Tangazo La Mafunzo Ya Ufugaji Wa Samaki

Chuo kikuu cha sokoine  cha kilimo kwa kupitia idara ya sayansi ya wanyama,viumbe maji na malisho kimeandaa mafunzo ya ufugaji wa samaki yatakayofanyika kuanzia tarehe 02/05/2018 hadi tarehe 05/05/2018 katika ukumbi wa ICE uliopo kampasi kuu ya SUA

Ili kushiriki katika mafunzo haya mshiriki anatakiwa

  • Awe na uhitaji endelevu na nia ya dhati ya kutaka  kufuga samaki
  • Aliyeanza kufuga na anataka kupata mbinu za ufugaji zaidi

Idadi ya washiriki ni watu 30 tu, watakaowahi kuchukua fomu na wenye nia ya dhati ya kufuga samaki ndio watakaopewa kipaumbele. Mshiriki atajigharamia usafiri, malazi pamoja na chakula cha jioni. Fomu zinapatikana SUAMEDIA na ICE kampasi kuu ya SUA

 

Mafunzo ni bure wote mnakaribishwa

Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0768503292 au 0754370047

 

Kwa wanaotoka mbali, hostel zipo ICE SUA kwa bei nafuu kabisa