UGIRIKI YAHITAJI MGAWANYO SAWA WA WAKIMBIZI.

                                                                                                                                               

                                       PICHA NA MTANDAO

Na: Alfred Lukonge/BBC NEWS

Kufuatia wito uliotolewa na nchi za Balkani na Austria hivi karibuni kuhusu kupunguzwa kwa wahamiaji wanaovuka mipaka yao, nchi ya Ugiriki inataka kupinga maazimio yoyote yatakayofikiwa kwenye mkutano ujao wa viongozi wa jumuiya ya  ulaya iwapo nchi wanachama hazitakubaliana kuweka uwiano sawa wa kugawana wakimbizi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 
 

ZIKA YAFANYA WANASAYANSI KUTOKA MAREKANI KWENDA BRAZIL

 

                                         PICHA NA MTANDAO 

       

Na: Alfred Lukonge/BBC Swahili

Timu ya wanasayansi kutoka Marekani imekwenda jimbo la Paraeeba lililoko kaskazini magharibi mwa Brazil kutafiti uhusiano wa watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na virusi vya Zika.

Wanasayansi hao kutoka kituo cha CDC kinachojishughulisha na udhibiti na uzuiaji magonjwa nchini Marekani ilienda kwenye maeneo yalioathirika na kuchukua sampuli ya damu pamoja na kufanya mahojiano na akinamama waliozaa watoto wakiwa na vichwa vidogo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

MIPAKA KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KATIKA BONDE LA MGONGOLA KUWEKWA

  

                                      PICHA NA MTANDAO

         
              


Na: Susane Cheddy

Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mh.Mwigulu Lamek Nchemba amewataka wananchi wa  tarafa ya Mvomero kuweka mipaka baina  ya wakulima na wafugaji katika bonde la Mgongola ili kuepusha mgogoro uliopo kati yao.

Waziri Nchemba amesema hayo Jumapili februari 22 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Dihombo  kujadili mgogoro wa mpaka wa eneo la bonde la Mgongola na kusema ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha anaheshimu  utaratibu utakaowekwa na kufuata sheria zilizowekwa ili kulinda amani na utulivu na wanachi wa eneo hilo  kuweza kuishi kwa amani.


Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WANASAYANSI WAPINGA MAJI KUBADILI RANGI YA NGOZI

        

Na  Catherine Mangula  Ogessa

Watanzania wametakiwa kuondokana na dhana ya kwamba kunywa maji mengi kunasaidia kubadilisha rangi ya ngozi na  kuwa nyeupe.

Mtaalamu wa chakula na Lishe kutoka Idara ya Sayansi ya chakula na Teknolojia ya chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Dr. Akwilina  Mwanri alisema kuwa kitaalamu maji hayawezi kubadili rangi asili ya mwanadamu  aidha kutoka nyeusi na kuwa nyeupe au nyeupe kuwa nyeusi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

SUMATRA MKOANI MOROGORO YAWATAKA WAMILIKI WA MAGARI YA ABIRIA KUFUATA SHERIA

        

Na: Susane Cheddy

Mamlaka ya uthibiti wa  usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) katika manispaa ya Morogoro imewataka wamiliki wa magari ya abiria yanayotoa huduma  ndani ya manispaa hiyo  kuhakikisha wanafuata sheria zilizowekwa ili kuondoa usumbufu kwa madereva na abiria wanaotumia usafiri huo.

Hayo yamesemwa na  Afisa Mfawidhi wa SUMATRA mkoa wa Morogoro Bw. Rahimu Kondo wakati akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake hivi karibuni na kubainisha kuwa ili gari liweze kuruhusiwa kutembea barabarani ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na SUMATRA.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

BABA MTAKATIFU AHAMAKI BAADA YA KUVUTWA KWA NGUVU.

 

                               PICHA NA   MTANDAO

        

Na Bujaga Izengo Kadago/mtandao

 

Baba mtakatifu francis wa kanisa katoliki duniani, ambaye daima huwa mtulivu na anayependa kuwa karibu na umma, hivi karibuni alipoteza tabasamu lake baada ya mtu mmoja kumvuta kwa nguvu hadi akamwangukia mtoto mlemavu aliyekuwa katika baiskeli yake.

 

Kwa mujibu wa picha za video zinamwonesha papa Francis akitembea jirani na umati wa watu katika uwanja wa mpira wa Mexico city  na kusimama kusalimiana na watoto waliokuwa wamekaa.

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

JAAFARI MPONDA ATOA KASWIDA MPYA “ TWAKUOMBA YAKARIM”

           

Na: HUSNA YAHYA

Muimbaji wa  nyimbo za dini ya kiislam  (kaswiida) Jaafari mponda  hivi karibuni ametoa wimbo mpya uitwao “Twakuomba Yakarim” aliomshirikisha bw. Abdullah Yussuph ambaye ni  mlemavu wa ngozi(Albino).

