Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) imewakutanisha waandishi wa habari na watafiti kutoka Kanda ya Mashariki

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) imewakutanisha kwenye mafunzo waandishi wa habari na watafiti kutoka Kanda ya Mashariki ili kuwajengea uwezo wa kufikisha matokeo ya Sayansi Teknolojia na ubunifu kwa walengwa.


IMG 7644Dkt. Emmanuel Nnko Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Makala na machapisho


Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo ya siku mbili kaumu Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya taarifa Emmanuel Nnko aliyemiwakilisha mkurugenzi Mkuu wa COSTECH amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa jitihada za Tume za kuhakikisha Tafiti zinazofanywa nchini ili ziweze kuleta tija kwa jamii.


IMG 20190912 WA0040 1  Afisa Utafiti Mkuu Kiongozi anayeshughulikia Makala na Machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi akiongea na waandishi wa habari mkoani Tanga.


Akifungua mafunzo hayo yaliyohusisha watafiti na waandishi kutoka Kanda ya Mashariki Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi za utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Zabron Nziku amesema Matokeo ya utafiti ndiyo yanayoweza kusaidia Uchumi wa viwanda endapo yatawafikia walengwa na kuyatumia.

Amesema kuwa tafiti nyingi zinafanywa lakini zinaishia kwenye vituo vya utafiti na hivyo wananchi na wadau wa tafiti hizo kutonufaika nazo wakati zimetumia fedha nyingi.

Amepongeza programu hiyo ambayo inafanywa na COSTECH nchi nzima na kuwataka waandishi wa habari kuyafanyia kazi ili yaweze kusaidia jamii ya watanzania.
IMG 20190912 WA0036
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo Emmanuel Nnko kaimu Mkurugenzi wa Idara ya menejimenti ya Taarifa kutoka COSTECH aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume amesema  mafunzo hayo ni muhimu kwani yanasaidia kuwaleta pamoja wansayansi na waandishi wa habari na kupanga mikakati ya namna wanavyoweza kushirikiana katika kusaidia jamii na Taifa kwa kubuni njia bora za kuwafikishia wadau matokeo ya tafiti hizo.

Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti ambayo yanafanyika nchi nzima ili kusaidia kufikia malengo kufanyika kwa tafiti mbalimbali zinazofanyika nchi nzima kwenye vituo na Taasisi mbalimbali.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo Afisa Programu ya Mafunzo hayo kutoka COSTECH Bw. Merchades Rutechura amesema ni kupunguza gepu kati ya watafiti na watumiaji wa tafiti hizo nchini.

Amesema kuwa toka mafunzo hayo yaanze kwenye kanda mbalimbali kumekuwa na ongezeko kubwa la Makala,vipindi na habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu na hivyo kusaidia jamii kujua ni wapi wanaweza kuzipata ili kuzitumia kwenye shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kuongeza tija.

Amewataka waandishi hao wa Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa  ya Dar es salaam,Pwani, Morogoro na Tanga kutumia kusanyiko hilo kujua miiko ya utoaji wa taarifa na kujenga mashirikiano na watafiti ili kuweza kuwatumia katika uandaaji wa vipindi vyao.

Akiwasilisha mada kuhusu Utafiti na umuhimu wa kutoa matokeo ya utafiti Afisa Utafiti Mkuu kiongozi anayeshughulikia Makala na Machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi waandishi wa habari wana umuhimu Mkubwa katika kufanya kazi hiyo kwakuwa wanasikilizwa na kuaminiwa na jamii.

Dkt. Msangi amesema katika kazi yoyote kuna miiko na maadili yake hivyo waandishi wa habari nao ni lazima wajue miiko na maadili ya kuandika habari na kuandaa vipindi vya Kisayansi na ubunifu ili waweze kufanya kazi hiyo vizuri kwa maslahi ya taifa bila kuleta matatizo kwa mtafiti na mwandishi mwenyewe.

Amesema habari za kisayansi zinahitaji ubunifu kwenye kupeleka kwa walengwa kwa kuandika habari zenye lugha nyepesi, Ufupi na kwa kutumia njia ambayo inaweza kuwafikia walengwa katika eneo fulani iwe Redio,Televisheni au Magazeti.

Dkt. Msangi amesema kuwa mbali na kuwafikia wakulima na wafugaji lakini pia inasaidia kuwafikia watoa maamuzi kutumia

Watafiti wa Tanzania wamegundua mbinu ya kukabiliana na Mbung’o kwa wanyama

Na: Calvin Gwabara

Watafiti wa Tanzania wamegundua mbinu ya kukabiliana na Mbung’o wanaosababisha  vimelea vya was  Nagana kwa wanyama na vimelea vya Ugonjwa wa malale kwa binadamu.

IMG 7485

Mtafiti Deusdedit Malulu akiwasilisha mada yake kwa waandishi wa habari na watafiti kwenye mafunzo hayo jijini Tanga.

Haya yamebainishwa na Afisa Utafiti Mifugo kutoka Wakala wa Maabara za Veterinary Kituo cha Tanga Bw. Deusdedit Malulu wakati wa mafunzo ya uandishi wa habari za sayansi,teknolojia na ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH yaliyowakutanisha waaandishi wa habari na watafiti kutoka kanda ya Mashariki.

