Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ilivyosherehekea Ushindi wa Kishindo katika Maonesho ya Nanenane Mwaka 2022, Morogoro, Tanzania

Linapokuja suala la utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo hiki kinahakikisha, wakati wote, kinapeperusha bendera ya Chuo katika viwango vya ubora wa hali ya juu. Ili kuendena na dira ya SUA ya kuwa kiongozi katika mafunzo, utafiti, ugani na huduma, Jumuiya ya SUA, kama sehemu ya kutekeleza shughuli za ugani, kilisherehekea kwa furaha, vifijo na ndelemo ushindi mkubwa ambao Chuo kiliupata katika Maonesho ya Kilimo ya Nanenane Kanda ya Mashariki yaliyofanyika kuanzia tarehe 1- 8 Agosti 2022 katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro, Tanzania. Maonesho hayo hujumuisha mikoa minne ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, na Tanga.

Picha 1: Mh. George Simbachawene (Mb), Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, (akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatuma Mwasa, kushoto) kwa furaha akikabidhi moja ya kikombe ambacho SUA ilichoshinda kwa Prof. Maulidi Mwatawala, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Huduma za Ushauri), ambaye ameambatana na  Prof. Dismas Mwaseba (Kulia), Mkurugenzi Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) wakati wa sherehe za kilele cha Maonesho ya Nanenane  iliyofanyika tarehe Nane Agosti 2022 katika Viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere Nanenane, Morogoro. (Picha hii, kwa hisani ya SUAMEDIA).

 

Katika maonesho hayo ya Nanenane, 2022, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kilinyakua zawadi nne, ikiwemo kikombe na cheti cha mshindi wa kwanza katika kundi la Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati, na kikombe na cheti cha mshindi wa pili wa jumla. Chuo kilikabidhiwa zawadi hizo na Mh. George Simbachawene  katika sherehe ya kufunga rasmi maonenesho ya Nanenane iliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro. Maonesho hayo ya Nanenane yaliyofunguliwa rasmi na Mh. Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu mstaafu tarehe 4 Agosti 2022 yalibeba kauli mbiu ya “ Ajenda 10/30: Kilimo ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi”. Ajenda hiyo, kama ilivyofafanuliwa na mgeni rasmi ina lengo la kuhakikisha kuwa kufikia mwaka 2030 kilimo katika nchi yetu kinakua kwa asilimia 10. Ushindi wa SUA katika maonesho ya Nanenane mwaka 2022, uliibua shamrashamra za aina yake miongoni mwa wanajumuiya ya SUA na wadau wake.

Picha 2: Zawadi ya kikombe kwa SUA kama mshindi wa kwanza katika kundi la Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki ya mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro, Tanzania

 

Picha 3: Zawadi ya kikombe kwa SUA kama mshindi wa kwanza katika kundi la Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki ya mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro, Tanzania

 

Photo 4: Zawadi ya cheti cha mshindi wa kwanza kwa SUA katika kundi la Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki ya mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro, Tanzania

 

Photo 5: Zawadi ya cheti cha mshindi wa pili wa jumla ambayo SUA imeipata katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki ya mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro, Tanzania

 

 

Photo 6: Cheti cha ushiriki cha SUA katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki ya mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro, Tanzania

 

Picha 7: Prof. Raphael Chibunda, Makamu Mkuu wa SUA (katikati, mstari wa mbele) pamoja na managementi ya Chuo, wakionekana kujiamini kwa ushiriki wa SUA wenye mafanikio katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki kwa mwaka 2022 katika picha ya pamoja, muda mfupi baada ya Mh. Mizengo Pinda kumaliza kutembelea banda la SUA katika siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenan, Morogoro

 

Picha 8: Mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki Mh. Mizengo Pinda, (Kulia, mstari wa mbele) akitembelea banda la SUA katika siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo uliofanyika tarehe Nne Agosti 2022. Viongozi wengine walioambatana na mgeni rasmi ni pamoja na Mashimba Mashauri Ndaki (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi (katikati, mstari wa mbele), Mh. Fatuma Mwasa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Kulia, mstari wa pili), Prof. Raphael Chibunda, Makamu Mkuu wa Chuo cha  SUA (kushoto, mstari wa mbele), na Prof. Amandus Muhairwa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha SUA, Mipango, Fedha na Utawala(kushoto, mstari wa pili, aliyevaa suti nyeusi na tai).

