MAFUNZO YA UFUGAJI BORA WA KUKU.NOV.2025.
Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA kupitia Taasisi yake ya Elimu ya Kujiendeleza ICE kwa kishirikiana
na Taasisi ya kujenga Uwezo kwa Watu Kujiletelea Maendeleo Afrika ( AICAD ) kwa pamoja
wameendesha Mafunzo ya Ufugaji Bora wa Kuku ambayo yamedumu kwa siku nne (4) yakianzia Tarehe
17.11.2025 hadi Tarehe 20.11.2025.Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ICE
kampasi kuu ya Edward Moringe,Morogoro.Mafunzo hayo yamehudhuliwa na washiriki wapatao 23
kutoka katika mikoa (6) sita ya Tanzania Bara ambayo ni Morogoro,Pwani,Dar es Salaam,Arusha,Mbeya
na Iringa ambapo idadi ya wanawake ni 12 na wanaume ni 13 wakiwa wafugaji wadogo,wakati na
wajasiliamali.Awali Gharama za kuendesha mafunzo haya ilikuwa ni Tsh.100,000/=kwa kila mshiriki
lakini AICAD nao wakachangia nusu gharama kwa kila mshiriki Tsh 50,000,hivyo kuongeza hamasa na ari
kwa washiriki.Mafunzo ya msimu huu wa Nov 2025, yamekuwa ya tofauti kwani mafunzo ya msimu huu
wa November washiriki wenyewe wameweza kupokea vifaranga wa siku moja(day old chick) kutoka
kampuni ya Interchick na kuwalea kwa kufuata kanuni na miongozo yote waliofundishwa na
kuelekezana wakiwa darasani na jambo la faraja hadi wanahitimisha mafunzo yao hakuna kifo hata
kimoja kilichiripotiwa kwa vifaranga hii inaonesha ni namna gani washiriki hawa wamejidhatiti katika
tasnia hii ya ufugaji wa kuku, hili kwetu sisi ni jambo la kujivunia sana na hongera nyingi kutoka kwa
wakufunzi wa mafunzo haya wakiongozwa na Prof.Faustine Lekule,Dr.Juma Yusuph na Ndg.Williamu
Hoza kutoka katika idara ya Sayansi ya Wanyama,Ukuzaji wa Viumbe maji na Nyanda za malisho pamoja
na Washiriki wenyewe.
Mafunzo hayo yalihitimishwa na Mgeni rasmi ambae alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro
Ndugu Hilary Sagara akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh.Musa.Kilakala na kwa upande wa
Management ya Chuo waliwakilishwa na Prof.Akwilina Mwanri kwa niaba ya Makamu Mkuu wa
Chuo.Prof Raphael.Chibunda.
- 21 Nov
- 2025
