UGONJWA WA USONJI UATHIRI WATOTO HUKU WAZAZI WAKIDHANI NI WATUKUTU


  

                                         

       

Na: Kelvin Gwabara

Wazazi na walezi wote nchini wametakiwa kuwa karibu na kufuatilia tabia na mwenendo ya watoto wao ili kuweza kugundua magonjwa mbalimbali yanayoweza kuwapata wototo wao ikiwemo ugonjwa wa Usonji kwa kitaalamu AUTISM ambao wazazi wengi uwa hawafahamu dalili zake na hivyo kuathiri watoto huku wazazi wakidhani ni watukutu.

Wito huo umetolewa na Mzazi mwenye mtoto mwenye ugonjwa huo na mtaalamu kutoka Taasisi ya LADDER FOR CHANGE Bi. Sammy Mrisho wakati akizungumza na kutoa elimu kwa baadhi ya wazazi waliofikiwa na asasi yao katika maadhimisho ya siku ya Usonji Duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe mbili mwezi wa nne katika maadhimisho yaliyoandaliwa na asasi yao Mkoani Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WANANCHI MKOANI MOROGORO WATAKIWA KUSHIRIKI KWA KINA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE

          

Na: Kelvin Gwabara

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dt. Kebwe Steven Kebwe amewataka wakazi wote wa mkoa wa Morogoro kushiriki kwa kina katika maandalizi ya uzinduzi wa mbio za mwenge unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi huu katika uwanja Jamhuri Mkoani Morogoro.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Dt.Kebwe amesema kuwa mkoa wa Morogoro umepewa heshima kubwa ya za kuwasha mwenge wa Uhuru katika manispaa ya Morogoro hivyo ni vyema heshima hiyo kila mwananchi akashiriki kikamilifu katika kufanikisha zoezi hilo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WATUMISHI KATIKA TAASISI MBALIMBALI HAPA NCHINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KAMA TIMU

               

  Na: Alfred Lukonge

Watumishi katika Taasisi mbalimbali wanatakiwa kufanya kazi kama timu ili waweze kupata  lugha moja kwenye maamuzi  kama wanataka maendeleo ya   kweli katika Taasisi hizo.

 

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo Prof. Simon Msanjila alipofanya ziara katika  Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine  SUA mjini Morogoro Jumamosi ya tarehe 2 Aprili kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho ikiwemo kuongea na uongozi wa juu wa chuo hicho, wakuu wa vyuo, vitivo, wakurugenzi,wakuu wa idara za uendeshaji, vyama vya wafanyakazi pamoja na serikali ya wanafunzi.

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WAFUGAJI WA KUKU WATAKIWA KUFUGA KITAALAM

   

                                           PICHA NA MTANDAO

       

Na: Neema Shayo

Wafugaji wa kuku nchini wameshauriwa kufuata ushauri wa wataalam kwa kuwapati kuku chanjo,kuwatunza katika mazingira mazuri ili kuwalinda na ugonjwa wa mdondo, ambao huwapata kuku wasiokuwa na uangalizi mzuri.

Hayo yamebainishwa na  Daktari wa mifugo kutoka kitivo cha mifugo katika Chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) Dkt. Ayoub Emanuel wakati  akiongae na SUA MEDIA ofisini kwake na kusema kuwa ugonjwa wa  mdodo kwa kitaalam unaitwa Newcastle ni ugonjwa unaosambazwa kwa njia ya hewa hivyo ni muhimu wafugaji wakazingatia utaalamu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

SUA YAZINDUA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MATREKTA

            

Na:  Catherine Mangula Ogessa

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na kampuni ya John Deere wamezindua mafunzo ya matumizi ya matrekta katika kilimo kwa wakulima na wanafunzi wa chuo hicho wanaochukua masomo ya uhandisi kilimo, maafisa ugani wataalamu wa kilimo kutoka mkoani na wilayani.

