WATUHUMIWA NANE WA UPOTEVU WA MAKONTENA BANDARINI KUFIKISHWA MAHAKAMANI

PICHA NA MTANDAO   

Na: ADAM RAMADHAN

Watuhumiwa  wanane  wa  upotevu  wa makontena 349  bandarini Dar Es Salaam  akiwemo  kamishna  wa  kodi na  forodha  TRA  Bw.Tiagi Masamaki wamefikishwa katika mahakama ya  hakimu  mkazi  kisutu jijini Dar es salaam leo ijumaa ya   desemba 4.

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

MWANASHERIA MKUU ASEMA ASIHUSISHWE NA WAKUU WA MIKOA WANAOSITISHA LIKIZO ZA WATUMISHI

  PICHA NA MTANDAO     

 

Na:TATYANA CELESTINE

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amezungumzia suala la wakuu wa mikoa kutoa matamko ya kusitisha likizo za watumishi wa umma kwa kuwataka wafanye kazi tu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Kituo cha Runinga cha Azam, Masaju amesema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuhusu taarifa za kuwepo matamko hayo kutoka kwa baadhi ya wakuu wa mikoa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

"WAFANYABIASHARA WAKWEPA KODI NAWAPA SIKU SABA"- DR.POMBE MAGUFULI

    

Na:TATYANA CELESTINE

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.John  Pombe  Magufuli amewapa siku saba kuanzia tarehe 03/12/2015 wafanyabiashara wote ambao waliingiza mizigo yao bila kulipa kodi wakalipe kwani baada ya hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria
 
Hayo  yamesemwa jana Ikulu  jijini Dar es Salaam na Mheshimiwa Rais katika Mkutano wake na wadau wa Sekta binafsi  alipoamua kufanya mazungumzo nao pamoja na kuwasikiliza maoni  yao ikiwa ni sehemu ya ahadi zake katika kipindi cha kampeni za kuomba kura za kiti cha Urais,lengo likiwa ni kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta binafsi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi....... 

AFISA ARDHI MOROGORO APEWA SIKU 14 ZA KUJIELEZA KWA NINI ASIFUKUZWE KAZI

      

Na:TATYANA CELESTINE

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Jumanne Sagini ametoa siku 14 kwa afisa ardhi, Mhandisi wa Majengo na Afisa Mipango Miji Manispaa ya Morogoro kuandika maelezo ya kwanini wasifukuzwe kazi kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango na kukiuka maadili ya utumishi wa Umma

 

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

WAZIRI MKUU AVAMIA TENA BANDARINI NA TRL........ABAINI UPOTEVU WA MAKONTENA ZAIDI YA 2431

    

HABARI MPASUKO

Na:TATYANA CELESTINE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya tena ziara ya kushtukiza bandarini na Shirika la Reli Tanzania (TRL). Akiwa bandarini amekagua mfumo wa utoaji na uingizaji mizigo bandarini.

 

Katika maongezi ya awali Meneja wa Bandari alimuhakikishia kuwa mfumo hauruhusu kontena kuibiwa cha ajabu Waziri Mkuu alienda na Ripoti ya Ukaguzi na kumuonyesha majina ya waliopitisha makontena zaidi 2431 bila kulipiwa kodi.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

 

ADA ELEKEZI KWA WANAFUNZI KUJULIKANA DESEMBA 15

      

Na:TATYANA CELESTINE

 

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imewataka wazazi na walezi wenye wanafunzi wanaotegemea kuanza masomo au kuendelea na masomo katika shule binafsi mapema Januari mwezi ujao, kuvuta subira hadi Desemba 15, mwaka huu serikali itakapotoa maelekezo mbalimbali ikiwemo suala la ada elekezi.

 

Akizungumzia na vyombo vya habari kuhusu hatua zinazofanywa hivi sasa na serikali kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome, alisema timu mbili hivi sasa zinafanya kazi ya uchambuzi wa michanganuo ya ada kwenye shule hizo, na baada ya muda mfupi uamuzi utatolewa.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

MAGUFULI MACHO KWA MACHO NA WAWEKEZAJI JIJINI DAR LEO

      

  

Na:TATYANA CELESTINE

RAIS John Magufuli anatarajiwa kukutana na wafanyabiashara na wawekezaji jijini Dar es Salaam leo. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais kukutana na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji tangu aingie madarakani.

 

 Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli atakutana na jumuiya hiyo Ikulu kwa nia ya kufahamiana na kuona namna ya kushirikiana kufikia malengo ya maendeleo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

MILIMA YA TAO LA MASHARIKI HATARINI KUTOKANA NA MITI VAMIZI

   

Na: GERALD LWOMILE

Wakulima katika Milima ya Usambara Mashariki wako katika hatari ya kushindwa kuzalisha mazao kutokana na miti vamizi aina ya Mihavi kuvamia katika milima hiyo na kuleta athari kubwa ikiwa ni pamoja na kuharibu bioanuai katika milima hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mradi wa Utafiti juu ya miti vamizi  Profesa George Kajembe na Prof  Urs Schaffer ambaye ni Mkuu wa Mradi katika warsha ya kimataifa juu ya utafiti wa miti vamizi katika milima ya Usambara mashariki eneo la hifadhi asili ya Amani  wilayani Muheza mkoani Tanga.

