Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia apongeza jitihada zinazofanywa na SUA

Katibu mkuu wizara ya elimu sayansi na teknolojia Dr. Leonard Akwilapo amepongeza jitihada zinazofanywa na Uongozi wa Chuo kikuu cha sokoine cha Kilimo SUA kwa kushirikiana na serikali katika kuboresha miondombinu chuoni hapo.

Katibu mkuu huyo ameyesema hayo wakati akikagua jingo jipya la kulia chakula wananfunzi na wafanyakazi wa chuo linalojengwa kwa fedha za serikali kupitia wizara hiyo  pamoja na miundombinu ya umwagiliaji inayojengwa kwaajili ya kuwezesha upatikanaji wa maji ya kumwagilia bustani na mashamba ya chuo kama sehemu ya kufundishia wanafunzi na wakulima nchini.

Katibu mkuu wa wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo (Wa tatu kutoka kushoto) Akitoka kukagua jengo la kisasa la Chakula kwajili ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) lililojengwa kwa ufadhili wa wizara,kushoto kwake ni Makamu mkuu wa chuo Prof. Raphael Chibunda na wengine ni viongozi wa chuo walioambatana nae kwenye ziara hiyo fupi.

 

Kwa upande wake Makamu mkuu wa chuo Prof. Raphael Chibunda ameishukuru wizara kwa fedha hizo na kumhakikishia kuwa ujenzi wa jingo la kulia wanafunzi litakuwa tayari kabla ya mwezi wa sita mwaka huu ili kurahisisha wanafunzi kupata sehemu nzuri na ya kisasa kwaajili ya chakula.

Bwawa kubwa linalojengwa na SUA kwa lengo la kuhifadhi maji mwaka mzima ambayo yatatumika kumwagilia bustani na mazao mbalimbali yanayotarajiwa kulimwa katika eneo hilo kwaajili ya kufundishia wanafunzi lakini pia kusaidia watanzania kujifunza kilimo bora cha mazao mbalimbali.

Prof. Chibunda pia amemwambia Katibu mkuu huyo kuwa wameamua kujenga bwawa kubwa ambalo litahifadhi maji mengi cha zaidia ya lita za ujazo milioni 4 kwaajili ya kusaidia umwagiliaji wa bunstani na mashamba ya maonyesho ya chuo mwaka mzima sambamba  na kuchimba kisima kirefu cha mita mita 100  ili kusaidia shughuli hiyo.  Ili kukifanya chuo hicho cha kilimo kiweze kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa na bustani nzuri,mashamba ya mfano kwaajili ya kufundishia wanafunzi na wakulima kutoka maeneo yote nchini.