KWAYA YA SAYUNI KUZINDUA ALBAM YAO YA DUNIA TAMBALA BOVU
Na: ALFRED LUKONGE Mwenyekiti wa kwaya ya uinjilisti ya Sayuni KKKT usharika wa Majengo mjini Morogoro Winfred Ngullo amesema watu watakaofika kwenye uzinduzi wa albamu yao ya Dunia tambala bovu utakaofanyika Jumapili wiki hii kuanzia saa 3:00 asubuhi wategemee ubunifu wa hali ya juu kwenye sauti, hala pamoja na uchezaji. Katika uzinduzi huo utakaofanyika usharikani hapo , mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Bw. Maimu Daftari mmoja wa marafiki wa siku nyingi wa kwaya hiyo huku wageni wengine wakiwa ni kutoka usharika wa Mazimbu, Bungo, Mji Mpya, CRDB mji wa Morogoro, wageni kutoka Dar es Salaam na Tanga pamoja na kwaya ya vijana kutoka usharika wa Azania Front, Kola na kwaya kuu kutoka usharika wa Mazimbu. |
MAJALISI WASEMA “USAFI LIWE JAMBO ENDELEVU ILI KUEPUKA MAGONJWA”
TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA MPUNGA CHA SHADIDI YABORESHA MAISHA YA WAKULIMA.
BUNGE LA 11 LA SHAURIWA KUTUNGA SHERIA KALI YA KUSIMAMIA SERA YA ELIMU
MAJALIWA RASMI KUAPISHWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA
PICHA NA MTANDAO |
Na: HUSNA YAHYA Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amemuapisha rasmi Mh. Majaliwa Kasim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika Ikulu ndogo chamwino mjini Dodoma.
Sherehe hizo za kuapishwa kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma zimehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein na wabunge wa jamuhuri ya muungano la Tanzania. |
RAIS MAGUFULI AFUNGUWA BUNGE, ASISITIZA FALSAFA YA HAPA KAZI TU
DR MAJALIWA NI WAZIRI MKUU MTEULE WA TANZANIA
PICHA NA MTANDAO |
Na:AMINA B. MAMBO Mbunge wa Ruangwa Dk. Majaliwa Kassim Majaliwa ametangazwa rasmi kuwa Waziri Mkuu mteule wa Tanzania baada ya jina lake kupendekezwa na Rais na baadaye kuthibitishwa na wabunge kwa kupigiwa kura ambapo aliweza kupata ushindi kwa asilimia 73.5 ya kura zote zilizopigwa. Akitangaza matokeo hayo Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kuwa ushindi alioupata Mh. Majaliwa ni ushindi wa kimbunga ambao unatokana na uaminifu wake katika utendaji wa kazi na kwamba wapo tayari kushirikiana naye katika ili taifa liweze kusonga mbele. |
“HAPA KAZI TU”– PROF. MONELA
PICHA NA MNGEREZA MNTAMBO |
Na: FARIDA MKONGWE Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kwa bidii ili kuendana na falsafa ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli isemayo hapa kazi tu. Wito huo umetolewa na Makamu wa Mkuu wa chuo hicho Prof. Gerald Monela wakati akizungumza na wafanyakazi wa SUA katika mkutano uliofanyika siku ya Jumatano chuoni hapo ambapo aliwataka wafanyakazi kwenda na kasi ya mabadiliko ya kisiasa. |
WAKULIMA WASHIRIKIANE KUDHIBITI PANYA-PROF. MULUNGU
![]() |
Na: CALVIN E. GWABARA Imebainishwa kuwa Udhibiti wa panya wa pamoja kwenye skimu za umwagiliaji imeonekana kuwa ndio njia pekee ya kukomesha hasara itokanayo na panya badala ya udhibiti wa mtu mmoja mmoja. Ushauri huo umetolewa na mtaalamu wa udhibiti wa Panya kutoka SUA kwenye kituo cha udhibiti wa viumbe hai waharibifu Prof. LOTH MULUNGU wakati akizungumza kwenye semina ya uwasilishaji wa matokeo ya utafiti wa kilimo cha mpunga cha shadidi na udhibiti wa panya kwenye sikimu ya umwagiliaji ya mkindo wilayani Movomero mkoani Morogoro. Bofya hapa kwa Habari zaidi..........
