Pamoja na kutoa kozi za sayansi ya kilimo lakini pia SUA inatoa kozi mbalimbali zisizo za kilimo

Na Gerald Lwomile

Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa pamoja na ukweli kuwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kinatoa kozi mbalimbali za kilimo lakini pia chuo hicho kinatoa kozi katika fani mbalimbali tofauti na Kilimo kama Ualimu wa Masomo ya Sanyansi Mazingira pamoja na Maendeleo Vijijini.

udahili min min

Maafisa udahili wa SUA waliovaa fulana za kufanana wanaendelea na udahili wa wanafunzi katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam (Picha na Gerald Lwomile)

Ufafanuzi huo umekuja kufuatia kuwepo kwa taarifa kwa wananchi wengi kuwa SUA imekuwa ikitoa kozi za kilimo pekee na wanafunzi wengi kushindwa kujua ukweli wa kozi zinazotolewa SUA

Akizungumza katika maonesho ya vyuo vikuu ambayo yanaendela katika viwanja vya mnazi mmoja Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusianao na Masoko SUA Bi. Mariam Mwayela alifafanua hayo wakati akizungumza na wanafunzi na wananchi mbalimbali waliofika katika maonesho hayo.

“….. maana imekuwa inaaminika kuwa SUA inatoa kozi za kilimo pekee, hapana mbali na kuwepo kwa kozi za kilimo lakini pia SUA inatoa kozi zingine ambazo mwanafunzi anaweza kusoma hata kama amesoma masomo ya sanaa yaani Arts”

Wakati huo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amewataka wanafunzi mbalimbali wanaotaka kusoma katika chuo cha SUA waendelee kutembelea katika banda la SUA wakati huu wa maonesho kwani zoezi la udahili pia linaendelea katika eneo hilo.

chibunda min min

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Chibunda akizungumza na vyombo vya habari katika maonesho ya TCU (Picha na Tatyana Selestine)

Amesema mbali na wanafunzi hao kujionea teknolojia na ubunifu mbalimbali unaofanywa na chuo lakini pia watapata fursa ya kuchagua programu mbalimbali wanazotaka kusomea

“Tunatoa huduma za ushauri kwa wanafunzi na kuwaelekeza kuhusu kozi mbalimbali ambazo zinatolewa chuoni kwetu hivyo mwanafunzi anaweza kuchagua kozi ambayo anataka kusoma kutokana na ufaulu wake wa kidato cha sita”

Ikiwa ni siku ya nne tangu Maonesho haya ya Vyuo Vikuu kuanza muitikio wa wanafunzi na wazazi umekuwa ni mkubwa sana. Maonesho haya vyuo vikuu yanaendelea jiji Dar es Salaam hadi julai 20 huku yakiwa na kauli mbiu “JUKUMU LA VYUO VYA ELIMU YA JUU KATIKA KUZALISHA UJUZI UNAOHITAJIKA KWA AJILI YA VIWANDA”

Serikali inafurahishwa na hatua Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kusimamia Ithibati na Ubora wa Elimu

Na Gerald Lwomile

Dar es Salaam

Serikali imesema inafurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara ya Sayansi na Teknolojia katika kusimamia Ithibati na Ubora wa elimu unaotolewa na vyuo vikuu nchini vikiwemo vya umma na binafsi jambo linalosaidia kuwafanya wahitimu kuwa na soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo julai 17 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa maonesho ya vyuo vikuu wakati akizungumza na washiriki wa maonesho na wananchi katika viwanja vya mnazi mmoja jiji Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema uandaaji wa mitaala mbalimbali katika vyuo umeboreshwa kufuatia mafunzo yaliyotolewa na wizara hiyo na kuwa hatua zinachuliwa na vyuo mbalimbali vya kuhuisha mitaala na kuja na mitaala mipya ni jambo ambalo linainua ubora wa elimu nchini

waziri mkuu 2 min

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonesho ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam (Picha na Mariam Mwayela)

Waziri mkuu amesisitiza kuwepo kwa mitaala ambayo haiwaandai wahitimu kuajiriwa pekee lakini pia kuwepo na mitaala ambayo inawaandaa wahitimu kujiajiri, amesema kutokana na hali hiyo taifa litachochea hali ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu

“Bado nieendele kutoa wito kwa vyuo vikuu hapa nchini kuendelea kuhuisha mitaala ya elimu hiyo ili kutoa matokeo tunayoyatarajia”

Akitoa shukrani kwa Waziri Mkuu  baada ya kuzindua rasmi maonesho hayo Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nchini ambaye pia ni Makamu wa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa ushirikiano katika kuimarisha utendaji katika vyuo vikuu nchini.

