WATOTO WA KIKE WASIPOPELEKWA SHULE ITAKUWA VIGUMU KUWEKA USAWA WA HAMSINI KWA HAMSINI-KIHANGA

                                        

 Na: Farida Mkongwe

Imeelezwa kuwa iwapo wazazi na hasa wanawake wale wasiopenda kuwapeleka shule watoto wao wa kike hawatabadilika basi itakuwa ni vigumu kufikia malengo ya hamsini kwa hamsini katika nafasi mbalimbali za uongozi ikifapo mwaka 2030.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mstahiki Meya wa manispaa ya Morogoro Bw. Paschal Kihanga wakati akizungumza na wanawake waliokusanyika kufanya usafi katika eneo la Kaloleni lililopo kata ya mji mpya mjini Morogoro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa mkoa wa Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

SERIKALI YAANZISHA MFUMO MPYA WA MALIPO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA

   

Na:TATYANA CELESTINE

SERIKALI imeanzisha mfumo wa Kielektroniki wa malipo ya mishahara kwa watumishi wa umma ambao unalenga kuondoa tatizo la madai ya malimbikizo ya stahili zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Jumamosi, Machi 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali  katika wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu.

  Waziri Mkuu alisema mfumo huo ujulikanao kama LAWSON, unatumika kwenye ajira za watumishi wote nchini, wa Serikali Kuu na wale wa Serikali za Mitaa  

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

NCHEMBA AFANYA ZIARA CHUONI SUA


                              

Na: Alfred Lukonge

Waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba  hivi karibuni ametembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) mkoani Morogoro na kuwataka wanataaluma wa chuo hicho kuwa kamusi kwenye wizara hiyo ili kuleta mabadiliko ya kweli kwenye sekta ya kilimo.

Mh. Nchemba ametoa wito huo chuoni SUA alipokutana na wanataaluma waliobobea katika fani ya sayansi ya mazao,sayansi ya mifugo na sayansi ya ufugaji wa viumbe wa majini na kubainisha kuwa “kuna mambo mengi yanajitokeza ambayo kwa asili ya wanazuoni mnayajua na mmeshayafikisha wizarani lakini utekelezaji wake bado haujafanyika, hivyo ujio wangu hii leo unalenga kuwafanya wanataaluma wa SUA muweze kuhusika moja kwa moja kwenye mabadiliko ya wizara”.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WANAWAKE WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU ILI WAFIKIE MALENGO YAO

    

 

Na: FARIDA MKONGWE

Changamoto imetolewa kwa wanawake mkoani Morogoro kuhakikisha wanajiendeleza kielimu pamoja na kuongeza bidii mahala pa kazi ili kuleta maendeleo yao pamoja na taifa kwa ujumla.

Changamoto hiyo imetolewa na aliyekuwa naibu makamu wa mkuu wa chuo utawala na fedha Pro. Appolinaria Peleka wakati wa sherehe za matendo ya huruma zilizofanyika katika viwanja vya Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA, sherehe ambazo ziliandaliwa na chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi stadi, Habari na Utafiti (RAAWU) tawi la SUA.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

KUELEKEA PASAKA WANAJUMUIYA CHUONI SUA WATAKIWA KUWA MAKINI

 

                      

Na: Susane Cheddy

Idara ya Usalama ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo sua imeonya wanajuiya wa sua kuwa makini kartika kipindi hiki kuelekea sikuu ya Pasaka ili kuhakikisha usalama wao na mali zao.

Wito umetolewa na mkuu wa Idara hiyo afande Ally Ntunguja na kuwataka wanajumuiya hiyo kulinda maeneo wanayoishi ili  kuhakikisha amani na utulivu inatawala katika makazi yao katika kipindi hiki cha sikukuu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAARIFA YA MVUA ZA MASIKA

 

                                     PICHA NA MTANDAO

 

Na: Consolata Philemon

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa utabiri wa mwelekeo wa mvua za masika kwa kipindi  cha mwezi Machi hadi Mei 2016 katika sekta mbalimbali  ikiwepo sekta ya Kilimo na Chakula.

Mkurugezi Mkuu wa  mamlaka hiyo Dk. Agnes Kijazi amesema katika Kilimo na Usalama wa Chakula wakulima wanashauriwa kuendelea na shughuli za kilimo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu za kuongeza uzalishaji, kupanda mazao na miti pamoja na kuzingatia ushauri wa wataalam wa kilimo katika matumizi ya ardhi na mbegu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WANAWAKE WANA UELEWA MDOGO KUHUSU MPANGO WA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA HEWA UKAA - UTAFITI

           

Na: FARIDA MKONGWE

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Misitu (CIFOR), umebainisha kuwa idadi kubwa ya wanawake hawana uelewa wa kutosha kuhusu Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na Ukataji na uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) ukilinganisha na wanaume.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

