na Chanjo,Uhamilishaji (breeding) pamoja na uzalishaji wa chakula cha mifugo.

Akizungumzia lengo la warsha hiyo ya siku mbili kwa wanahabari hao Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ANSAF Bw. Mbarwa Kivuyo amesema ni kutaka kukumbushana na kuelimishana juu ya changamoto na fursa zilizopo kwenye sekta ya mifugo na kuona namna ya kuzitumia fursa hizo katika kuleta matokeo makubwa.

Subcategories

Page 8 of 51