Prof Chibunda min

 

Mwenyekiti wa Watendaji Wakuu wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki nchini ambaye pia ni Makamu wa  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akitoa neno la shukrani kwa serikali (Picha na Tatyana Selestine)

uboreshaji na upelekaji wa mikopo kwa wanafunzi katika vyuo vikuu nchini kwa kiasi kikubwa imeondoa tatizo la migomo katika vyuo vikuu nchini na kuwa Bodi ya Mikopo na Serikali kwa kiasi kikubwa vinatakiwa kupongezwa.

“Kwa niaba ya wasimamizi wa vyuo vikuu napenda kuishukuru sana serikali kwa hili ambalo tume wamelifanya la kumaliza uhakiki katika baadhi ya vyuo vikuu ambavyo vilikuwa vimefungiwa udahili na sasa vimeruhusiwa kuendelea na udahili tunaishukuru sana tume pamoja na serikali na nipende kutoa rai kwa tume kufanya uhakiki katika vyuo vikuu vilivyobaki” amesema Prof. Chibunda

Tazama Hapa Matokea Ya Kidato cha Sita 2019

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita 2019.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.

Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.
 
1.Kutazama matokeo ya Kidato cha Sita  <<BOFYA HAPA>>.

2.Kutazama Matokeo Ya Mtihani Wa Ualimu 2019  <<BOFYA HAPA>>

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFICHUA WALA RUSHWA

Na: Farida Mkongwe
Waandishi wa Habari mkoni Morogoro wametakiwa kuendelea kutoa elimu kuhusu rushwa na madhara yake sanjari na kuwatangaza wale wote wanaojihusisha
na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa ambao wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoo Dkt. Kebwe Steven Kebwe akifungua Semina fupi kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Morogoro Bi. Janeth Machulya wakati akitoa
mada kwenye semina fupi ya waandishi wa habari iliyolenga kutoa elimu kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Morogoro Bi. Janeth Machulya akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya wanahabari katka mapambano dhidi ya rushwa
 
Bi. Janeth amesema waandishi wa habari ni kiungo na daraja baina ya wananchi na serikali hivyo wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kufichua na kukemea
vitendo rushwa ambavyo vinafanywa na baadhi ya watu wakiwemo watumishi wa umma wasio waadilifu.
Awali akifungua semina hiyo mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.  Kebwe Steven Kebwe amesema katika mkoa huo bado kuna taasisi nne ambazo zimeonekana kuwa tatizo
katika suala la rushwa na kuzitaja taasisi hizo kuwa ni taasisi za kipolisi, mahakama, ardhi na serikali za mitaa na kuahidi kuendelea kuzishughulikia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro
Amesema kwa sasa sehemu nyingi za taasisi za umma kuna mabadiliko katika utendaji kwani huduma nyingi zimeboreshwa hali inayosaidia ongezeko la kodi na
nidhamu ya matumizi ya fedha kwa watumishi wa serikali.

WAANDISHI SUAMEDIA WASHIKA NAFASI YA PILI TUZO EJAT UPANDE WA TV 2019

Na Ayoub Mwigune

Waandishi wa habari wa SUAMEDIA Gerald Lwomile na Calvin Gwabara wameibuka miongoni mwa washindi katika nafasi ya pili katika mashindano ya Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania EJAT yanayoendeshwa na Baraza la Habari Tanzania MCT kwa mwaka 2018.

Waandishi hao ambao wameshirika katika katika mashindano hayo Calvin Gwabara kwa mara ya pili na Gerald Lwomile kwa mara ya kwanza wameshika nafasi ya pili katika makundi ya uandishi wa habari za Kilimo na Kilimo Biashara, Utalii na uhifadhi na Usalama wa Chakula na Vipodozi upande wa Televisheni.

IMG 7361Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Jaji Mtaafu Joseph Sinde Warioba aliyekuwa mmoja wa wageni mashuhuri katika tuzo za EJAT akiwa katika picha ya pamoja na Gerald Lwomile kushoto na kulia ni Calvin Gwabara.