Akizindua mafunzo hayo katibu mkuu wa wizara ya kilimo, ufugaji na uvuvi Mhe. Dr. Florens Turuka amesema kuwa ni wakati sasa washiriki wa mafunzo hayo wakazingatia mafunzo hayo kwa makini ikizingatiwa kuwa changamoto inayopatikana katika kilimo ni suala zima la matumizi bora ya zana za kilimo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WAFUGAJI WA MBWA WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI ZA AFYA ILI KUWAEPUSHA NA MARADHI

           

Na:Farida Sadiki                                                       

Wafugaji wa mbwa wametakiwa kuzingatia suala la afya kwa wanyama hao ili kuwaepusha na maradhi mbalimbali yanayo weza kuwa kumba ikiwemo ugonjwa mbaya wa kichaa unao sababishwa na virusi vinavyo julikana kwa jina la Rhabdovirus.

Akizungumza na SUAMEDIA daktari wa mifugo katika kitivo cha tiba ya mifungo na afya ya binadamu cha   chuo kikuu cha Sokoine  cha kilimo sua Dr.  Emanueli Mwakijungu amesema kuwa wafugaji wa mbwa  wanatakiwa kuacha  ufugaji wa mazoea usiofuata taratibu za kitaalamu na badala yake amewataka kufuga kitaalamu kwa  kujali afya za wanayama hao ili kuwanusuru na maradhi hususani ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WAENDESHA BODABODA WANOVUNJA SHERIA KUCHUKULIWA HATUA

 

             

Na:  Selina Samson

Tatizo la madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda  kutokutii sheria za barabarani ndani ya mkoa wa Morogoro limezidi kuwa kero kwa wakazi wa mkoa huo jambo lililopelekea jeshi la polisi kikosi cha  usalama barabarani kuanzisha zoezi endelevu la kukagua na kukamata madereva wote wanaokiuka sheria zilizowekwa

Akiongea na SUA MEDIA Askari wa kikosi cha  usalama barabarani  Salum  Salum ameeleza kuwa licha ya kutoa elimu ya usalama wa barabarani  kwa madereva hao kabla ya kupewa leseni lakini bado asilimia kubwa ya madereva hao ni wale ambao hawajapata elimu jambo linalosababisha madhara makubwa ikiwemo kusababisha ajali za barabarani kuongezeka.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

SERIKALI YATAKIWA KUTAMBUA MAHITAJI YA VIZIWI

            

Na: Jesca Pelembela                    

Watu wenye ulemavu wa kusikia wameitaka Serikali ya Awamu ya tano kutambua na kutathimini mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa kuwajengea shule maalum za viziwi hasa za sekondari ili waweze kupata elimu sawa na wasio na ulemavu.

Hayo yamesemwa na katibu mtendaji wa  Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoani Morogoro, Bwana. Henry Mtasiwa wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake na kuiomba serikali kupitia halmashauri za wilaya kusaidia walemavu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

SUA FM YARUDI TENA HEWANI

             

Na: Selina Samson

Radio ya SUA FM inayomilikiwa na Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)  imerejea tena hewani kwa kurusha matangazo yake  hewani kwa majaribio.

Baada ya kukaa kimya kwa takribani miezi 3, mmoja wa waandishi waandamizi wa radio hiyo Bw. Bujaga Izengo Kadago amesema kuwa radio hiyo imerudi tena hewani  baada ya kusitisha matangazo yake tangu Desemba 23 mwaka jana kutokana na mitambo ya kurushia matangazo kuunguzwa na radi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WAKULIMA KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA NAMNA YA UTUMIAJI WA MATREKTA YA JOHN DEERE

            

Na: Consolata Philemon

 
Wakulima wadogo, wakati pamoja na baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA   wanatarajiwa kunufaika na Mafunzo ya matumizi bora ya Trekta aina ya John Deere na zana zake yatakayodumu kwa  wiki moja  katika idara ya Uhandisi Kilimo na Mipango.

