WANANCHI WATAKIWA KUZINGATIA KANUNI BORA ZA KILIMO CHA MAEMBE

     

                                          PICHA NA MTANDAO

 

        

Na: Jesca Pelembela

Idara ya Baologia na Misitu SUA, imewashauri wananchi kuzingatia kanuni bora za kilimo cha miembe hasa kanuni za kuchagua aina bora ya upandaji wa miti hiyo kulingana na mahitaji ya soko.

Akizungumza na SUAMEDIA msimamizi wa wanafunzi wanaojifunza kwa vitendo bw. Mnyonge James amesema miti ya miembe inatakiwa ipandwe umbali wa mita 10 kwa 10 kama utatumia miembe ya kuunga, kwa sababu miti hii haiwi mikubwa sana na haiishi miaka mingi, kwa ile ambayo ya kuunga ipandwe umbali wa mita 15 kwa 15 kwa kila mti mmoja.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

SEKTA YA MADINI YATAKIWA KUCHANGIA ASILIMIA KUMI YA PATO LA TAIFA IFIKAPO MWAKA 2025

            

Na: Alfred Lukonge

Maafisa madini katika Wizara ya Nishati na Madini kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania wametakiwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na ubunifu ili ifikapo mwaka 2025 sekta hiyo iweze kuchangia asilimia 10 ya pato la taifa.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe alipokuwa anafungua mafunzo ya SMMRP " sustanable management of mineral resources project" yanayohusu uombaji wa leseni za uchimbaji madini kupitia mtandao Jumatatu ya Machi 21 katika kituo cha kompyuta chuoni  SUA mjini Morogoro

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WANANCHI WAHAMASISHWA KUTUMIA ASALI KAMA CHAKULA NA DAWA

                  

                                             PICHA NA MTANDAO

       

Na: Farida Sadiki

Mtaalamu wa nyuki na uvunaji asali kitengo cha baolojia ya misitu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mkoani Morogoro Bw. Michael Edward Singila amewahamasisha wananchi kujikita katika utumiaji wa asali kama chakula na dawa kwa kuwa asali ina manufaa mengi katika mwili wa binadamu.

Singila amezungumza hayo alipohojiwa na SUAMEDIA na kusisitiza kuwa jamii inatakiwa kujihusisha haswa katika kutumia asali katika matumizi yao ya kawaida kwani zao hili linajitosheleza na lina faida nyingi kwa mtumiaji ikiwemo kula na kutibu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WADAU WA EPINAV WATAKIWA KUTUMIA MATOKEO YA MIRADI WALIYOSHIRIKI KUNUFAISHA WANANCHI

    

                                           PICHA NA MTANDAO

        

Na: Bujaga Izengo Kadago

Wadau wote wa programu ya epinav wametakiwa kutumia matokeo ya miradi waliyoshiriki kuwanufaisha watanzania ili waboreshe maisha yao na pia kushawishi kuwepo kwa sera bora na sahihi nchini.

Wito huo umetolewa na mratibu wa programu ya epinav kutoka chuo kikuu cha sokoine cha kilimo sua Prof. Vedasto muhikambele alipokuwa akifunga kongamano la tatu na la mwisho la programu ya epinav, kongamano lililofanyika sua, Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KULETA MAENDELEO

                         

Na: Farida Mkongwe                                  

Imeelezwa kuwa iwapo vyombo vya habari vitatimiza majukumu yake ipasavyo katika kuibua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi na hasa wanawake, basi kwa kiasi kikubwa serikali ya awamu ya tano itafanikiwa katika kuleta maendeleo ya sekta mbalimbali hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Bw. Melkizedeck Karol wakati wa majadiliano na waandishi wa habari mkoani Morogoro kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuandika habari zilizoibuliwa kwenye vituo vya taarifa na maarifa vilivyopo katika kata ya Kibuko na Mbuyuni zilizopo katika halmashauri ya Morogoro vijijini mkoani Morogoro.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

SERIKALI IMETOA ELIMU KWA WAHASIBU NA WASADIFU MADINI JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA KIELEKRONIKI KATIKA MALIPO

                                                                        

Na:Suzane Cheddy

Serikali kupitia wizara ya nishati na madini imetoa elimu kwa wahasibu wa sekta hiyo ili kuwawezesha wachimbaji madini kufanya malipo kupitia benk pamoja na simu za mikononi.