“Nimeamua kumshirikisha mlemavu  wa ngozi katika kaswida yangu kama sehemu ya kuwafariji ili na wao waweze kujiona kuwa na wao ni watu muhimu katika jamii  wasikatishwe tamaa na watu wachache wanaowafanyia ukatili kwa kuwakata viungo vyao” alisema Bw. Mponda.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WAANDISHI WATAKIWA KUTHUBUTU KUIBUA MAWAZO

        

Na: Catherine Mangula  Ogessa

Waandishi wa habari wametakiwa kuacha uoga na badala yake wathubutu kuibua mawazo mbalimbali ili wapate ruzuku kutoka Wakfu wa tasnia ya habari Tanzania TMF.

Kauli hiyo ilitolewa na mkurugenzi Mtendaji wa TMF Bw. Ernest Sungura wakati akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro na Pwani  kwenye mafunzo ya uelimishaji juu ya uombaji ruzuku kupitia mtandao.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

SINTOFAHAMU YAIBUKA KWA WAFANYABIASHARA BAADA YA BEI YA SUKARI KUPANDA

                                   PICHA  NA  MTANDAO  

       

Na: ADAM RAMADHAN

Kumekuwa na hali ya sintofahamu miongoni mwa wafanyabiashara wa maduka ya rejareja mjini Morogoro baada ya bei ya sukari kupanda ghafla katika maduka ya jumla na kufikia elfu 90 ukilinganisha na bei ya awali ya shilingi elfu 85 kwa mfuko wa kilo 50.

Wakizungumza na SUAMEDIA baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya  rejareja wamesema bei imepanda kutoka shilingi elfu 85 bei ya kutoka Februari mwaka jana hadi kufikia elfu 90 Januari 2016,ikiwa wao bado wanawauzia wananchi bei ileile ya shilingi 2000.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

WANANCHI MKOANI MOROGORO WAUPONGEZA UONGOZI WA DR.JOHN POMBE MAGUFULI

  

                                               PICHA NA MTANDO

       

Na: Susane Cheddy

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Morogoro wameupongeza uongozi wa Rais wa awamu ya tano Mh. Dr.John Pombe Magufuli kutokana na kuongezeka  kwa mapato katika kipindi cha siku 100 tangu kuingia  madarakani tofauti na Marais wengine waliotangulia.

Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya wafanyabiashara wa matunda eneo la nanenane akiwemo bibi. Halima abdallah na kusema kuwa Raisi Magufuli amefanya kazi nzuri ndani ya muda mfupi wa uongozi wake hivyo amewataka wananchi kuendeleza ushirikiano ili kuleta maenedeleo ya nchi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

UTAFITI WABAINI WANACHUO WENGI KUBADILI MALENGO YAO KUTOKANA NA MAZINGIRA

           

Na: ALFRED LUKONGE

Utafiti mdogo uliofanywa na SUAMEDIA kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro katika kampasi kuu umebaini malengo ya wanafunzi waliyokuwa nayo hapo awali yamebadilika kutokana na mazingira waliyokutana nayo, hali ambayo itasaidia kuleta tija katika sekta ya kilimo.

Akizungumza na SUAMEDIA mwanafunzi Christian Mushi anayesoma shahada ya utafiti wa udongo katika chuo hicho amesema lengo lake lilikuwa ni kusomea udaktari lakini baada ya kukosa nafasi kwenye vyuo vya  udaktari alipata ushauri kutoka kwa kaka yake asomee utafiti wa udongo chuoni  SUA.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

NYARAKA NA PICHA ZA PAPA AKIWA NA RAFIKI YAKE WA KIKE ZAWEKWA HADHARANI.

 

                                         PICHA NA MTANDAO

                                           

Na: Susan Cheddy/BBC NEWS

Mamia ya barua na picha  yanayoelezea mahusiano ya karibu yaliyokuwepo kati ya Mwanafalsafa Anna-Teresa Tymieniecka  na Mkuu wa zamani wa kanisa katoliki papa John paul II yaliyodumu kwa miaka 30 sasa yamewekwa wazi kwa umma.

Mwanafalsafa mzaliwa wa  Marekani bi. Tymieniecka ambaye wakati huo alikuwa mke wa mtu, anajidhihirisha jinsi alivyokuwa karibu na papa John kutokana na barua na nyaraka hizo zilizohifadhiwa mbali na macho ya umma katika Maktaba ya Taifa ya Poland kwa miaka mingi na zilionesha uhalisia wa papa huyo, ambaye alifariki mwaka 2005.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

UTURUKI YAKANUSHA MAJESHI YAKE KUINGIA SYRIA.

