VIDEO YA RAIS MAGUFULI AKIPONGEZA MFUMO WA MAWASILIANO UTAKAOWASAIDIA WAKULIMA KUPATA TAARIFA ZA KILIMO

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelipongeza shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa kuanzisaha mfumo wa mawasiliano utakaowasaidia wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo nchini.
Rais Magufuli ameota pongezi hizo May 21 wakati wa hafla ya kupokea gawio la Serikali kwa mujibu wa sheria kutoka shirika hilo ambapo limetoa jumla ya shilingi bilioni2.1 Aidha Rais Magufuli ameonesha kushangazwa na Shirika hilo kuendelea kukodisha minara ya mwasiliano katika Mikoa mbalimbali wakati linatakiwa kuwa na minara yake na kuiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Injiania Isack kamwelwe kuhakikisha wanapata fedha ili kujengwa minara watakayopewa TTCL.

KITUO CHA KUFUNDISHIA WAKULIMA VIJIJINI KUJENGWA NA WAKOREA SUA


Chuo Kikuu  Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kimeingia Mkataba wa Makubaliano wa miaka mitano  na Chuo Kikuu cha Yeungnam cha Korea  Kusini  ili kujenga kituo cha kufundishia  wakulima   vijijini  lengo likiwa ni kuendeleza na kuinua  kilimo hapa nchini.
Makubaliano hayo yamefanywa May 20 ambapo Makamu Mkuu wa Chuo cha Yeungnam Prof. Changdeog Huh pamoja na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu  cha Sokoine Cha kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda wamesimamia kutiwa saini Mkataba wa Makubaliano.


Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu  cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amesema kuwa  makubaliano hayo yatasaidia  katika kusambaza teknolojia bora za kilimo vijijini.
 
 
 

Chibunda ameongeza kuwa chuo kitatoa baadhi ya walimu kwenda kusoma shahada ya pili na ya tatu katika Chuo cha Yeungnam cha Korea Kusini ili kuongeza uelewa zaidi katika taaluma zao za kilimo 


Naye Makamu  Mkuu wa Chuo cha Yeungnam Prof. Changdeog Huh  ameipongeza SUA kwa kutoa elimu ya kilimo  na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano  ili kuhakikisha kilimo kinaendelea kutoa mchango kwa Taifa..

 

RAIS MAGUFULI APONGEZA MFUMO WA MAWASILIANO UTAKAOWASAIDIA WAKULIMA KUPATA TAARIFA ZA KILIMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa kuanzisha mfumo wa mawasiliano utakaowasaidia wakulima kupata taarifa mbalimbali za kilimo nchini.

Rais Magufuli ametoa pongezi hizo leo, May 21 wakati wa hafla ya kupokea gawio la Serikali kwa mujibu wa sheria kutoka Shirika hilo ambapo limetoa jumla ya shilingi bilioni 2.1.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema wakulima kupata taarifa mbalimbali ni jambo la msingi ambalo kwa kiasi kikubwa litasaidia wakulima hao kuwa na mafanikio ukizingatia hivi sasa zaidi ya watanzania milioni 23 nchini wanatumia huduma za mawasiliano na hapana shaka wakulima ni miongoni mwao.
Aidha Rais Magufuli ameonyeshwa kushangazwa na Shirika hilo kuendelea kukodisha minara ya mawasiliano katika mikoa mbalimbali wakati linatakiwa kuwa na minara yake na kumwagiza Waziri wa Ujenzi, Mawasilino na Uchukuzi Injinia Isack Kamwelwe kuhakikisha wanatoa fedha ili kujengwa minara watakayopewa TTCL
Rais Magufuli amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kutoa gawio kwa serikali na kuagiza mashirika mengine ambayo hayawezi kutengeneza faida na kutoa gawio ni afadhali yakafungwa
Awali akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Injinia Isack Kamwele amesema mapato ya Shirika la TTCL yameongezeka na ndiyo maana Shirika hilo limefanikiwa kutoa gawio kwa Serikali.
Naye Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba amesema wamefanikiwa kutoa gawio hilo la bilioni 2.1 ikiwa ni ongezo la shilingi milioni mia sita walizotoa mwaka jana na hii ni kutokana na kuongezeka kwa wateja wanaotaka huduma bora kutoka shirika hilo