Akizungumza na SUAMEDIA ofsini kwake mkuu wa idaya ya Uhandisi Kilimo na Mipango ya Ardhi kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Profesa Sylivester Mpanduji amesema  mafunzo hayo yatazinduliwa rasmi katika viwanja vya Uhandisi Kilimo vya SUA Morogoro tarehe 01 April.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

ILI KUONDOKANA NA UMASKINI WANAWAKE WATAKIWA KUJIUSISHA NA VIKUNDI VYA UZALISHAJI FEDHA

                                         PICHA NA MTANDAO   

      

Na: Farida Sadiki

Wanawake wanatakiwa kujihusisha katika vikundi mbalimbali vya uzalishaji fedha kwa njia ya halali ikiwemo VICOBA (Village Community Bank) ili kujiongezea kipato na kupunguza umaskini au kumaliza kabisa tatizo hilo katika familia zao.

Hayo yamezungumzwa na Bibi Nuru Shabani ambaye ni mwenyekiti wa vicoba vya kina mama wa misufini katika manispaa ya Morogoro kinachotambulika kama kikundi cha faraja alipohojiwa na SUAMEDIA katika ofisi za kikundi hicho.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

FEDHA ZILIZOTENGWA KWA AJILI YA WALEMAVU ZITUMIKE JINSI ILIVYOKUSUDIWA-MTAJIWA

            

Na:Suzane Cheddy

Serikali imetakiwa kuhakikisha fedha zinazotolewa katika halmashauri za wilaya kwa ajili ya watu wenye  ulemavu zitumike kwa malengo yanayokusudiwa ili kuweka usawa wa haki za binadamu.

Hayo yamesemwa na katibu mtendaji  chama cha viziwi Tanzania CHAVITA mkoa wa Morogoro Bw.Henry Mtajiwa kuwa kutokana na changangamoto wanazokutana nazo katika maisha ikiwemo uhaba wa fedha za kujiendeleza, ukosefu wa rasilimali za kimaendeleo pamoja na vitendea kazi ni sababu kubwa ya chama kutofikisha malengo yake.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

JESHI LA POLISI LASHIKILIA WATUHUMIWA WATANO KWA MAKOSA TOFAUTI

            

Na: Neema Shayo                      

Jeshi la polisi mkoa Morogoro, limefanya msako katika maeneo mbali mbali ya mkoa Morogoro na kufanikiwa kukamata watuhumiwa watano katika matukio matatu tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa morogoro kamishna msaidizi wa polisi Ulrich Matei amesema kuwa katika jeshi hilo limewakamata watu wawili Bi. Magreth Mosha (34) mkazi wa Kibaha, na mwningine Bw. Hamisi Kileo.kwa kosa la kukutwa na  Nyara za serikali ikiwemo Pembe za ndovu na nyama ya mnyama aina ya Sheshe.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

JESHI LA POLISI MKOANI MOROGORO LAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU

            

Na: Jesca Pelembela

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limekamata wahamiaji haramu sita waliokuwa wakisafirishwa kutoka nchini Ethiopia kwa nia ya kwenda nchini Afrika ya kusini.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro, Ulrich Matei amesema kuwa tarehe 27/3/2016 majira ya saa kumi na mbili jioni huko maeneo ya ya Sangasanga kata ya mzumbe tarafa ya Mlali Wilaya ya Mvomero jeshi la polisi limewakamata raia hao wa Ethiopia wakiwa kandokando ya barabara kuu ya Morogoro/Iringa wakiwa wameterekezwa na gari lilokuwa likiwasafirisha.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WANANCHI KATA YA KIWANJA CHA NDEGE MJINI MOROGORO WALALAMIKIA WIZI WA UKATAJI MADIRISHA

             

Na: Farida Sadiki

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa lusogo maarufu kama (chakabovu) kata ya kiwanja cha ndege wamelalamikia vikali na kusikitishwa na vitendo vya wizi wa ukataji madirisha unao endelea kufanywa na watu wasio julikana  mtaani hapo.

