SUA na SWISSCONTACT Zaimarisha Ujuzi na Ajira kwa Vijana katika Kilimo cha Bustani Manispaa ya Morogoro

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) kimeendelea kueneza kwa jamii ya watanzania na ulimwengu kwa ujumla elimu, maarifa, ujuzi, teknolojia na bunifu mbalimbali zinazozalishwa SUA, na kwa kushirikiana na wadau wengine, hususani SWISSCONTACT katika andiko hili.

Picha: Baadhi ya vijana waliopata mafunzo wakiendelea na shughuli ya kutunza bustani yao iliyopo katika kata ya Mlimani

Kufuatia mafunzo ya muda mfupi yaliyotolewa kwa vijana katika Manispaa ya Morogoro kuhusu Kilimo cha Bustani Kibiashara, matokeo yanayothibitisha kuongezeka kwa ujuzi na ajira kwa vijana sasa yanaonekana waziwazi. Matokeo hayo yamedhihirika wakati Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), SUA ilipofanya ufuatiliaji hivi karibuni wa vijana waliopata mafunzo ya muda mfupi yenye lengo la kuwaongezea vijana ujuzi na ajira katika uzalishaji na utunzaji wa miche ya matunda kibiashara.

Video ifuatayo inadhihirisha namna mafunzo ya muda mfupi ya ICE, SUA yaliyotolewa kwa kushirikiana na SWISSCONTACT yalivyochangia katika kuimarisha ujuzi na ajira kwa vijana katika Manispaa ya Morogoro

Makala hii inapatikana pia kwa lugha ya Kingereza kwa kubofya HAPA au kwenye alama ya bendera inayoonesha lugha ya Kingereza katika tovuti ya ICE

Kwa habari zaidi kuhusu makala hii mwandikie Dk. Innocent Babili at ibabili@sua.ac.tz