Habari ya kufurahisha kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), SUA

Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza, (ICE), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), inayo furaha kubwa kuwaarifu kuwa ICE itaendesha mafunzo mahsusi ya muda mfupi kuhusu “Uzalishaji na Utunzaji wa Malisho ya Mifugo” yatakayotolewa kwa mfanyakazi kutoka katika Serikali ya Zambia kuanzia tarehe 18 hadi 22 Aprili 2022.

Tunaamini kuwa mafunzo haya yatafungua fursa nyingi za ushirikiano kati ya SUA na idara nyingine za serikali nchini Zambia.

 

Picha 1: Picha ikionesha malisho ya mifugo aina ya Bricharia (Bricharia brizantha) yaliyolimwa katika shamba la mafunzo (Model Farm) ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, Tanzania

 

Picha 2: Picha ikionesha malisho ya mifugo aina ya Bricharia (Bricharia ruziziensis) yaliyolimwa katika shamba la mafunzo (Model Farm) ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, Tanzania

 

Picha 3: Picha ikionesha malisho ya mifugo aina ya Elephant grass yaliyolimwa katika shamba la mafunzo (Model Farm) ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, Tanzania

 

Picha 4: Miss Grace Ngomalilo- mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, Tanzania akionesha malisho ya mifugo aina ya Rhodes (Chrolis gayana) katika shamba la mafunzo (Model Farm) la Chuo hicho. (Picha zote katika andiko hili ni kwa hisani ya Dk. Innocent Babili)

 

 

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu mafunzo hayo, tafadhali mwandikie barua pepe Dk. Innocent H. Babili kupitia anwani ya ibabili@sua.ac.tz