Hayo yamesema na mkuu wa idara ya HICT(Head of Information and Communication Technology) wizara ya nishati na madini Bw.Fransis Fungameza marchi 16 katika semina ya wiki mbili inayofanyika katika kituo cha kompyuta chuoni SUA na kusema kuwa serikali imeamua kutoa elimu hiyo kutokana na mabadiliko ya mfumo wa utoaji malipo ambapo kwa sasa malipo yote yatafanyika kwa njia ya kielekroniki.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA ASALI ILIYOTENGENEZWA NA NYUKI WADOGO

                                        PICHA NA MTANDAO  

        

Na. Jesca Pelembela

Idara ya Biologia ya Misitu SUA, imewashauri wananchi kutumia asali bora iliyotengenezwa na nyuki wadogo kwa sababu ni asali iliyo na virutubisho vingi na muhimu kwa matumizi, pia hutumika kama dawa ya magonjwa mbali mbali.

Akizungumza na SUAMEDIA mtaalamu wa mambo ya nyuki na uvunaji wa asali, Bwana Michael Singila, amesema kuwa asali ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi kwa sababu nyuki wadogo hutengeneza asali yenye virutubisho vingi ukilinganisha na asali ya nyuki wakubwa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WANANCHI WASHAURIWA KUJUA AINA ZA MITI ZINAZOFAA KUPANDWA KATIKA NYUMBA ZAO

      

        

Na: Farida Sadiki

Wananchi wameshauriwa  kujua aina za miti inayo weza kupandwa katika maeneo ya nyumba zao kabla ya kufanya zoezi hilo la upandaji  ili kuepuka madhara yanayo weza kusababishwa na miti hiyo ikiwemo kubomoa nyumba

Akizungumza na SUAMEDIA msimamizi wa wanafunzi wanao jifunza kwa vitendo  kwenye Idara ya Misitu katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA Bwana Mnyonge James  amesema wananchi wana takiwa kuwaona wataalam wa miti  kabla ya kupanda miti kwenye nyumba zao  ili kujua aina ya miti itakayo weza kukua vizuri katika maeneo yao pasiponkuleta madhara inapo pandwa  karibu na nyumba ikiwa ni pamoja na kubomoa nyumba.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

ZAIDI YA WATU 500 MOROGORO VIJIJINI WALIATHIRIKA BAADA YA KUTUMIA MAJI YASIYOKUWA SAFI NA SALAMA

                                                                                          

Na: Farida Mkongwe

Utafiti mdogo uliofanywa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP umebaini kuwa zaidi ya watu 500  wanaoishi kata ya mkuyuni na kibuko zilizopo katika Halmashauri ya Morogoro vijijini mkoani Morogoro walifikishwa katika kituo cha afya cha mkuyuni kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2015 hadi Februari mwaka 2016 kutokana na kutumia maji yasiyo safi na salama.

Akitoa matokeo ya utafiti huo wakati wa majadiliano na waandishi wa habari mjini Morogoro Afisa mawasiliano wa TGNP Bw. Melkizedeck Karol amesema kuwa utafiti huo wa siku tisa ni sehemu ya kazi zao za kila mwaka ambapo hufanya uraghibishi yaani utafiti shiriki na ufuatiliaji wa jambo hadi linapokamilika katika maeneo mbalimbali na kwa mwaka huu kwa mkoa wa Morogoro wameamua kujikita katika kata ya Kibuko iliyopo Halmashauri ya Morogoro vijijini.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........


KITENGO CHA UZALISHAJI MICHE YA MATUNDA IDARA YA SHAMBA CHUONI SUA CHAOMBA ENEO LA KUDUMU

           

Na: Jesca Pelembela    

Kitengo cha Uzalishaji wa miche ya matunda  SUA  kilicho chini ya kitengo cha Idara ya Shamba katika kampasi ya  Solomon Mahlangu, kimeomba kupewa eneo la kudumu kwa ajili ya uzalishaji wa miche hiyo ili kukuza biashara na kuingiza mapato ya ndani.