Gerald Lwomile ambaye ameshiriki kwa mara ya kwanza ameshinda nafasi ya pili katika tuzo mbili na nafasi ya tatu katika tuzo moja, ameshika nafasi ya pili  katika kundi la uandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi ambapo alipeleka makala za runinga zinazohusu Msitu wa Hifadhi Kimboza na Mti Vamizi wa Mrushia ambazo zote ni utafiti uliofanywa na Dkt. Charles Kilave mtafiti kutoka SUA huku pia akishika nafasi ya pili katika uandishi wa habari za Usalama wa Chakula na Vipodozi ambapo aliwasilisha makala mbili.

Naye Calvin Gwabara ambaye alikuwa mshindi wa kwanza wa Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo na Kilimo Biashara mwaka 2017 upande wa Radio mwaka huu amekuwa mshindi wa pili wa tuzo hizo upande wa Televisheni.

 

 

EJAT

Salome Kitomary( wa pili kulia), mshindi wa jumla wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania, EJAT 2018 iliyofanyika Juni 29, 2019 katika

Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Oysterbay Dar es Salaam. Picha  na MCT.

 

Akizungumzia ushindi huo Lwomile amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano mzuri baina ya watafiti wa SUA ambao wamekuwa tayari kutoa matokeo ya utafiti wao kwa umma ili kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo wakulima na wananchi kwa ujumla.

Aidha amesema ushirikiano na wafanyakazi wa SUAMEDIA umekuwa chachu ya ushindi huo ambapo wamekuwa wakipeana mawazo mbalimbali namna ya kuzalisha vipindi bora ambavyo vinalenga kuihabarisha jamii juu ya Kilimo na sayansi zingine zinazoendana na kilimo.   

 

Kwa upande  Calvin Gwabara ametoa wito kwa wafanyakazi wengine wa SUAMEDIA pamoja na waandishi wa habari nchini  kujikita katika kuandika na kuandaa habari ambazo zitaweza kutatua changamoto katika jamii inayowazunguka badala ya kuandika habari ambazo hazina msaada katika jamii huku akipongeza SUA kwa ushirikiano wao ambao wamekuwa wakitoa na kuwazesha katika kuandaa vipindi  vyao.

Aidha Gwabara amempongeza  Gerald Lwomile baada ya kujitokeza kwa mara ya kwanza na kuwania tuzo na kufanikiwa kushika nafasi  ya pili ya katika kundi la uandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi na akishika nafasi ya pili katika uandishi wa habari za Usalama wa Chakula na Vipodozi akimtaka aendelee kujituma na kuwania tuzo nyingine/

Lwomile pia ameshika nafasi ya tatu katika wapiga picha mahiri wa televisheni huku nafasi ya kwanza ikienda Azam TV

 

Kwa mujibu wa MCT Jumla ya kazi 644 ziliwasilishwa kwa ajili ya kushindanishwa kwenye Tuzo hizi ambazo 176 (27%) kati ya hizo zimeletwa na waandishi wa habari wanawake huku zilizowasilishwa na waandishi wa habari wanaume zikiwa 468 (73%).

TUZO 1 1

Mzalishaji wa vipindi SUAMEDIA Gerald Lwomile mwenye suti akipokea cheti cha mshindi wa pili 

Kazi zilizowasilishwa zimetoka katika vyombo vya habari 67, ambapo Mwananchi Communications Ltd (MCL) ikiongoza kwa idadi ya kazi nyingi zaidi, zikiwa jumla 114 (14.1%) ikifuatiwa na The Guardian Ltd wakiwa na kazi 96 (11.9%).

IMG 7230Mzalishaji wa vipindi SUAMEDIA Calvin Gwabara mwenye suti akipokea cheti cha mshindi wa pili 

EJAT ni tukio la kila mwaka linaloandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na washirika wake Wakfu wa vyom,bo vya habari (TMF), Taasisi ya habari ya Kusini mwa Afrika - (MISA-Tan) Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri Tanzania Chama cha wamiliki wa Vyombo vya habari (MOAT) , (MOAT) Umoja wa Klabu za Habari Tanzania (UTPC), HakiElimu SIKIA and ANSAF.

Subcategories

Page 5 of 50