Mwandishi wa SUAMEDIA Calvin Gwabara aibuka mshindi wa Tuzo ya Mwandishi bora wa habari za Kilimo na Uchumi Kilimo

Mwandishi wa SUAMEDIA Calvin Edward Gwabara ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mwandishi bora wa habari za Kilimo na Uchumi Kilimo kwa upande wa Radio katika tuzo zilizoandaliwa na Baraza la Habari Tanzania MCT 2017. Mwandishi huyo Mwandamizi katika habari za Kilimo amepata Tuzo, Cheti na Zawadi ya fedha, kama mshindi wa Kwanza katika kipengele hicho. Katika tuzo hizo zaidi ya waandishi wa habari 470 kutoka vyombo tofautitofauti vya habari nchini walishiriki na baadae kuchujwa na kubakia 47 ambao waliingia kwenye fainali za kuwania tuzo hizo katika vipengele mbalimbali.

Mgeni rasmi katika tuzo hizo alikuwa Mwalimu. Nguli wa sheria Prof. Issa G. Shivji wakati jopo la majaji tisa liliongozwa na Mwandishi wa habari nguli Ndimara Tegambwage.

Hongera sana Bwa. Calvin E. Gwabara kwa ushindi huo na pia kwa kukibeba Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, SUA, katika shindano hilo adhimu katika tasnia ya Habari hapa nchini na duniani kwa ujumla.