SUAMEDIA Yaendelea Kung’ara Kwenye Tuzo Za Umahiri Katika Kilimo Nchini

Mwandishi wa Habari wa SUAMEDIA,Calvin Edward Gwabara ameibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa Televisheni kwenye tuzo za Umahiri wa uandishi wa habari za mazao lishe na Lishe Nchini na kuwabwaga waandishi kutoka vyombo vingine vya habari nchini kwenye upande wa Televisheni.

Josephine Mallango Mwandishi wa habari wa SUAMEDIA akipena mikono na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba wakati akipokea Tuzo ya Mshindi wa Kwanza upande wa Televisheni kwa niaba ya Mshindi wa tuzo hiyo Calvin Edward Gwabara huko jijini Arusha.

Tuzo hizo zimetolewa na mradi huo wa uimarishaji w a mazao lishe (BFNB) chini ya Kituo cha kinataifa cha  Viazi (CIP) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia kituo cha Utafiti wa mazao katika nchi za Kitropiki zimetolewa July 20 mwaka huu jijini Arusha na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba.

Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba akiipongeza SUAMEDIA kwa ushindi wa Kwanza kwa upande wa TV nchini kabla ya kumkabidhi Josephine Mallango cheti hicho cha Ushindi wa Kwanza kwa niaba ya Calvin Edward Gwabara.

Tuzo hizo ambazo ni kwa Mara ya Kwanza kutolewa hapa nchini zimehusisha washiriki kutoka vyombo vyote vya habari nchini na baadae kupatikana  washindi watatu kwenye Televisheni, Redio na Magazeti ambapo Pamoja na kupata cheti washindi pia walipewa zawadi ya Hundi kama mshindi wa Kwanza.

Hii ni tuzo ya Pili kwa mwaka huu kunyakuliwa na Mwandishi Calvin Edwadwa Gwabara ya Umahiri nchini kwenye kuandika habari na vipindi vinavyohusiana na masuala ya kilimo ambapo tuzo ya kwanza kwa mwaka huu aliinyakua mwezi wa tano kwa kuwa wa kwanza kwenye kipengele cha habari za kilimo upande wa Redio zilizotolewa na Baraza la habari Tanzania MCT kupitia tuzo za EJAT (Exellence in Jornalism Award Tanzania)