Bwana Malulu amesema katika kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na Mbung’o wamebaini mnyama aina ya Kuro hashambuliwi na mbung’o kama wanyamapori wengine na kubaini kuwa mnyama huyo anatoa harufu ambayo mbung'o  huogopa na hivyo kushindwa kumkaribia.
IMG 7582
Amesema baada ya utafiti wao maabara wamebaini kuwa harufu hiyo inauwezo wa kufukuza Mbung’o kwa zaidi ya asilimia 60 ikilinganishwa na teknolojia zingine zilizopo sasa.

Bwana Malulu ameongeza kuwa baada ya kutambua kemikali zilizopo kwenye harufu hiyo ya Kuro wakachanganya kemikali za aina hiyo ili kuizalisha maabara inayofanana na ile ya Kuro na kuwakinga na kushambulia na Mbung'o hao.

Mtafiti huyo amebainisha kuwa ili kuhakikisha harufu hiyo inawafikia walengwa kwa maana ya wafugaji na hivi sasa wanatengeneza kifaa maalum ambacho kitakuwa kinabeba harufu.

“Hivi sasa tunashirikiana na Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha katika kutengeneza kibebeo hicho cha harufu hiyo kwa mifugo” Alisema Bwana Malulu.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya kubuni kibebeo inakwenda sambamba na hatua za kufanya usajili na majaribio katika maeneo husika

HABARI MPASUKO:Robert Mugabe amefariki dunia

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia.

images

Mmoja wa wanafamilia ameithibitishi, Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95.

Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.

Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong'olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho.

"Kamarada Mugabe alikuwa ni mwanga wa mapinduzi, mwana umajui wa Afrika ambaye aliyatoa maisha yake katika ukombozi na kuwawezesha watu wake. Mchango wake kwa taifa letu na bara (la Afrika) hautasahaulika..." ameandika Mnangagwa.

Taarifa zaidi zitaendelea kukujia.

TANAPA YAMPA TUZO MTAFITI WA SUA KWA UTAFITI BORA WA WANYAMAPORI

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA,  Bw. Godwell Ole Meing’ataki amekishukuru  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA kwa mchango
mkubwa wanaoutoa kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi  TANAPA,Bw. Ole Meing’ataki akimkabidhi tuzo   Prof. Rudovick Kazwala kutoka Ndaki ya Tiba ya
wanyama na sayansi za afya yaChuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA
 
Kamishna Ole Meing’ataki ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo kwa   Prof. Ludovick Kazwara kutoka Ndaki ya Tiba ya wanyama na sayansi za
afya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo,SUA iliyofanyika chuoni hapo.
Akikabidhi tuzo hiyo Kamishna Msaidizi wa uhifadhi  TANAPA,Bw. Ole Meing’ataki amekipongeza Chuo pamoja na Uongozi  kwa kupata tuzo hiyo, Pia kwa
mapokezi waliyofanya ambayo yameweka alama ya ushirikiano na umoja katika utendaji kazi nchini.
Amesema Tuzo hizo zinazotambulika kama TANAPA TOURISM AWARDS na ndio mara ya kwanza kutolewa zikiwa na vipengele mbalimbali
ikiwemo  cha kushindania Utafiti uliofanyika kwa muda mrefu ambao umebeba taarifa nyingi zilizosaidia katika Utalii. 
Amesema  kipengele hicho ndicho ambacho   Prof. Rudovick Kazwala ameibuka kinara kutoka kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA. 
Akipokea tuzo hiyo Prof. Kazwala amesema amefurahi sana  kupata tuzo hiyo na hivyo kushauri wadau na wananchi kulinda hifadhi na vivutio mbalimbali
vya Taifa ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na rasilimali hizo.
Amesema Tuzo hiyo ni ishara kwamba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kina mchango mkubwa katika kusaidia uhifadhi wa wanyama na vivutio
vingine vya taifa.
Pia mshindi huyo wa tuzo hiyo  ameomba tafiti zinazolenga kuboresha afya za Wanyamapori na mimea zipewe kipaumbele ili kuweza kuleta tija kwenye
uhifadhi na  utalii nchini.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu kamishna huyo Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Raphael Chibunda amesema tuzo hiyo ni heshima kwa
Mtafiti mwenyewe lakini pia ni hehima kwa Chuo.
Amewapongeza TANAPA kwa kutoa zawadi hizo kwa watu waliochangia kwenye kazi mbalimbali za kutunza na kuhifadhi utalii wa Tanzania kwani inaongeza
chachu ya watafiti na watu wengine kushiriki kwenye kutunza maliasili hizo za taifa.

Prof. Kazwara  ni mtafiti mzawa aliyebobea  ambaye amefanya tafiti ndani ya hifadhi za wanyamapori hasa  tafiti zinazolenga afya za wanyamapori nchini amepata tuzo hiyo kutokana na mchango wa tafiti hizo kwenye masuala ya utalii nchini. 

Uteuzi aliofanya Rais Magufuli jioni ya September 2, 2019

magufulib

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Fredrick Cassian Kahimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Kahimba umeanza 31 Agosti, 2019.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kahimba alikuwa Profesa Mshiriki na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala na Fedha), Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro.

Prof. Kahimba amechukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi.

Subcategories

Page 3 of 51