Akizungumza na SUAMEDIA mingoni mwa wakazi hao bibi Maangaza Makupa amesema kuwa hawana raha wala amani mtaani hapo kwa kua wizi huo wa madirishani unazidi kushika kasi kila kukicha, kwani watu hao wasio julikana hukata madirisha na kutumia matobo hayo kuiba vitu mbalimbali ikiwemo simu nguo fedha na kadhalika.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

TANESCO MKOANI MOROGORO YATAKIWA KUANGALIA HALI YA USALAMA KWA WAFANYAKAZI WAO

              

Na: Suzane Cheddy

Shirika la umeme tanesco mkoani Morogoro limetakiwa kuwa makini katika shughuli za ufundi ili kuweka wafanyakazi wake katika hali ya usalama pindi wawapo kazini

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kata ya mafiga walioshuhudia tukio la kifo cha mfanyakazi wa TANESCO aliyepigwa na shoti ya umeme wakati akiwa kwenye matengenezo ya umeme kwenye nguzo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WATANZANIA WAHIMIZWA KUPANDA MITI YA MIKARATUSI

            

Na: Gerald Lwomile

Imeelezwa kuwa watanzania wanaweza kuepuka kuipeleka nchi katika jangwa na kujitengenezea maisha bora kama watapanda miti kwa wingi na kuitunza ikiwa ni pamoja na miti ya mikaratusi ambayo ina faida kubwa.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti cha Lushoto kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa misitu Tanzania TAFORI Bw. John Richard wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake Lushoto Mkoani Tanga.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

MTOTO AKUTWA AMAEKUFA NDANI YA KISIMA

            

Na: Selina Samson

Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Helena Mussa mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitano mkazi wa kijiji cha Mazoka wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro amekutwa akiwa amekufa ndani ya kisima cha maji kwa kile kilichodaiwa kudumbukizwa na baba yake mzazi mwenye matatizo ya akili kwa muda mrefu.

Baadhi ya  mashuhuda wa tukio hilo na ndugu wa marehemu wamesema wakati walipo enda kuchota maji katika kisima  hicho waliuona mwili wa mtoto huyo ukielea majini kisha kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kitongoji  cha Rozi  Bw.  Paulo John ambapo ameeleza  kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hilo  alitoa taarifa polisi ndipo taratibu za kutoa mwili huo zilipoanza.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

BABA NA MAMA LISHE KATIKA MANISPAA YA MOROGORO WAPEWA ELIMU YA AFYA

                                                                                                             

Na:SelinaSamson/JescaPelembela                                                        

Idara ya afya mkoa wa Morogoro imetoa elimu kwa wafanyabiashara wa chakula maarufu kama  baba na mama lishe na kuwataka kuhakikisha wana sehemu maalum ya kuandalia vyakula iliyokaguliwa na kuruhisiwa na mamlaka husika, na kukumbushwa kuwa usafi  uanzie katika mazingira ya miili yao wenyewe kwani wengi wao wamekuwa wakifanya usafi wa mazingira ya nje na kusahau kusafisha miili yao

Hayo yameelezwa na, kaimu mkurugenzi huduma za afya na usafi wa mazingira katika wizara ya afya, ustawi wa jamii,wanawake, jinsia na watoto, Bw. Theophil Likangaga katika semina iliyofanyika kata ya Boma mjini Morogoro ambapo amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kutoa elimu ya afya kwa  wafanyabiashara hao ili kupunguza kasi ya maambukizi ya magonjwa ya milipuko.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

TATIZO LA UHABA WA MAJI NI KILIO KIKUBWA KWA WANANCHI WA ENEO LA MAFISA LILILOPO NDANI YA MANISPAA YA MOROGORO

            

Na: Suzane Cheddy

Kutokana na maji kuwa sehemu kubwa ya maisha ya mwanadamu wananchi wa mtaa wa Mafisa uliopo ndani ya manispaa ya Morogoro wamelalamikia uongozi wamtaa kutokana na tatizo la uhaba wa maji wanaoupata kadiri siku zinavyoendelea.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wanakijiji kutokana na mgao wa maji unaendelea ambapo awali walikuwa wakipata maji kila baada ya siku tatu lakini kwa sasa wanapata maji baada ya wiki moja hadi nne hali inayopelekea kuhatarisha maisha yao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

Subcategories

Page 43 of 52