                    

Na: Susan Cheddy/BBC NEWS

Wito umetolewa kwa umoja wa mataifa kuchukua hatua dhidi ya majeshi ya uturuki yanayojaribu kuvuka mpaka na kuingia Syria na kusema kuwa huo ni ukiukaji wa uhuru wa Syria.

Taarifa hiyo imetolewa  kufuatia barua ya malalamiko kutoka Syria kwamba jeshi la uturuki limekuwa likiruhusu askari wapatao 100 kuvuka  mpaka na kuingia Syria.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

KUFUNGA KWA RESMA NI ISHARA YA KUKUMBUKA MATESO YA YESU

           

Na: ALFRED LUKONGE

Waumini wa dini ya kikristo duniani kote wiki iliyoishia februari 10 siku ya  Jumatano waliadhimisha jumatano ya majivu kama ishara ya kuanza kwa kipindi cha Kwaresma ambacho huambatana na kufunga kama ishara ya kukumbuka mateso ya mwokozi wao Yesu kristo.

Akizungumza na SUAMEDIA  Mch. Kiongozi kutoka KKKT usharika wa Kigogo jijini Dar es Salaam Richard Hananja amesema lengo la kipindi hiki cha kanisa ni watu wapate kutubu kwa kuwa wayahudi wa enzi hizo walitumia majivu kama ishara ya toba  wapate kupewa msamaha wa dhambi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

ZIKA YAFANYA JIMBO LA FLORIDA MAREKANI KUTANGAZA DHARURA

        

Na: ALFRED LUKONGE

Hali ya dharura imetangazwa na Gavana wa jimbo la Florida nchini Marekani Bw. Rick Scott katika kaunti nne kutokana na virusi vya Zika baada ya kesi tisa za ugonjwa huo kugundulika  jimboni humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na maafisa wa afya wanaamini mambukizi hayo yametokea  kufuatia kuingia jimboni humo kwa watu walioathirika na ugonjwa huo wa zika kutoka katika nchi zilizoathirika za amerika ya kusini.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

WANAWAKE NA WATOTO NI WAHANGA WAKUU WA MABADILIKO YA TABIA NCHI

         

Na:GELARD LWOMILE

Mabadiliko ya tabia nchi kama ukame, mafuriko, upepo mkali na kuongezeka kwa joto vimetajwa kama visababishi vya hali ngumu ya kimaisha na vinavyoleta umaskini mkubwa kwa wakulima na wananchi wengine wanaoishi katika maeneo hayo.

Hayo yamesemwa na Dk. Samwel Kabote Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wakati akiwasilisha matokeo ya Utafiti juu ya athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na namna ya kukabiliana nazo kwa mtazamo wa kijinsia katika kilimo na maliasili kwenye maeneo kame ya Tanzania uwasilishaji uliofanyika katika wilaya za Iramba mkoani Singida na Meatu mkoani Simiyu.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

WANAFUNZI CHUO CHA ARDHI WAFANYA ZIARA MKOANI MOROGORO

                                                                                         

Na: HALIMA KATALA

Wanafunzi wa mwaka wa pili wa  Chuo Kikuu cha Ardhi kilichopo Dar-es-salaam wamefanya ziara ya kimasomo mkoani Morogoro kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na uzalishaji wa maji pamoja na vyanzo vyake vikuu vilivyopo mkoani Morogoro.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

  

 

 

 

CHRIS ROCK MCHEKESHAJI MWEUSI AWASALITI WENZAKE KATIKA HAFLA ZA OSCAR.

        

Na BUJAGA I. KADAGO na MITANDAO

 

katika hali ya kushangaza msanii/mchekeshaji  mwafrika Chris Rock ameweka wazi kuwa yeye atashiriki katika hafla za ‘oscar’ licha ya wasanii wenye asili ya kiafrika kutangaza rasmi kuzisusia sherehe hizo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

 

 

 

 

                                       PICHA NA MTANDAO

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA MWELEKEO WA MVUA KWA MIEZI YA JANUARI NA FEBUARI

 

Na Consolata Philemon

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za msimu kwa miezi ya Januari na Februali 2016 katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka ambapo imesema mifumo ya hali ya hewa iliyopo inatarajiwa kuendelea kuimarika.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

                                               PICHA NA MTANDAO

WATUHUMIWA WAWILI WA MAUAJI WAACHIWA HURU NA KULIPWA KITITA CHA FEDHA.

  

 

  

 

 

 

Na   Mtandao

Jimbo la Los Angeles nchini Marekani  linatarajiwa kuwalipa fidia ya zaidi  shs. bilioni 50 kwa watu wawili baada ya kugundulika kuwa walihukumiwa kimakosa kwenda jela kwa madai ya kuua.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

                                                  PICHA NA MTANDAO

Subcategories

Page 46 of 52