Bofya hapa kwa Habari zaidi.......

WANANCHI WAFUATE USHAURI UNAOTOLEWA NA MAAFISA KILIMO KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZA VULI

 PICHA NA MTANDAO  

 

Na: AYOUB  MWIGUNE

Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Mashariki imesema kwamba mvua zinazoendelea sasa ni mvua za vuli na sio mvua za masika hivyo wananchi wanapaswa kufuata ushauri kutoka kwa maafisa kilimo walio karibu nao ili waweze kujua ni mazao yapi ambayo wanaweza kuyapanda katika msimu huu wa mvua za vuli

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

MZAZI ANACHANGIA 25% ILI KUONGEZA UFAULU KWA WATOTO MASHULENI- ENG .DOROTH MTENGA

    

Na:TATYANA CELESTINE

Wazazi na Walimu wametakiwa kushiriana kwa karibu ili kwa kuweza kuinua taaluma ya watoto wawapo mashuleni na hivyo kuwajengea msingi ulio bora katika maisha yao ya kila siku.

Akizungumza wakati wa kutoa pongezi kwa Taasisi ya kielimu chini ya Shirika la Montfon Brothers katika siku ya wazazi na mahafali ya watoto shule ya awali mwaka 2015 Mgeni Rasmi Meneja wa Tanroad Mkoa wa Morogoro Injinia Doroth Mtenga amesema wazazi ni nguzo ya kwanza kwa watoto na ili wafanikiwa ni lazima wanapowapeleka shuleni wahakikishe wanashirikiana na walimu wa watoto hao kikamilifu.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

MTOLEE MUNGU SADAKA KWA FAIDA YA VIZAZI VYAKO

   

Na: ALFRED LUKONGE

Imeelezwa ukimtolea Mungu kwa uaminifu  baraka zitaenda paka kwa vizazi vyako  kwakuwa hata nchi zilizoendelea kama Marekani na Israeli ukifuatilia historia zao kuna watu walikuwa waaminifu kwa Mungu kwenye suala la utoaji na ndio maana zimeendelea hadi hii leo.

Hayo yamesemwa na Mwl. Maimu Dafa alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya Dunia tambala bovu ya kwaya ya uinjilisti ya Sayuni uliofanyika katika kanisa la kilutheli usharika wa Majengo mjini Morogoro Jumapili ya wiki iliyopita na kubainisha “utoaji watu wengi unawasumbua paka wanaacha kuja kanisani kwasababu shetani anawapanda mbegu mbaya”.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

WANAKWAYA DAR WAFANYA ZIARA KATIKA MJI WA MOROGORO

   

Na: ALFRED LUKONGE

Kwaya ya Uinjili ya Agape kutoka Usharika wa Azania Front jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita imefanya utalii wa ndani kutembelea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika mji wa Morogoro.

Katika ziara hiyo Agape walipata fursa ya kutembelea baadhi ya maeneo ya vivutio kwenye mji wa Morogoro ikiwemo Jahazi Delmon Garden, bwawa la Mindu, na shule ya sekondari Junior Seminary.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

WANACHUO WAJASILIAMALI WASIFUATE FIKRA MGANDO ZA WAZAZI- DK.TEMU

    

Na: ALFRED LUKONGE

Msimamizi wa Shirika la wajasiliamali  wanafunzi waliohitimu Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro ( SUGECO) Dk. Anna Temu amesema watahakikisha wanatimiza lengo lao ambalo ni kufanya watu kuwa wajasiliamali na kwenda kinyume na fikra mgando za wazazi wengi wanaotaka watoto wao wanapohitimu masomo wapate fursa ya kuajiriwa kwenye mashirika mbalimbali.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

SUA YAONGEZA IDADI YA WAHITIMU KWA ASILIMIA 23

      

Na: FARIDA MKONGWE

Idadi ya wanafunzi waliohitimu shahada mbalimbali kutoka kwenye Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA imeongezeka kutoa wanafunzi 1935 waliohitimu mwaka jana hadi kufikia wanafaunzi 2384 waliohitimu mwaka huu sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 23.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

UKIWA NA WAZO LA BIASHARA UWE NA UHAKIKA WA KUPATA FAIDA-PROF. LEKULE

      

Na: ALFRED LUKONGE

Mkurugenzi wa kampuni ya Tanfeeds L.T.D iliyopo Mjini Morogoro inayojishughulisha na utenegenezaji wa vyakula vya mifugo Prof.Faustine Lekule amesema mtu akiwa na wazo la biashara awe na uhakika wa kupata faida huko mbele na sio kufuata mkumbo.