 

 

Picha 9: Sehemu ya jumuiya na SUA na waoneshaji wakisherehekea kwa furahi ushindi mkubwa wa SUA wakiwa na Prof. Maulid Mwatawala, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu (Katikati, aliyevaa suti nyeusi) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la SUA la maonesho katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 10: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakipiga picha ya pomoja ndani ya jengo kuu la SUA la maonesha huku wakishangilia ushindi katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 11: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya banda la maonesha la Taasisi ya Kuthibiti Viumbehai Waharibifu, SUA (IPM) kwa ushindi wa SUA katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 12: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya maonesha ya maabara inayotembea ya Afya Moja, SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 13: Sehemu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya banda la maonesho la Shamba la Mafunzo la SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

 

Picha 14:  Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya banda la maonesha la Shirika lisiyokuwa la Kiserikali la “Kilimo Endelevu-SAT” (liliyoanzishwa na mhitimu wa SUA miaka mingi iliyopita) kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 15: Kwa kweli inafurahisha! Sehemu ya timu ya uratibu ya maonesho ya SUA kutoka Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) wakishangilia kwa furaha kubwa, hata kupata wakati mgumu kuendelea kushikilia zawadi mikononi mwao wakati wa kupiga picha katika banda la maonesha la SUA kusherehekea ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 16: Sehemu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele jirani na maonesho ya Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara na wahitamu wa SUA waliojiajiri kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 17: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha karibu na maonesha ya AICAD kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 18: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya maonesho ya malisho ya mifugo, na karibu na banda la maonesho la mifugo kwa ushindi wa SUA katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 19: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya banda la maonesho la Shule Kuu ya Uhandishi na Teknolojia, SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 20: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha mbele ya maonesha ya vipando ya Ndaki ya Kilimo, SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 21: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha karibu na maonesha ya Ndaki ya Sayansi Asilia na Sayansi Mtambuka, na Shule Kuu ya Elimu, SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 22: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha jirani na maonesha ya Ndaki ya Stadi za Awali, Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhamilishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam, na Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo, SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Picha 23: Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia wakati wa kupiga picha jirani ya maonesha ya maabara ya udongo inayotembea, Ndaki ya Kilimo (CoA) kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro

 

Photo 24: Jamani raha ya ushindi asikwambie mtu!

Sehemu ya timu ya waoneshaji wa SUA wakishangilia kwa furaha kubwa wakati wa kupiga picha mbele ya banda la maonesha la Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii, SUA kwa ushindi wa Chuo katika maonesho ya Nanenane kanda ya mashariki mwaka 2022 yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, Nanenane, Morogoro. (Picha zote katika andiko hili, ni kwa hisani ya mwandishi wa makala hii, isipokuwa Picha 1).

Hongereni sana Jumuiya ya SUA na wadau wote kwa ushindi wa kishindo!

Andiko hili pia linapatikana katika lugha ya Kingereza kwa kubofya alama ya lugha ya Kingereza katika tovuti ya ICE au kwa kubofya hapa: Taking Stock of SUA-Community Celebrations for Resounding Victory at 2022 Nanenane Agricultural Exhibition in Morogoro, Tanzania – Institute of Continuing Education – Sokoine University of Agriculture

Kutoka Ofisi ya Mkurugenzi,
Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE),
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)

Kwa maelezo zaidi kuhusu andiko hili tafadhali mwandikie Dk. Innocent Babili kwa barua pepe ibabili@sua.ac.tz