Kozi fupi

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) hutoa kozi fupi zinazoakisi nyanja mbalimbali za mafunzo yanayotolewa hapa SUA na Ndaki (colleges), Vituo, Taasisi, na Shule Kuu (School) zilizopo hapa Chuoni. Hizi ni pamoja na Ndaki ya Kilimo, Ndaki ya Tiba ya Mifugo na Sayansi ya Wanyama, Ndaki ya Misitu, Wanyama Pori na Utalii, Ndaki ya Solomon Mahlangu ya Sayansi na Elimu, Shule Kuu ya Uchumi Kilimo na Masomo ya Biashara, Kituo cha TEHAMA, na Kituo cha Wanyama Waharibifu.

Kozi zinazotolewa SUA hujumiisha zile zilizoandaliwa tayari, na zinazoandaliwa kutokana na maombi mahsusi ya mdau au wadau. Mifano ya kozi fupi zinazotolewa SUA ni kama ifuatavyo:

  • Ufugaji wa samaki
  • Uzalishaji wa mazao ya bustani, mboga na matunda
  • Usindikaji wa chakula
  • Ufugaji wa kuku
  • Ufugaji wa ng’ombe wa maziwa
  • Ufugaji wa mbuzi
  • Ufugaji wa sungura
  • Uzalishaji na tunzaji wa malisho ya mifugo
  • Takwimu
  • TEHAMA