NAIBU WAZIRI WA AFYA DR KIGWANGALLA AZINDUA WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI MUHIMBILI

  PICHA NA MTANDAO   

Na:TATYANA CELESTINE

Serikali imesema ina mpango wa kusitisha kupeleka wagonjwa nje ya nchi kupatiwa matibabu na kuhakikisha kila kitengo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kinakuwa na chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

MBIO ZA KUWANIA URAISI NCHINI MAREKANI ZAPAMBA MOTO

                                   PICHA NA MTNDAO  

       

Na: Husna Yayha

Muwania kiti cha urais kupitia chama cha democratic Hillary Clinton na mwenzake  wa  Republican Donald Trump wote wameshinda majimbo yote katika siku yao kubwa ya mapambano ya kuwania kuteuliwa kuwania kiti cha urais kupitia vyama vyao.

Shughuli ya kuhesabu bado inaendelea lakini TRUMP hadi sasa ameshinda majimbo saba ikilionganishjwa na yale mawili pekee yaliyochukuliwa na mpinzani wake wa karibu  TED CRUZ na  Marco Rubio.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

MAMILIONI YA SHILINGI KUTUMIKA KWA AJILI YA KUSAIDIA WAKIMBIZI ULAYA

 

                                  PICHA NA MTANDAO

       

Na: Halima Katala na Mitandao

Umoja wa ulaya unatarajia kutumia mamia ya milioni ya EURO kwaajili ya kutoa misaada ya kibinadamu huku ugiriki ikipambana na wimbi la wahamiaji.

Chini ya mpango huo ambao unatarajiwa kuwasilishwa jumatano ya wiki hii Misaada ya umoja wa ulaya inatarajiwa kumiminika kutoka ulaya katika njia zilezile zilizotumika kusaidia nje ya mpaka.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

MPANGO WAANDALIWA KUWEZESHA WANAFUNZI KUJIFUNZA PASIPO KUKAA DARASANI

                                                                       

Na: Adam Ramadhan

Kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia wataalamu wa mbinu za ufundishaji kutoka nchi  tatu duniani wameandaa mpango unaolenga kumuwezesha mwanafunzi wa chuo kikuu kujifunza mwenyewe tofauti na kukaa darasani na kutegemea kumsikiliza mwalimu peke yake.

Wataalamu hao ambao ni walimu wa vyuo vikuu wamekutana katika mkutano wa siku moja uliofanyika katika Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA) mkoani Morogoro  ambapo ndani yake umehusisha wataalamu kutoka nchi ya Tanzania,Ghana na Denmark huku lengo kubwa likiwa kumwezesha mwanafunzi anayesoma chuo kikuu awe na uwezo wa kutatua matatizo katika  jamii  atakayokwenda kuitumikia baada ya maisha ya chuo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

WARSHA YA MPANGO WA KUPUNGUZA UZALISHAJI WA HEWA UKAA KUFANYIKA DAR ES SALAAM

   

                          PICHA NA MTANDAO

     

Na. Farida Mkongwe

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na kituo cha kimataifa cha utafiti wa misitu (CIFOR) kilichopo Nairobi nchini Kenya kimeandaa warsha ya siku moja yenye lengo la kuelezea matokeo ya tafiti kuhusu fursa na changamoto zilizopo katika mradi wa mfumo wa ugawanaji wa faida na mapato yatokanayo na juhudi za utekelezaji wa  Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na Ukataji na uharibifu wa Misitu -MKUHUMI.

Akizungumza na SUAMEDIA mratibu wa mradi huo kwa upande wa Tanzania Dk. Josiah Katani amesema warsha hiyo ya kisera ambayo imehusisha watunga sera kutoka maeneo mbalimbali itafanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumatano tarehe 2 mwezi Machi, mwaka huu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

SHUGHULI ZA MAENDELEO ZATAKIWA KUFANYIKA ILI KUKUZA UCHUMI MOROGORO

                                                                      

                                       PICHA NA MTANDAO

Na: Susane Cheddy

Viongozi mkoani Morogoro wametakiwa kuhakikisha wanafanya shuguhuli za maendeleo ya jamii inayowazunguka kwa wakati ili kukuza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Rajabu Lutengwe ambaye ni mwenyekiti  katika kamati ya ushauri mkoa wa Morogoro katika mkutano uliofanyika eneo la ukumbi wa shule ya sekondari Kilakala februari 27 na kusema kuwa ni wajibu wa kila kiongozi aliyechaguliwa na wananchi kukamilisha mikakati iliyowekwa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

WATANZANIA WATAKIWA KUFUGA NYUKI KISASA ILI KUONGEZA KIPATO- MSALILWA

                                        PICHA NA MTANDAO  

       

Na: Adam Ramadhan

Watanzania  wametakiwa kutumia  njia za kisasa za ufugaji wa nyuki ili  kujiongezea kipato cha haraka kwa muda mfupi  huku  serikali nayo ikishauriwa iweze kuwapatia  elimu ya kutosha wananchi  ili kuongeza uchumi na pato la Taifa.