Prof. Lekule amesema hayo wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa siku mbili wenye lengo la kubadilishana ujuzi kwa wanafunzi waliowahi kusoma Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo Morogoro (SUA) maarufu kama Majalisi kwenye ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Elimu ya kujiendeleza (ICE) na kubainisha “ hili biashara ifanikiwe lazima uwe na washirika wa kibiashara ndio maana  ninashirikiana na watu mbalimbali kama WFP, World Vision,YARA na wengine wengi”.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

MAJALISI WAPATA FURSA YA KUONYESHA MIRADI YAO

 

 

Na: HALIMA KATALA

Wanafunzi waliowahi kusoma Chuo  Kikuu cha Sokoine cha Kilimo  SUA miaka iliyopita   maarufu kama Majalisi,  wamepata fursa ya kuonesha miradi   mbalimbali wanayoifanya ikiwemo ile ya ujasiriamali kwenye sekta ya kilimo na ufugaji kama njia mojawapo ya kuendeleza ujuzi walioupata wakiwa chuoni hapo.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa wanachama hao, mwenyekiti wa chama hicho Prof. Gabriel Mbassa amesema ana imani wanachama hao wamenufaika vya kutosha kutokana na mada kuwa ni za vitendo zaidi ambapo pia ametoa wito kwa wanachama waliopo SUA wakati mwingine kujitokeza kwa sababu ni uwanja wa nyumbani na kwamba   mikutano  kama hiyo haiwalengi  Maprofesa wa SUA pekee.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WAFANYAKAZI , WANAFUNZI SUA WAZINGATIE MUDA KATIKA SHEREHE ZA UTOAJI WA ZAWADI- PROF. PETER GILLAH

 

    Na: CONSOLATA PHILEMON                                                                

Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) upande wa Taaluma Prof. Peter Gillah amewataka viongozi mbalimbali wa chuo hicho, wageni waalikwa na wanafunzi watakaoshiriki kwenye shehere ya utoaji zawadi na majalisi wa chuo itakayofanyika siku ya Alhamis tarehe 26 mwezi huu kufika kwa wakati kwenye eneo la tukio ili ratiba ya sherehe hizo  iweze kwenda kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza na SUAMEDIA Prof. Gillah amesema sherehe ya utoaji zawadi itafanyika kuanzia saa 2.00 hadi saa 5.30 asubuhi kwenye ukumbi wa baraza la chuo uliopo jengo kuu la utawala, Kampasi kuu ya chuo ambapo mgeni rasmi atakuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mawasiliano , Sayansi na Teknolojia  Mheshimiwa Dkt Yamungu Kayandabila.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

WAKAZI WA MANISPAA YA MOROGORO WAVUTIWA NA AGIZO LA MAGUFULI

 

 

Na: HUSNA YAHYA

Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Morogoro wamelipokea kwa mtizamo tofauti agizo lililotole wa na Rais Dk. John Pombe Magufuli la kufuta sherehe za sikukuu ya uhuru kwa mwaka huu na badala yake watu waitumie siku hiyo ya 9 Desemba kufanya kazi za usafi katika maeneo mbalimbali

Wakizungumza na SUAMEDIA baadhi ya wakazi  waliounga mkono kauli hiyo akiwemo bi. Grace Mapunda na  bw. Limangwa adam ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wamesema kuwa ni vizuri kuwajenga watanzania katika utendaji kazi na pia kupunguza matumizi ya fedha ambazo hutumika katika maandalizi ya shehere hizo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

WANAFUNZI WA SUA WAPASWA KUELIMISHA JAMII KUHUSIANA NA UGONJWA WA UKIMWI.

 

Na: AYOUB  MWIGUNE

Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wametakiwa kuwa mabalozi wazuri kuhusu kuelimisha jamii kuhusiana na ugonjwa wa UKIMWI ambao umeendelea kuwa tatizo hapa nchini.

Akizungumza kwenye semina ya ukimwi bi. Rebecca Shemeta kwa niaba ya Daktari mkazi wa SUA Omary Kasui,  amewasihi wanafunzi kuzingatia yale waliyofuata chuoni pamoja na kujiepusha na tamaa mbalimbali ambazo zinaweza kuwaletea wanafunzi hao maambukizi ya UKIMWI.

 Bofya hapa kwa Habari zaidi..........

 

IDARA YA USALAMA SUA YA ENDESHA OPERESHENI

 

Na: HALIMA KATALA

Idara ya Usalama katika  Kituo cha Polisi  Wasaidizi  cha SUA kimeendesha zoezi  la kukamata pikipiki  na magari yanayoingia na kutoka Chuoni hapo  kwa ajili ya  ukaguzi  wa kiusalama.

Akiongea na SUAMEDIA  Kaimu Mkuu Idara ya Usalama SP. Ally Omary Mtunguja amesema kuwa zoezi hilo ni la kushtukiza ila litakuwa ni endelevu na ni kwa ajili ya kulinda Usalama  hasa katika kipindi hiki cha  kuelekea kufanyika  Mahafali ya chuo.

Bofya hapa kwa Habari zaidi..........