SUA KUWA KITOVU CHA UZALISHAJI WA CHAKULA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Calvin Gwabara

Morogoro

Serikali ya Ufaransa kupitia Ubalozi wake nchini Tanzania imeahidi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na  wadau wengine katika kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula na malighafi zingine katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Hayo yamesemwa na Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Mhe. Fredrick Clavier wakati wa ziara yake chuoni hapo iliyolenga kujifunza kuhusu mradi wa Kilimo Hifadhi unaofadhiliwa na ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikiana na  Shirika la Misaada la Switzland  (SWISSAID) na kutekelezwa na timu ya watafiti wa SUA,SAT na TOAM ambapo ubalozi huo umechangia kiasi cha EURO 850,000.

IMG 1612

 

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Mhe. Fredrick Clavier akisisitiza jambo katika kikao hicho (Picha na Calvin Gwabara)

“Mradi huu wa miaka mitano unalengo la kuboresha maisha ya wakulima wadogo wapatao elfu 6 na kuhifadhi baioanuai  na mazingira kupitia uzalishaji kwa kutumia kilimo hai, matumizi sahihi ya mnyororo wa thamani wa kilimo hai, kuimarisha vikundi 269 vya wakulima wadogo wadogo, taasisi mwamvuli za vyama hivyo na kuweka kumbukumbu mbinu za kilimo hai zilizokubaliwa na wakulima ili kusaida utetezi  wa kitaifa na kimataifa” Alisema Balozi Fredrick Clavier.

Balozi huyo  ameongeza  kuwa katika mikakati yake anataka kuona kunakuwa na ushirikiano mkubwa kati ya wataalamu wa SUA na kutoka vyuo vingine nchini Ufaransa lakini pia wataalamu na wanafunzi hao waweze kutembeleana pamoja  ili kubadilishana uzoefu.

Amewataka wataalamu wa SUA, FAO, IRD na SWISSAID kukaa pamoja na kuangalia maeneo mawili au matatu ya mashirikiano katika utafiti na  kuandika mradi wa pamoja na kisha kuuwasilisha kwake ili aweze kuuombea fedha kwenye Serikali yake.

Mwakilishi fao

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akiteta jambo na mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bw. Fred Kafeero (Picha na Calvin Gwabara)

Awali akitoa taarifa fupi ya kazi za SUA, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema kuwa Serikali ya Ufaransa ina historia ya muda mrefu na SUA kwani imefadhili baadhi ya miradi hususani mradi wa Kilimo Bustani na ujenzi wa jengo la kufundishia.

“Ujio huu wa Balozi  ni faraja kwa Chuo kwani ni hatua muhimu ya kufungua milango ya ushirikiano zaidi baina ya chuo na Serikali ya Ufaransa katika Nyanja za utafiti na maendeleo katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano ambayo inahimiza uwekezaji ili kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025” Amesema Prof. Chibunda.

IMG 1666

Viongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wakiongozwa na Prof. Chibunda aliyevaa miwani mbele wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Ubalozi wa Ufaransa nchini ulioongozwa na Mhe. Balozi Fredrick Clavier aliyekaa katikati mbele na kushoto kwa Balozi ni mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bw. Fred Kafeero ( Picha Calvin Gwabara)

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani FAO Bw. Fred Kafeero  amesema kuwa FAO Tanzania wapo tayari kuingia kwenye ushirikiano huo na kwamba atatuma wataalamu kutoka ofisi yake ili waweze kukaa na timu ya watu watakaoteuliwa kuandaa mradi huo wa ushirikiano.