Akizungumza na SUA MEDIA Afisa Kilimo, Kitengo cha uzalishaji wa miche ya matunda SUA, Bibi. Urusula Mosile amesema kuwa licha ya kuwa wanahusika na uzalishaji na uuzaji wa miche ya matunda kwa ajili ya kuongeza kipato cha chuo lakini pia wanakabiliwa na tatizo la eneo la kudumu kwa ajili ya uzalishaji ambao hupelekea kushindwa kuzalishaji miche mingi iwezekanavyo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WADAU WA KILIMO WATAKIWA KUANZISHA JUKWAA LA KUJADILI NA KUTETEA MASLAHI YAO KATIKA KILIMO

                       

Na: Bujaga Izengo Kadago

Kumezuka mjadala mkubwa kuhusu umuhimu wa majukwaa ya wadau wa kilimo kusajiliwa rasmi au la.

 

Mjadala huo umetokewa wakati wa kujadili mada iliyotolewa na Prof.Dismas Mwaseba kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika kongamano lililoshirikisha watafiti na wadau wa programu ya EPINAV,kongamano linalofanyika SUA.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WAKULIMA WAPATIWA USHAURI WA KILIMO KWA NJIA YA MTANDAO

                                                              

                                  PICHA NA MTANDAO 

Na: Halima Katala

Watafiti pamoja na maafisa wa kilimo kutoka sua wameanzisha huduma ya bure ya kutoa ushauri kwa wakulima kwa njia  simu ya mokononi kupitia  mtandano wa ushauri kwa wakulima MUWA chini ya ufadhili wa mradi wa EPINAV.

Akizungumza na SUAMEDIA  Prof. Malongo Mlozi ambae ni mtafiti mkuu wa mradi kutoka SUA amesema kuwa mradi umeamua kuanzisha huduma hiyo ya ushauri kwa njia ya mtandao ili kurahisisha utoaji huduma ili iwe kwa haraka zaidi  kwa wakulima wadogo katika zoezi la kupata elimu ya kitaalamu  ikiwemo kupashana habari za kilimo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WATAFITI NA WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MIRADI YA EPINAV KULETA MAENDELEO NCHINI

Mratibu wa program ya EPINAV Prof. Lusato Kurwijila ( wa tatu kushoto)

akishiriki katika majadiliano ya vikundi wakati wa kongamano lililofanyika

katika ukumbi wa ICE- SUA  Morogoro

 

 

             

      

Na: Bujaga Izengo Kadago

Watafiti na wakulima walioshiriki katika miradi ya EPINAV wametakiwa kutumia kwa vitendo majadiliano katika kongamano la uzoefu na ubunifu uliopatikana katika utafiti  ili kuinua kipato cha wananchi na kuleta maendeleo nchini.

Wito huo umetolewa na mkuu wa Chuo cha Kilimo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof Suzani Nchimbi Msolla alipokuwa akifungua kongamano la tatu na la mwisho la program ya EPINAV, kongamano lililofanyika Jumatano Machi 16 mwezi huu chuoni SUA.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

BINADAMU HAWAPASWI KUFANYA KAZI YA MUNGU KWA MAZOEA-MAMEO

         

Na:Alfred Lukonge

 

Askofu Jacob Mameo Ole Paulo mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Morogoro amesema binadamu wote ni watumwa mbele za Mungu hivyo hawapaswi kuifanya kazi yake kwa mazoea kama kweli wanataka upatanishi naye.

Askofu  Mameo amezungumza hayo alipofanya ziara KKKT Usharika wa Majengo kata ya Kihonda mjini Morogoro  siku ya Jumapili tarehe 13 Machi na kubainisha kuwa “ Dayosisi inaendelea vizuri na hata kelele mnazozisikia kuhusu migogoro ya ardhi sio kelele kwani hazijasitisha shughuli yoyote ndani ya Dayosisi”.

 
Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                                         PICHA NA MTANDAO

BILA ELIMU HAMSINI KWA HAMSINI KWENYE TAALUMA NI NDOTO - DSI

                                            

Na: Farida Mkongwe

 
Imeelezwa kuwa wanawake wasipojiendeleza kielimu katika Nyanja mbalimbali ikiwemo sayansi na taaluma nyingine basi suala la kufikia uwiano wa hamsini kwa hamsini   katika nafasi mbalimbali za madaraka litakuwa ni ndoto kutokana na idadi ndogo ya wanawake wanaosoma na kufanya kazi katika taasisi za elimu ya juu ukilinganisha na wanaume.