Hayo yamesemwa na mtaalamu wa nyuki idara ya bailojia ya misitu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kilichopo mkoani Morogoro Bw.Jackson Msalilwa alipozungumza na SUAMEDIA ambapo amewataka watanzania kuyatumia maeneo ambayo hayafai kwa kilimo kuyatumia kwa kufuga nyuki kwa kutumia mizinga ya kisasa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

MITIHANI YA MUHULA WA KWANZA KUANZA LEO CHUONI SUA

                                                                      

Na: Alfred Lukonge

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro leo February 29 wanatarajia kuanza mitihani yao ya mwisho ya kumaliza muhula wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2015-2016, huku baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho  wakitoa maoni yao kuhusu mitihani  hiyo.

Akizungumza na SUAMEDIA Bi. Grace Bilishan anayesoma Shahada ya Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyama Pori mwaka wa tatu chuoni SUA kwa upande wake anaona mitihani itakuwa ya kawaida kwa kuwa amejiandaa vya kutosha kwa kupitia baadhi ya  mitihani ya nyuma ili kujua mtindo wa utungaji maswali ya walimu wao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI MOROGORO

  

                                           PICHA NA MTANDAO

          

Na: Susane Cheddy

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (tamisemi) Mh.George Simbachawene amepongeza uongozi wa manispaa ya Morogoro baada ya kutembelea baadhi ya maeneo ndani ya manispaa na kuridhishwa na shughuli za maendeleo zinazoendelea.

Mh.Simbachawene amesema hayo siku ya jumanne februari 23 katika ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Morogoro na kuweza kutembelea kituo cha mabasi Msamvu ambako ujenzi bado unaendelea na kutoa ushauri kwa wananchi kudumisha amani na utulivu katika wilaya ya Mvomero.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WANANCHI WILAYANI MVOMERO KUPATA HATIMILIKI YA MAENEO YAO.

  

                                             PICHA NA MTANDAO

        

Na: Susane Cheddy

Wananchi wilaya ya Mvomero wametakiwa kuhakikisha wanapata hati za umiliki wa ardhi, nyumba na makazi pamoja na pia kuwa na matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji kuendelea katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na waziri wa ardhi, nyumba na makazi Mh.William Lukuvi siku ya Jumatano februari 24 wakati akizungumza na wananchi hao katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kupokea hati ya usuluhishi wa mgogoro wa arhi katika kijiji cha mabwelele ili kutolea hukumu.

 

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

UGIRIKI YAHITAJI MGAWANYO SAWA WA WAKIMBIZI.

                                                                                                                                               

                                       PICHA NA MTANDAO

Na: Alfred Lukonge/BBC NEWS

Kufuatia wito uliotolewa na nchi za Balkani na Austria hivi karibuni kuhusu kupunguzwa kwa wahamiaji wanaovuka mipaka yao, nchi ya Ugiriki inataka kupinga maazimio yoyote yatakayofikiwa kwenye mkutano ujao wa viongozi wa jumuiya ya  ulaya iwapo nchi wanachama hazitakubaliana kuweka uwiano sawa wa kugawana wakimbizi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 
 

ZIKA YAFANYA WANASAYANSI KUTOKA MAREKANI KWENDA BRAZIL

 

                                         PICHA NA MTANDAO 

       

Na: Alfred Lukonge/BBC Swahili

Timu ya wanasayansi kutoka Marekani imekwenda jimbo la Paraeeba lililoko kaskazini magharibi mwa Brazil kutafiti uhusiano wa watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na virusi vya Zika.

Wanasayansi hao kutoka kituo cha CDC kinachojishughulisha na udhibiti na uzuiaji magonjwa nchini Marekani ilienda kwenye maeneo yalioathirika na kuchukua sampuli ya damu pamoja na kufanya mahojiano na akinamama waliozaa watoto wakiwa na vichwa vidogo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

MIPAKA KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KATIKA BONDE LA MGONGOLA KUWEKWA

  

                                      PICHA NA MTANDAO

         
              


Na: Susane Cheddy

Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mh.Mwigulu Lamek Nchemba amewataka wananchi wa  tarafa ya Mvomero kuweka mipaka baina  ya wakulima na wafugaji katika bonde la Mgongola ili kuepusha mgogoro uliopo kati yao.

Waziri Nchemba amesema hayo Jumapili februari 22 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Dihombo  kujadili mgogoro wa mpaka wa eneo la bonde la Mgongola na kusema ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha anaheshimu  utaratibu utakaowekwa na kufuata sheria zilizowekwa ili kulinda amani na utulivu na wanachi wa eneo hilo  kuweza kuishi kwa amani.


Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

Subcategories

Page 37 of 44