|
PHILEMON LUHANJO ATEULIWA KUWA KAIMU MKUU WA CHUO - SUA
![]() |
Na: FARIDA MKONGWE Serikali imemteua Bw PHILEMONI LUHANJO ambaye ni mwenyekiti wa baraza la Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kuwa kaimu mkuu wa chuo hicho kutokana na aliyekuwa mkuu wa chuo AL NOOR KASSUM kustaafu mwezi Machi mwaka huu. Akitoa taarifa hizo kwa wafanyakazi wa SUA Makamu wa Mkuu wa Chuo Prof. Gerald Monela amesema Luhanjo ameanza kukaimu nafasi hiyo kuanzia tarehe 13 mwezi Machi mwaka huu, tarehe ambayo mkuu wa chuo hicho alistaafu rasmi kisheria. |
WANANCHI WA MANISPAA YA MOROGORO WAFURAHISHWA NA UTEUZI WA SPIKA MPYA
![]() |
Na: AYOUB MWIGUNE Wananchi mbalimbali wa Manispaa ya Morogoro wametoa maoni yao na pongezi kwa Spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ambaye alichaguliwa na wabunge wenzake siku ya Jumatatu tarehe 17 mwezi huu. Amanzi Husseni ambaye ni Mkazi wa Magadu katika Manispaa hiyo alimpongeza Mh. Job Ndugai kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge na kumtaka aweze kufanya kazi kwa kujali maslahi ya nchi na kutekeleza yale yote ambayo aliyaahidi kutenda wakati wa kuomba ridhaa kwa wabunge wenzake. |
WAKRISTO WAASWA KUVUNJA MADHABAU CHAFU
Na: ALFRED LUKONGE Siyo kila kifo kinachotokea kwa mwanadamu kimepangwa na Mungu hivyo wakristo wanatakiwa kuvunja madhabau chafu hili tuweze kupambana na hila za mwovu shetani na washirika wake. Hayo yamesemwa na Mchungaji Merry Kyomo kutoka Dayosisi ya Konde wakati akihubiri kwenye siku ya mwisho ya semina ya neno la Mungu katika kanisa la KKKT usharika wa majengo kata ya Kihonda mkoani Morogoro Jumapili iliyopita. |
VIPAJI VYA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU VIPEWE KIPAUMBELE
Na: ALFRED LUKONGE Serikali inatakiwa kuwapa kipaumbele watu wote wenye vipaji na kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwasaidia kuendeleza vipawa vyao hasa kwenye Sekta ya Teknolojia na ubunifu. Hayo yamesemwa na kijana Ansgar Chalila aliyefanikiwa kubuni mashine ya kuzalisha umeme iliyokuwa inasoma 0.5 kwenye kifaa cha Ampia yenye uwezo wa kuwasha taa ndogo akiwa masomoni shule ya Sekondari Charlotte mjini Morogoro. |
CLUB YA UKIMWI SUA KUANDAA TAMASHA KUBWA
![]() |
Na: HALIMA KATALA Club ya Ukimwi ya wanafunzi wa Chuo Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) imendaa tamasha maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusiana na jinsi ya kujikinga na Ukimwi kwa wanafunzi wageni wa mwaka wa kwanza. Akizungumza na SUAMEDIA mwenyekiti wa Club hiyo Okanda Julius amesema kuwa tamasha hilo linatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 21/11/2015 kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 8 mchana na itafanyika katika Kampasi Solomon Mahlangu iliyopo Mazimbu . Bofya hapa kwa Habari zaidi..........
|
JOB NDUGAI ACHAGULIWA SPIKA WA BUNGE LA KUMI NA MOJA
![]() |
Na: AYOUB MWIGUNE Mbunge wa Kongwa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mh. Job Ndugai amechaguliwa kuwa spika wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 254 na kumshinda mpinzani wake Goodluck Ole Medeye wa CHADEMA ambaye anaungwa mkono na Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) aliyepata kura 109. Bofya hapa kwa Habari zaidi..........
|
WANATAALUMA SUA KUFANYA USAFI KATIKA MANISPAA YA MOROGORO
![]() |
NA: GERALD LWOMILE Zaidi ya wahitimu 23 elfu waliomaliza Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) tangia mwaka 1984 hadi mwaka jana wanatarajiwa kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira novemba 21 katika manispaa ya morogoro. Akizungumza na SUAMEDIA Mwenyekiti wa Majalisi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Gabriel Mbassa amesema SUA imeamua kushiriki na wananchi kufanya usafi katika eneo la Mjimpya hadi Mwembesongo mjini Morogoro ili kuikumbusha jamii kutunza mazingira. |
WANAFUNZI WA SUA WAMEASWA KUMPA MUNGU KIPAUMBELE
![]() |
Na: AYOUB MWIGUNE Wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wameaswa kumpa Mungu kipaumbele ili aweze kuwaongoza katika masomo yao. Hayo yamesemwa na Mchungaji wa Kanisa la CCT SUA Emmanuel Faranta katika ibada ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la CCT SUA liliopo katika Kampasi Kuu ya Chuo hicho. |
VIONGOZI WA DINI WAACHE KULA PESA ZA WAJANE NA YATIMA
JOB NDUGAI KUPEPERUSHA BENDERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI
WATANZANIA KUSHAURIWA KUPUNGUZA MATUMIZI YA VIPATO
PICHA NA MTANDAO |
Na: MNGEREZA MNTAMBO Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Morogoro wamewashauri Watanzania wenzao kupunguza matumizi ya vipato vyao hasa katika kipindi hiki cha mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali ili waweze kujipatia maendeleo binafsi. Wakiongea na SUAMEDIA katika maeneo tofauti ya manispaa hiyo wakazi hao wamesema katika kipindi hiki kumekuwa na mfumuko wa bei za bidhaa mfano unga wa sembe umepanda kutoka sh. 750 hadi sh. 950 kwa bei ya jumla huku shilingi nayo ikiendelea kushuka thamani hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini katika matumizi yao ya kila siku. |
Subcategories
Page 49 of 52