ICE NA SUAMEDIA NI KITOVU CHA UGANI

Ugani (Outreach) ni moja ya majukumu makuu ya manne ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), ambayo hujumuisha mafunzo, utafiti na huduma kwa jamii. Chuo hiki hutekeleza majukumu yake ya ugani kupitia Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza (ICE), ambayo ndiyo kiungo cha SUA na wadau mbalimbali ndani na nje ya Chuo.

Taasisi ya ICE iliyoanzishwa mwaka 1988 kupitia Tangazo la Serikali Na.25 imeundwa na vitengo vitatu. Vitengo hivyo ni Ugani, Elimu ya Kujiendeleza na Elimu kwa Jamii (Outreach, Continuing and Community Education), Huduma za kumbi za mikutano (Conference Services), na Vyombo vya Habari za Elimu (Education Communication Media). 

SUAMEDIA hufanya kazi chini ya kitengo kilichotajwa hapo mwishoni. Kitengo hiki ni kati ya nyenzo muhimu ambazo ICE na SUA kwa ujumla hutumia katika kutekeleza majukumu ya ugani. 

Historia ya SUAMEDIA inaanzia mwaka 1994 wakati Chuo kilipoanzisha televisheni iitwayo SUATV.  Miaka 11 baadaye (yaani mwaka 2015), Chuo kilianzisha redio ya masafa ya FM (SUAFM Radio); hivyo jina likabadilishwa kutoka SUATV kuwa SUAMEDIA.

Vyombo hivi hutangaza vipindi mbalimbali vya elimu, teknolojia, bunifu zilizozalishwa na SUA kwa kushirikiana na wadau wengine. Pia SUAMEDIA inavipindi vya shughuli za maendeleo kwa ujumla.

Vipindi vya SUAMEDIA huwalenga wakulima, wafugaji, wafanya biashara, wasindikaji na wadau mbalimbali katika mnyororo mzima wa thamani katika shughuli za kilimo, ufugaji na usimamizi wa maliasili. Pia, SUAMEDIA inavipindi murua vya michezo na burudani.

Hivyo, faidika na SUAMEDIA!

Angalia SUATV katika kingamuzi cha TING Channel 50.

Sikiliza Redio ya SUAFM katika masafa 101.1 FM