 

Hayo yameelezwa na Mhadhiri Msaidizi katika Chuo cha SUA cha sayansi ya jamii na hyumanitia Judith Kahamba wakati akitoa mada kwenye semina ya jinsia iliyofanyika katika chuo cha Ardhi mjini Morogoro wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

KIWANGO CHA UVUNAJI MISITU TANZANIA KIPO CHINI UKILINGANISHA NA PERU NA INDONESIA -UTAFITI

                                   

Na: Farida Mkongwe

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Misitu (CIFOR), umebainisha kuwa kiwango cha uvunaji misitu hapa nchini ni kidogo ukilinganisha na nchi za Peru na Indonesia.

Akizungumza na SUAMEDIA  mtafiti msaidizi kutoka SUA Baraka Naftal amesema kuwa matokeo ya utafiti huo ni ya kujivunia na kwamba iwapo elimu zaidi itaendelea kutolewa kwa watanzania basi kiwango cha uvunaji misitu hapa nchini kitaendelea kuwa chini zaidi ukilinganisha na nchi nyingine.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WANAWAKE WAJIFUNZE SHERIA ILI WADAI HAKI ZAO- RAAWU

          

Na: Farida Mkongwe                    

Wakazi wa mkoa wa Morogoro hususani  wanawake wametakiwa kujenga utamaduni wa kuzisoma na kuzielewa sheria zilizopo hapa nchini hasa zile zinazowahusu ili waweze kudai haki zao katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo wanayofanyia kazi.

Wito huo umetolewa na katibu wa RAAWU mkoa wa Morogoro Bw. Baraka Issa wakati akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kufuatia wanawake wengi walioshiriki katika maadhimisho hayo kuonyesha kutokielewa vema kifungu namba 33 cha sheria ya ajira na mahusiano kazini, sheria namba 6 ya mwaka 2004 kinachozungumzia haki ya mwanamke kupata likizo ya uzazi baada ya kujifungua.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

MAMA WA KIVIETNAM AJIFUNGUA MAPACHA WENYE BABA TOFAUTI

PICHA NA MTANDAO   

Na: BUJAGA E. KADAGO NA BBC SWAHILI

Katika hali isiyo ya kawaida, mama mmoja raia wa Vietnam amejifungua watoto mapacha lakini  wenye baba tofauti hali ambayo imethibitishwa na wataalamu wa afya nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la uingereza BBC, hali hiyo ilibainika baada ya uchunguzi wa vinasaba (DNA) kufuatia wazazi wa mama huyo kubaini utofauti wa mapacha hao.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

WANAWAKE WA TAASISI ZA ELIMU MKOANI MOROGORO KUADHIMISHA SIKU YA MWANAWAKE DUNIANI

                                                

Na: Suzane Cheddy


Wanawake kote nchini wameaswa kuongeza juhudi katika nyanja za elimu, uchumi na uongozi ili kuweza kubadilisha mtazamo wa kijinsia ifikapo mwaka 2030.

Hayo yamesemwa na mkuu wa chuo cha ardhi Morogoro Bw. Desderius kimbe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia, maadhimisho yaliyofanyika chuoni hapo machi 8 na kusema kuwa ni wajibu wa kila mwanamke kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kunakuwa na haki sawa kwa wote katika uongozi wa juu, elimu  na uchumi kwani watu wengi hufikiri kuwa mwanamke hawezi kusimama na kutoa maamuzi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WANAWAKE WATAKIWA KUPUNGUZA UZITO ILI WAWE NA AFYA BORA


                                       

Na: Farida Mkongwe

Zaidi ya asilimia 82 ya wanawake waliojitokeza kupima uzito katika kituo cha zahanati ya kata ya mji mpya iliyopo Kaloleni manispaa ya Morogoro wamebainika kuwa na unene uliokithiri huku zaidi ya asilimia 17 ya wanawake wote waliopima uzito ndiyo walioonekana kuwa na uzito unaoendana na urefu waliokuwa nao.

Kwa mujibu wa muuguzi mkunga wa zahanati hiyo bi. Alice Joshua Malunde kati ya wanawake 47 waliojitokeza kupima uzito wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, wanawake 39 wameonekana kuwa na uzito mkubwa ambao haulingani na urefu waliokuwa nao hali ambayo inatafsiriwa kuwa ni unene uliokithiri.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

Subcategories

Page 44 of 52