Mafanikio ya Mafunzo kwa Vijana ya Uzalishaji wa Miche ya Matunda Kibiashara Yaanza Kudhihirika

Moja ya majukumu ya Taasisi ya Elimu ya Kijiendeleza (ICE), katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ni kutoa mafunzo ya muda mfupi.  Kwa kutoa mifano michache tu, mafunzo hayo ya muda mfupi huandaliwa kwa ajili ya kuwanufaisha wadau wa aina mbalimbali wakiwemo wakulima wa mazao, wafugaji, wajariliamali, watafiti, watunga sera, maafisa ugani, maafisa wa maendeleo ya jamii, wafanyakazi waliostaafu ajira rasmi, na vijana.

Picha: Washiriki  wa mafunzo ya uoteshaji na uzalishaji wa miche ya matunda kibiashara wakiwa katika ziara ya mafunzo katika bustani ya biashara ya miche ya matunda katika kata ya Magadu, Manispaa ya Morogoro

Tangu mwaka 2021 hadi 2022, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE) kimeendesha mafunzo ya muda mfupi ya Uoteshaji na Uzalishaji wa Miche ya Matunda Kibiashara. Tayari mafanikio ya aina mbalimbali yameaanza kupatikana kupitia utekelezaji wa mradi huu ambao umefadhiliwa na SWISSCONTACT ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali (NGO).  Kudhihirisha haya, anwani ya tovuti iliyoandikwa hapo chini inakupeleka kwenye video inayoonesha mafanikio yaliyofikiwa kupitia mafunzo hayo ya muda mfupi ya kuimarisha ujuzi na kuongeza ajira kwa vijana katika Manispaa ya Morogoro.

Tazama video kuona mafanikio yaliyofikiwa: https://www.youtube.com/watch?v=UyZ9GgK64-k&t=188s


Makala ya Kingereza ya andiko hili inapatikana hapa: https://www.ice.sua.ac.tz/highlighting-emerging-outcomes-of-training-on-horticulture-as-agribusiness-for-youths-employment/

Kwa habari zaidi kuhusu andiko hili mwandikie barua pepe Dk. Innocent Babili  kupitia anwani ibabili@sua.ac.tz