Nae mwakilishi mkazi wa SWISSAID Tanzania Bw. Blaise Burnier amesema wao wamesaidia wanafunzi wawili wa shahada ya Uzamivu yaani  PhD kwenye utafiti  unaolenga masuala ya kilimo hifadhi wanaosoma SUA.

Mti wa Mrashia au Mgunga Taveta ni mti ulioingia Tanzania kutoka nchini Kenya

Mti wa Mrashia au Mgunga Taveta ni mti ulioingia Tanzania kutoka nchini Kenya, mti huu ni mti vamizi na umeenea katika mikoa ya Kaskazini kama Kilimanjaro na Mikoa inayozunguka Mkoa huo.

Pamoja na maeneo hayo mti huu unatajwa kuendelea kusambaa nchini na usipothibitiwa unaweza kuleta madhara ya kijamii,kiuchumi na hatari kwa afya kwani unaweza kusababisha ulemavu.

Dr. Charles Kilawe ni Mtafiti kutoka SUA ambaye amefanya utafiti kuhusu mti huo.

FAHAMU NJIA BORA ZA UFUGAJI WA MBUZI

Ili uweze kuwa mfugaji bora wa mbuzi yapo mambo ya muhimu unayopaswa kuyafahamu, mambo hayo yatakusaidia kwa namna moja ama nyingine kuweza kusonga mbele kwenye suala la mafanikio ya kiufugaji.

Yafutayo ndiyo mambo ya msingi ya kuzingatia katika ufuagaji wa mbuzi.

Namna bora ya ufugaji.
1. Wafugwe kwenye banda bora.
2. Chagua  mbuzi kulingana na sifa zao na lengo la ufugaji (uzalishaji) nyama au maziwa.
3. Walishwe chakula sahihi kulingana na umri wa mbuzi.
4. Kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa mifugo hasahasa namna ya udhibiti wa magonjwa hili ni jambo la muhimu sana.
5. Kuweka kumbukumbu za uzalishaji.
6. Kuzalisha nyama au maziwa bora yanaokidhi mahitaji ya soko.

Sifa za banda bora la kufugia mbuzi.
1. Banda bora linatakiwa liwe ni lenye kuweza kuwakinga mbuzi au kondoo na mashambulizi ya wanyama wakali (hatari) na wezi.
2. Liwepo sehemu ambayo maji hayawezi kutuama.
3. Mabanda yatenganishwe kulingana na umri.
4. Liwe na ukubwa ambao linaweza kufanyiwa usafi.

Kama utafuga mbuzi kwa kuwafungia (shadidi) muda wote zingatia yafuatayo:-
1. Banda imara lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya,upepo/mvua.
2. Lenye hewa ya kutosha.
3. Liwe na sakafu ya kichanja na sehemu ya kuwekea chakula na maji.
4. Liwe na vyumba tofauti kwa kuweka vijitoto/wanao ugua/wanao kua.

Ujenzi wa banda la mbuzi.
1. Banda lijengwe kwa kutumia vifaa vilivyopo eneo husika na kwa kuzingatia uwezo wa mfugaji.
2. Kuta ziwe imara na zinazo ruhusu mwanga na hewa ya kutosha.
3. Mlango uwe na ukubwa wa 60X150 sentimeta.
4. Sakafu iwe ya udongo/zege ya kichanja unaweza kutumia mabanzi/mianzi na iruhusu kinyesi na mikojo kudondoka chini.
5. Chumba cha majike na vitoto kiwe na sentimeta 1.25kati ya fito na fito au papi na papi, chumba cha mbuzi wakubwa kiwe na sentimeta 1.9 kati ya mbao na mbao.

KWA HISANI YA MUUNGWANA BLOG

Habari Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 8

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

TANZANIA BARA NA ZANZIBARI UPOTEZA HEKTA 7,218 ZA MISITU KILA MWAKA TANZANIA BARA NA ZANZIBARI UPOTEZA HEKTA 7,218 ZA MISITU KILA MWAKA

Na.Vedasto George.

 Imeelezwa kuwa uchunguzi uliofanywa na serkali kupitia Mradi wa NOPHAM umebaini kuwa Tanzania Bara imepoteza hekta 4,069 za misitu huku Tanzania Visiwani ikipoteza hekta 3,149 kutokana na uharibifu mkubwa wa  mazingira unaofanywa na binadamu ikiwemo kuchoma misitu na kulima karibu na vyanzo vya maji.


Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma SUA  Prof . Peter Gillah akipanda mche wa mti Siku ya Wiki ya Upandaji Miche ya Miti katika mpaka wa SUA uliofanyika katika Kijiji cha Kasanga mkoani Morogoro . (Mpiga picha Vedasto George)

Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Mkoa wa morogoro Bw. Cliford Tandali wakati wa uzinduzi wa wiki ya upandaji miti katika Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo SUA ambapo miti 5,000 imepandwa  katika kijiji cha kasanga kata ya Mindu Mkoani Morogoro.

Aidha imedhiilishwa kuwa maeneo yaliyo ifadhiwa tanzania bara inapoteza kiasi cha hekita takribani 97101 kila mwaka, huu ni uharibifu mkubwa  wa mazingira serkali yetu inaendelea kuchukua hatua kadhaa kupambana na uharibifuu huu ikiwa ni pamoja na kupitia na kuandaa sera mpya ya misitu tanzania alisema Cliford Tandali.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw. Cliford Tandali akipanda mche wa mti Siku ya Wiki ya Upandaji Miche ya Miti katika mpaka wa SUA uliofanyika katika Kijiji cha Kasanga mkoani Morogoro.(Mpiga picha Vedasto George)

Akimwakilisha Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda, Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Taaluma Prof. Peter Gillah amesema kuwa upandaji huo wa miti ni moja ya majukumu ya chuo  katika kuboresha na kuhifadhi mazingira yanayoharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu.

Chuo kikuu cha sokoine cha kilimo hapa  Morogoro kinayo majukumu manne ambayo ni  kutoa mafunzo, kufanya utafiti,kutoa ushauri wa kitaalamu na kuzalisha mali majukumu haya yanatekelezwa katika nyanja mbalimbali hapa chuoni ikiwemo ufugaji, tiba ya mifugo,misitu, usimamizi wa wanyamapori na utalii, ifadhi ya mazingira  na fani nyingine, shughuli ya upandaji miti hapa chuoni ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu shuguli hii kama ilivyo elezwa na Rasi wa ndaki ya misitu wanyamapori na utalii imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu mwaka 1997 ili kuifadhi na kutunza mazingira  yanayo halibiwa na shuguli za binadamu alisema Prof Peter Gillah.
Baadhi ya wanafunzi wa SUA waliojitokeza Siku ya uzinduzi wa Wiki ya Upandaji Miche ya Miti katika mpaka wa SUA uliofanyika katika Kijiji cha Kasanga mkoani Morogoro. (Mpiga picha Vedasto George)

Kwa upande wake Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Prof. Frances John Kessy amesema kuwa tangU mwaka 1997 chuo tayari kimeishapanda miti  578,300 lengo kubwa likiwa ni kuhifadhi mazingira, kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuelimisha jamii juu ya uhifadhi wa mazingira.

Tangu tulivyoanza zoezi hili mwaka 1997 likiongozwa na Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii tumeisha panda miti jumla ya  ekari 328 katika maeneo yanayo tuzunguka ni vipande vidogovidogo lakini ukivijumlisha tayali vimeisha fika ekari 328 ni kiwa na maana jumla  ya miche 578,300 sasa miche hii tumefatilia inaendelea vizuri nyingine tumepanda katika chanzo cha maji kule mindu ambayo inasaidia sana hali ya hewa inakuwa nzuri zaidi na maji yanapatikana kwa wingi zaidi lakini kwenye mipaka yetu ya chuo lakini pia kwenye mashamba ya watu binafusi alisema Prof. Frances John Kessy

Subcategories

Page 10 of 51