Mafunzo ya SUA na FAO Yachochea Kilimo Biashara kwa Vijana Mkoani Dodoma

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), waliotoa ufadhili wa fedha, walitoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu Ufugaji wa Kuku, na Uzalishaji na Utunzaji wa Miche ya Matunda Kibiashara mkoani Dodoma ili kuwapatia ujuzi wa kuweza kujiajiri au kuajiriwa. Video hii inaonesha miradi ya kilimo iliyoanzishwa na vijana baada ya kupata mafunzo hayo ya Kilimo Biashara.

Bofya hapa chini kuangalia video hiyo ya Kilimo Biashara: