SUA YAIBUKA NA USHINDI WA KWANZA KWENYE MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE 2025.KANDA YA MASHARIKI.
Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA kimeibuka na ushindi wa kwanza katika kipengele cha mshindi wa jumla kwenye maonesho ya wakulima nanenane 2025.Akitoa pongezi hizo Makamu Mkuu wa Chuo.Prof.Raphael.Chibunda amewashukuru waoneshaji kutoka idara,ndaki na taasisi zote zilizo chini ya SUA kwa ushirikiano,ubunifu na moyo wa dhati wa kujituma kwa kipindi chote cha maonesho hali iliyopelekea kupata ushindi huo.Pia ametoa pongezi nyingi kwa Mkurugenzi wa ICE.Dkt.Devotha. Mosha na timu yake ambao ndio waratibu wa maonesho hayo kwa niaba ya chuo.Maonesho hayo kwa mwaka huu wa 2025 yalibeba kauli mbiu isemayo.Shiriki kikamilifu ktk kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo,mifugo na uvuvi.

- 09 Aug
- 2025